Ni kwanini Jina la YESU linafukuza mapepo tofauti na Jina Allah au Yehova?

Ni kwanini Jina la YESU linafukuza mapepo tofauti na Jina Allah au Yehova?

Ili kuelewa lazima ujue utatu mtakatifu Mungu Baba, Mungu mwana na Roho mtakatifu

Na tunatumia jina lake sababu alisema mwenyewe kuwa lolote muombalo kupitia jina langu naye Baba yangu awapeni

Jina la Mungu tunalitumia kwa muda maalum tu maana hata yeye muweza wa yote alisema usilitaje bure jina lake
MUNGU BABA,MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO NI FUNDISHO MAARYFU SANA ILA AJABU NI KUWA HAKUNA HATA VERSE MOJA KWA BIBLE INAFUNDISHA HIVI.
NI MANENO MATUPU TU YA WAKRISTO.
 
Salaam, shalom!!

Mods acheni mjadala huu upate majibu Toka Kwa wadau.

Nimeishi miaka mingi duniani Hadi sasa, na sijawahi kukutana na shehe au pastor akifukuza Roho chafu zilizowapagaa watu Kwa Jina la YEHOVA au Allah!!

Kwanini Jina YESU Lina nguvu kiasi hicho?

Karibuni🙏
Jina ni nembo tu ila nguvu inatumikaga ni ya kichawi hakuna uzito Wala muujiza wowote ktk jina Hilo
 
Huo mwili wa Yesu uko wapi?

Ulizikwa wapi?

Alifufuka na mwili wake, akapaa nao Mbinguni, sasa Mungu muweza wa yote ashindwe vipi kuvaa mwili na kuonekana kama mwanadamu?

Kumbuka, matusi hayajibiwi,

Karibu Kwa HOJA.
Kwani Maria mwili wake uko wapi? Na kaburi? Hamsomi ll. Mnarukiarukia tu mistari ya kitabu Cha watu. Matusi umeanza wewe.
 
Nikiwa high school kuna dogo alipandwa na pepo. Ndugu zetu wa makubadhi walikesha wanapiga dua hadi asubuhi bila majibu. Dogo alipigwa 'kwa jina la Yesu' kadhaa, akakaa sawa!
 
H aha.. Mtoa mada amesema kwanini jina la Yesu lina nguvu.. nadhani umetoka nje ya mada
Hiyo nguvu kwanini haikufanya kazi na kujitetea alipokua anasulubiwa na Wayahudi?

Hiyo nguvu ni imani tu wala haiwezi kuthibitishwa,ni sawa na wanavyoaminishwa kua maji ya upako yatawapa utajiri bila hata ya kua na mtaji wala kua na kazi,mafuta ya upako eti yatawapa Magari.

😀 😀
 
(Wafilipi 2:10-11)

Kila goti litapigwa Mbinguni na duniani na Kila ULIMI utakiri kuwa Yesu ni BWANA Kwa utukufu wa Mungu baba.

Sasa ndipo ujue kuwa Jina YESU ndilo JINA personal la Mungu.
We nae imeisha darasa la nne au?

Yesu atakuwaje Mungu!?

Ivi unaelewa kilichoandikwa hapo kwenye huo mstari?
 
Hiyo nguvu kwanini haikufanya kazi na kujitetea alipokua anasulubiwa na Wayahudi?

Hiyo nguvu ni imani tu wala haiwezi kuthibitishwa,ni sawa na wanavyoaminishwa kua maji ya upako yatawapa utajiri bila hata ya kua na mtaji wala kua na kazi,mafuta ya upako eti yatawapa Magari.

😀 😀
Mwenyewe alipanga hivyo.
Kama fomular ya kulizindua Agano Jipya.

Yohana 10:17
Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena.
18 Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.
 
Hiyo nguvu kwanini haikufanya kazi na kujitetea alipokua anasulubiwa na Wayahudi?

Hiyo nguvu ni imani tu wala haiwezi kuthibitishwa,ni sawa na wanavyoaminishwa kua maji ya upako yatawapa utajiri bila hata ya kua na mtaji,mafuta ya upako eti yatawapa Magari.

😀 😀
Hapo sawa.. Hujajiuuliza kwanini asulubiwe? Kwanini Mungu aandae mpango wa kuzaliwa kwake bila baba.. atume nabii anasaidia watu kupona na mwisho wake uwe kusulubiwa?

Kwanini azaliwe bila baba.. Kusaidia watu wake kwa magonjwa na mambo mengine.. Kwanini asulubiwe na kwanini alimpa isha mbinguni na kwanini atarudi?
Hiyo nguvu kwanini haikufanya kazi na kujitetea alipokua anasulubiwa na Wayahudi?

