Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Nimemsikiliza mara nyingi sana tena kwa makini sana mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu, mara zote amekuwa akiisisitiza Tume ya uchaguzi nchini, iendeshe uchaguzi mkuu ujao, katika njia ya uwazi, Uhuru na Haki.
Amezidi kusisitiza kuwa wanachowataka Tume hiyo ya uchaguzi ni kuendesha uchaguzi huu mkuu ujao, ukiwa huru na wa Haki. NOTHING MORE, NOTHING LESS.
Lakini cha kushangaza sana ni namna hilo takwa la huyo mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, ilnavyopokelewa na ule upande wa pili wa washindani wake, ambao ni CCM, kwa kurudisha maneno ya kejeli mno kwa huyo mgombea wa Urais kwa kudai kuwa anatumiwa na mabeberu wake, kuwa yeye ni msaliti wa nchi hii na yeye ni mtetezi wa mashoga na maneno mengine chungu mzima ya kashfa dhidi yake
Hebu nijaribu kuwauliza wanaccm, hivi mgombea wa kiti cha Urais kuitaka Tume ya uchaguzi ya Taifa itende haki katika kusimamia uchaguzi mkuu ujao, ni kosa kubwa hadi mgombea huyo aweze kutukanwa kiasi hicho na wanaccm?
Inaelekea nyinyi CCM mlikuwa mmekula njama na Tume hii ya uchaguzi ili wauendeshe uchaguzi huu, kwa njia isiyo ya Haki na Uhuru, ndiyo sababu ya nyinyi kutoa povu lote hilo mnaposisitizwa na Tundu Lissu kuwa uchaguzi ujao anawataka Tume ya uchaguzi kuuendesha katika njia ya Uhuru na Haki.
NOTHING MORE, NOTHING LESS, WHAT ARE OUR DEMANDS