Ni kwanini jamii ya wahindi imesahaulika kwenye teuzi za kisiasa?

Ni kwanini jamii ya wahindi imesahaulika kwenye teuzi za kisiasa?

Ni moja ya swali huwa linanijia kichwani kila siku. Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimebahatika kuwa na hawa watu pamoja na nchi ya Kenya.

Jamii ya wahindi wa Tanzania na Kenya, wana historia ndefu kwa hizi nchi. Na wengi mpaka babu zao wamezaliwa huku, ikimaanisha wana haki zote za uraia wao wa Tanzania.

Binafsi, hawa watu nimefanikiwa kupambana nao shuleni, nimesoma na wahindi baadhi kuanzia sekondari na chuo nikibahatika kukutana nao. Na huku kwenye corporate world tunafanya nao kazi.

Kiufupi, hawa jamaa wapo smart sana na wanatuzidi kwa mbali sana sisi weusi. Moja kwa kwenye elimu, mbili kwenye management, tatu kwenye biashara.

Ukifananisha mabenki ya kihindi na yale yanayoongozwa na waswahili, utathibitisha nisemacho.

Dukuduku langu ni?? Kwanini wanasahaulika kwenye uongozi?????

Nchi kama Marekani na Uingereza, kwa miongo miwili iliyopita, jamii ya wahindi imekuwa ikipata chance sana kwenye management, na kikubwa ni kwasababu, wanajua.


Minister of Funance wa uingereza sasahivi anaitwa Rishi Sunak ni Muhindi halafu jamaa pia ana origin ya wagindi wa Tanzania na Kenya

Ceo wa Microsoft ni Muhindi Satya Nadella

CEO wa Google ni Muhindi

Na kuna makampuni mengine mengi America yanaongozwa na wahindi, maana yake ni kwamba hawa watu wana inborn quality kwenye management, na wanapaswa kutumiwa.

Huwa nahuzunika sana nikiona tuna hizi rasilimali watu ambazo hazitumiki ipasavyo.

Mnisamehe naandika bila mpango betri inaisha..
wajenge Kwanza.
wewe unasikiaga story za wafanyao job kwa wahindi? just asking
 
India ubaguzi upo kwenye katiba, kuna watu wamezaliwa kuwa madobi tu, wengine wamezaliwa kuwa wafalme, wengine wamezaliwa kuwa wabeba mizigo etc. Mpaka kwenye daftari unaandika caste yako.

Hata hawa unaowaona Tanzania hawakubaliki na waisilamu wala wahindu ndio maana wame settle huku kwetu.
.
Casts wanaita wenyewe ni watu wa ovyo sana sitaunga mkono wapewe cheo chochote kama wanaweza kubaguana wenyewe kwa wenyewe sisi watatufanyaje?!

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Napingana na wewe sana kwenye usmart hawa jamaa ni ovyo kabisa nimesoma nchini kwao hamna vilaza kama hao wanatusifia sana kwa waAfrica wenyewe akili, chuo nilichokuwepo tu kwenye notice board kulikuwa na waTz waliofanya vizuri na kuongoza kuzidi hao way back tena kwenye course ngumu kuliko zote hapo chuoni BSc Compture Science.
Walichotuzidi hamna zaidi ubinafsi na uchafu.

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
wahindi hawana akili?😲 Acha uduanzi. they are very bright of course not everyone of them.
 
Ndio maana nasema wamepata priority ya kwenda nje wengi refer to story ya Victoria na Abdul, hawa jamaa hawa cha kutuzidi nitasimama kwenye ilo

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
1.wamekuchagulia jina LA nchi, unajisifu mimi Mtanzania kwa jina alilokuchagulia mhindi
2. Wamekujengea hospitali yako ya Taifa
3.wamekujengea mashule makubwa makubwa
4. Makampuni makubwa nchi yako wanamiliki wao

Then unasema bila evidence yoyote hawana lolote?

Kwani kuna wa bongo wa ngapi nje? Je priority zao ni zipi? Tunao kina Jon Stephano waje watuambie.
 
Casts wanaita wenyewe ni watu wa ovyo sana sitaunga mkono wapewe cheo chochote kama wanaweza kubaguana wenyewe kwa wenyewe sisi watatufanyaje?!

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
Sababu wana kitu ambacho wewe huna, hao wazungu kwenye madini, dangote kwenye cement, wakenya mashuleni, MA CEO wa kigeni etc wote sio kwamba ni watu wa zuri, la hasha, Bali wana kitu ambacho sisi hatuna, iwe ni uzoefu, mtaji, uwezo etc.

