Ni kwanini jamii ya wahindi imesahaulika kwenye teuzi za kisiasa?

Ulianza vizuri lakini ulinipoteza ulipotoa kauli ya ki mjomba Tom ya kuwa wahindi ni bora kuliko sisi.
Wapewe nafasi kama raia wengine lakini sio kwa sababu ya uhindi wao.

Amandla...
 
Zamani kulikuwa na mpaka walimu wenye asili ya Asia, siku hizi kuwakuta kwenye public service ni nadra sana. Sijui unampaje ukuu wa wilaya au mkoa!
 
Kwanini huulizi kwanini wahindi huwaoni 👇👇

  • Nurses huko zahanati ya kata
  • Walimu shule za kata
  • Police
  • Wanajeshi
  • Watumishi halmashauri huko
 
Nadhani hujajua usmart haupimwi kwa kuongoza darasani,unawezaje kusema watu ambao hawazidi mil 2 na wanamiliki zaidi ya asilimia sabini ya uchumi wote wa Tz ni vilaza?unajua wanamiliki zaidi ya asilimia sitini ya kampuni zote kubwa Tz?
Neno smart linatafsiri kubwa sana kwa kila namna hawa jamaa hawako kwenye category ya watu smart nabisha ilo na nitaendelea kubisha. Kinachowabeba ni unyenyekevu wao wakinafki wakitaka chao na ilo ndio linalowabeba, nchi ambayo huwezi tuma hela kwenda nje ya nchi kama sio ubinafsi ni nini?

Katika kitu wanachotuzidi ni Government support financial hapo wako vizuri sana kama ata simu wanaweza nunua kwa installment, mikopo kwao iko nje nje sana ata kwa wafanya biashara iko ndio wanachotuzidi na kinawapa kiburi kuja kwetu kuinvest.
 
Ni kwasababu jamii ya kiafrika nayo imesahaulika kwny teuzi huko india
 
Kwanini huulizi kwanini wahindi huwaoni [emoji116][emoji116]

  • Nurses huko zahanati ya kata
  • Walimu shule za kata
  • Police
  • Wanajeshi
  • Watumishi halmashauri huko
Professor pratap, hakuna kama yeye Tanzania nzima. Anafundisha Biology karibia vyuo vyote Tanzania , hasa UDSM na matawi yake yote, pia nasikia na Muhimbili anakwenda kufundisha. Ni Mtanzaniamhindi.
Kama wana vigezo na sifa wanayo badi wateuliwe.lakini wahindi wengi walioko Tanzania wanapenda biashara kuliko masomo. DSM kuna shule nyingi za wahindi mfano Indian School kule Temeke .lakini huwezi kukuta wahindi wanafika chuo kikuu, Ila kariakoo, Mlimani city, na Posta wenye maduka makubwa ni wahindi.
 
Umenitafakarisha katika Angle tofauti...! Wapo watu Weusi Marekani Wanajiita ' 'Black Americans' .. kiuhalisia hawa ni Wajukuu Wa Watumwa Waafrika waliopelekwa Kule Kipindi Cha Slave trade.... ! Hawa kuna haja gani huko waliko Kujiita 'Eti Black American Au Wengine Wananeutralise Kwa Kujipachika jina Diaspora'. .... Ulimbukeni Au Kujidharau Yaani Unapo Kwenu unatakiwa kuJivunia Kwenu lakini Umeng'ang'ania Kuishi Ardhi Ya Wenyewe, Jitafakari ....! Nyongo nshatoa...!
 
Nazungumzia shule za secondary za umma wewe unaleta stori zisizoeleweka.
 
#"BSc compture science".....ulifanyaje ukafika India?
 
Kwanza wahindi wa India sio hawa wa Tanzania, hawa ambao wapo Tanzania wengi si wahindu ama waisilamu wa Sunni, ni mashia na wengi sio Shia mainstream Bali ni minority ambao wapo Sponsored baadhi na uingereza ama Iran etc.

Mfano kama Ismailia ambao wapo wengi kiongozi wao ni Aga khan, yupo uingereza hawa waki graduate Tanzania wa naenda kokote Duniani alipo Muingereza, iwe Australia, Kenya, uingereza, Canada etc. Na elimu yao sio hii ya Necta wanasoma mitaala ya Uingereza.

Hawa ndio wameijenga Tanzania kuanzia
1. Jina lenyewe la Tanzania
2. Mahospitali makubwa kama Muhimbili na Amana
3. Mashule mbalimbali kama Tambaza, mzizima na mengine katikati ya jiji etc.

Nyerere mwenyewe hawa alikuwa akiwa respect sana.

Kuhusu usmart ndio wengi ni smart na wamesoma kuliko muhindi average uliyemkuta India, nawafahamu wengi wanashika vitengo vingi duniani, kuna mmoja namfahamu muda mrefu kagraduate hapa Tanzania then straight ameanza kazi the Hague.
 
India ubaguzi upo kwenye katiba, kuna watu wamezaliwa kuwa madobi tu, wengine wamezaliwa kuwa wafalme, wengine wamezaliwa kuwa wabeba mizigo etc. Mpaka kwenye daftari unaandika caste yako.

Hata hawa unaowaona Tanzania hawakubaliki na waisilamu wala wahindu ndio maana wame settle huku kwetu.
.
 
Ndio maana nasema wamepata priority ya kwenda nje wengi refer to story ya Victoria na Abdul, hawa jamaa hawa cha kutuzidi nitasimama kwenye ilo

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…