Hiyo nguvu ni imani tu wala haiwezi kuthibitishwa,ni sawa na wanavyoaminishwa kua maji ya upako yatawapa utajiri bila hata ya kua na mtaji wala kua na kazi,mafuta ya upako eti yatawapa Magari.

😀 😀
 
Sijui kwanini nashindwa kuelewa.. Mtu yupo radhi aamini kwamba duniani tumeumbwa mateso, kutenda dhambi..

Unashindwa kuamini kwamba Mungu alimtoa Yesu Kristo kwa dhambi za watu wote.. Kwamba wewe can literally live without sinning.. Bila magonjwa..

Nini ambacho ni kigumu kiamini
 
Jina ni nembo tu ila nguvu inatumikaga ni ya kichawi hakuna uzito Wala muujiza wowote ktk jina Hilo
Yaani uchawi utumie Jina la YESU Ili kupata Maslahi yepi sasa?

Yaani ufalme wa Giza utumie Jina la ufalme wa Nuru Kwa maslahi yepi?

Ufalme huo Si utakuwa umefitinika🤔
 
Mungu ni mmoja na YESU KRISTO ndilo jina lake.
Akiwa katika nafasi ya uumbaji tunasema Mungu Baba, akiwa katika nafasi ya ukombozi wa mwanadam tunamuita Mungu mwana (YESU).
Akiwa katika nafasi ya kufundisha kuufunulia ulimwengu juu ya siri zake tunamwita ROHO MTAKATIFU.

Mungu ni mmoja hakika
Amen!
Watu waanze kujifunza kuanzia hapa.
Qurani pia inamtambua Roho Mtakatifu, na Neno (Mwana)
Ila haisemi ni Miungu wawili.
 
Uyafukuze yaende wapi na Mungu ndiyo kayaumba kayaleta duniani tuishi nayo.
Sio kweli.. Kama wewe una amini kuhusu Mungu huwezi kuzungumza kauli kama hii..

Mungu ni mwema.. Hana sura mbili.. Sura yake ni moja.. Ni mwema.. Haiwezekani kubadilika kutoka hapo..

Sasa hawezi kuwa mwema alafu ukuletee mabaya.. Atakuwa ana kipinga na haki haimo ndani yake.. Kitu ambacho sio kweli
 
Mwenyewe alipanga hivyo.
Kama fomular ya kulizindua Agano Jipya.

Yohana 10:17
Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena.
18 Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.
Ila waafrika Mungu atusaidie tu, bible inaongelea wayahudi na waisrael tu hakuna jina la Mwaisa, Masawe, Shayo, wala hata Mbwambo.

Tumeshikilia vitabu vya dini as if sisi ndiyo tumeandikiwa wakati hata havituhusu hata kidogo.

Dini ni strategy ya kiutawala duniani ndy maana Roman Empire iliweza kuitawala dunia nzima kwa kupitia vitabu vya biblia na kueneza dini, wachina wameondoa maswala ya udini tangu Mao tse tung au Mao ze dong alipoichukua nchi na sasa waone kwenye uchumi wa dunia unavyowategemea, wamarekani na waingereza wameshaondoka kwenye sana za udini na ukabila sisi bado tunamijadala ya kuhusu jina la Yesu, mapepo yapo na yanaondolewa hata kwa matambiko ya kiafrika, NaN kwa majina ya mababu wa kiafrika Acha kuwa mtumwa wa kifikra bana
 
Wafilipi 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁹ Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
¹⁰ ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
¹¹ na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
 
Amen,

Yesu ni Jina la Mungu.

Ubarikiwe
 
Ila waafrika Mungu atusaidie tu, bible inaongelea wayahudi na waisrael tu hakuna jina la Mwaisa, Masawe, Shayo, wala hata Mbwambo.

Tumeshikilia vitabu vya dini as if sisi ndiyo tumeandikiwa wakati hata havituhusu hata kidogo.

Dini ni strategy ya kiutawala duniani ndy maana Roman Empire iliweza kuitawala dunia nzima kwa kupitia vitabu vya biblia na kueneza dini, wachina wameondoa maswala ya udini tangu Mao tse tung au Mao ze dong alipoichukua nchi na sasa waone kwenye uchumi wa dunia unavyowategemea, wamarekani na waingereza wameshaondoka kwenye sana za udini na ukabila sisi bado tunamijadala ya kuhusu jina la Yesu, mapepo yapo na yanaondolewa hata kwa matambiko ya kiafrika, NaN kwa majina ya mababu wa kiafrika Acha kuwa mtumwa wa kifikra bana
Hapa ndo mnapokosea! tatizo sio dini, tatizo ni hiyo imani ya kuchakachua iliyotengenzwa na warumi ili kutawala watu!
 
Back
Top Bottom