Leo Simba toka naijua mimi haijawahi fanya vizuri bila MO, wakati MO ni mdhamini mwanzoni mwa miaka ya 2000 waliofanya vizuri, akaondoka timu ikawa mbovu, karudi timu imefanya vizuri tena, MO Ana nini? Ana pesa, timu inafanya vizuri Sababu anatoa hela, inawezekana akawa si mtu mzuri, ila pesa zake zinahitaji ka Kuinua mpira pale.

We hujaingia mtaani na sidhani hata kama Una biashara unafanya ila hawa jamaa wakisema wanaondoka trust me hata mafuta tunayojipaka tu mwilini utakosa pengine tukamue alizeti tupake, wapo behind nyuma ya wajasiriamali na industry nyingi hapa TZ.
 
Ukiwa na mfumo imara Wahindi ni rahisi kuwatumia vizuri sababu wana bidii na wanapenda kujipendekeza haswa kwa wazungu. Kwenye mifumo imara wanatumiwa vizuri tu kukuza uchumi na kuwa mawaziri,bankers kwa faida ya wote.Hapa kwetu watatupiga huku tukitoa ushirikiano.
 
Kwanini huulizi kwanini wahindi huwaoni 👇👇

  • Nurses huko zahanati ya kata
  • Walimu shule za kata
  • Police
  • Wanajeshi
  • Watumishi halmashauri huko
Mi pia namshangaa anakimbilia tu wapewe vyeo vikubwa wakat kaz ndogo hawataki
 
UKONSAHIHI, WAZIRI WA FEDHA, VIWANDA NA BIASHARA WA NYERERE, SOON AFTER INDEPENDENCE NI WAHINDI WALIKUWA.

Habib Jamali & Amir Jamal
Umelikoroga!! Waziri wa fedha muhindi kwenye cabinet ya Nyerere akiitwa Amir Jamal.. Hakukuwa na Waziri mwingine akiitwa Habib Jamal!!! Pia baadae alikuja Al Noor Kassum na Shamim Khan[ muhindi alikuja teuliwa naibu waziri]
 
Swali ni wao wanaamini ni waTZ?
Ikiwa hata kuchanganyika na wabongo tu ni wale wachache ndo hufanya hivyo tena wengi ni kama zimeruka kichwani,they don't care yani.
Pia waanze kukubali kuolewa na tuwaoe dada zao hapo ndo nafikiri tutajua pure ni wabongo otherwise baniani anaamini sisi ni watumwa wao
 
Akina Patel walustahili kuwekwa kwenye wizara zenye muelekeo wa biashara kama uwekezaji,viwanda na biashara na taasisi zake wakalete wawekezaji huko
 
Napingana na wewe sana kwenye usmart hawa jamaa ni ovyo kabisa nimesoma nchini kwao hamna vilaza kama hao wanatusifia sana kwa waAfrica wenyewe akili, chuo nilichokuwepo tu kwenye notice board kulikuwa na waTz waliofanya vizuri na kuongoza kuzidi hao way back tena kwenye course ngumu kuliko zote hapo chuoni BSc Compture Science.
Walichotuzidi hamna zaidi ubinafsi na uchafu.

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
Baada ya kusoma ulivumbua nini? Huenda hawakariri kwa umahiri kama wabongo lakini ni wavumbuzi wazuri
 
Wana vitu vya msingi vya kufanya.they are busy creating generational wealth for the next offsprings'offspring...hizi siasa watuachie wenye njaa😆
 
Uliona India waafrika wanateuliwa?
Ivi huko india mpo,usiwaone weusi kuliko sisi ukafikiri ni waafrika,hapa wengi wao waliopo wana historia hata kabla hatujapa uhuru na pengine wao walifika mwanzo katika ardhi hizi za Tanganyika na Zanzibar kabla ya sisi hatujahama katika misitu ya Congo,ndio waTz asili yetu tulipotokea huko.
 
Yaani Magufuli alimuona Professor Joyce Ndalichako kuwa anafaa kuwa waziri wa Elimu akashindwa kumuona Rakesh Rajan????

Inashangaza sana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaah
 
Kwanini huulizi kwanini wahindi huwaoni [emoji116][emoji116]

  • Nurses huko zahanati ya kata
  • Walimu shule za kata
  • Police
  • Wanajeshi
  • Watumishi halmashauri huko
Hatujatofautiana mawazo kabisa mkuu,
 
Back
Top Bottom