Ni kwanini Jina la YESU linafukuza mapepo tofauti na Jina Allah au Yehova?

Ase.. people are this blind🙌..

Inamaana kwa bandiko lako hili watu wamepotea?

Umesoma Biblia?
 
Ulimwengu wa mwili kuna mengi yamefichika na hasa kwa upande wa binadamu. Ndiposa tuna ambiwa kuwa kumkufuru baba Mungu au mwana kuna msamaha kama kufuru hiyo ikiungamwa na mhusika.
Lakini kumkufuru roho mtakatifu hakuna msamaha katika ulimwengu huu wala ule ujao.
Ulimwengu huu wa mwili kuna mapungufu mengi ya kutokupambanua ndiyo maana watu huchukuliwa na kila upepo wa kiimani kumhusu Mungu.
Mapepo (majini) ni ya daraja lingine juu ya mwanadamu katika mambo ya rohoni. Yana ufahamu juu ya mamlaka iliyopo ndani ya Jina la Yesu. Wanajua fika kuwa hawana hiari dhidi ya mamlaka iliyo nyuma ya jina la Yesu ila kutii.
Na pia wanajua mtu aliye na hayo mamlaka ya hili jina la Yesu na yule asiye nayo.
Hivyo anapoamrishwa na yule mwenye kupewa mamlaka ya kulitumia hana hiari ila kutii.
Mitume na manabii wote walikufa na miili yao ipo makaburini wakisubiri kufufuliwa siku ya kiama.
Lakini Yesu yeye aliye shangwe ya mbingu na tumaini la dunia, yuu hai milele na milele akiisha kufufuka kwa kushinda kifo na kaburi(mauti na kuzimu).
Malango yote ya kuzimu yaliyojitokeza baada ya uasi yamewekwa chini ya miguu ya Yesu na sii ya mwingine yeyote.
Adui wa mwisho katika haya malango ya kuzimu atakaye wekwa chini ya miguu ya Yesu na kuhitimishwa ni mauti katika ile kiama ya wafu.
Hayupo pepo awaye yote au malaika asiye anguka na kukiri kwa ulimi wake ya kwanba Yesu ni Bwana kwamba ni kwa uzima au kwa kudharauliwa milele.
 
Yaani ulivyo zungumzia Agano Jipya..

Hili hili la Matthew- ufunuo.. Asee

Doctrine ambayo inajenga Ukristo ni kuzaliwa kwake Yesu.. Kufa kwake.. Kufufuka kwake na kurudi kwake.. Ukiona unafundishwa nje ya hapa ujue upo katika njia ambayo sio sahihi na lazima upotoshwe..
 
Umeandika Ujinga Kwa kirefu sana.
 
Umeandika Ujinga Kwa kirefu.
Imani pasina maarifa n upuuzi,kwa hyo na wew unamsubiri Mwana wa Adamu aje na jeshi la malaika wake ili achukue wateule?,,,kwel Kam unamsubiri utasubiri sana ndgu usiye na maarifa
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa,unawafahamu waandishi wa agano jipya?
 
kwa hivyo hayo mapepo yaliyoondolewa na Yesu yalibaki kwa waafrika peke yao maana hatuoni wazungu wakiondolewa hayo mapepo
Wazungu mbona wanamapepo nao, au huangalii mahubiri ya Injiri ya huko Ulaya. T. B. Joshua kawatoa sana Mapepo wazungu. Kwa Jina la Yesu
 
Sasa,uliwahi kuona wapi ndugu wapendwa kuondoana au kufukuzana sehemu wanayopenda kujituliza kama kasuku?
 
Hivi mbona wenzetu hawatoi Mapepo ?
Yaani hata kuyakemea tu kiugomvi ugomvi hawayakemei.
Au huwa wanayauliza kwanza kama ni mema au maovu 🤔
Ninini kipo Nyuma ya pazia ?
 
Those about to die....
 
Sijawahi kumuona Papa anawatoa watu mapepo namuona kiboko ya wachiwi tu akitoa watu mapepo na kupiga laki 5 Kila kichwa
 
Yohana 1:1.,2.,3.,4.
1. Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. 4. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
 
Sijawahi kumuona Papa anawatoa watu mapepo namuona kiboko ya wachiwi tu akitoa watu mapepo na kupiga laki 5 Kila kichwa
unaijua exorcism

jana nilisema hivi.. Watu wengi wanapigwa kwasababu hawaijui kweli na wanaojua hawataki kufata principles..

lakini haimaanishi Ukristo ni uongo,porojo au siasa..

na kiukweli Ukristo sio dini ni maisha halisi
 
Yesu kusema ana mamlaka yote Mbinguni na Duniani hamwoni kuwa anaweza yote na ni Mungu tu mwenye hayo Mamlaka ?
.............
Mathayo 28:17
Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka.
18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
...........
Mwenye mamlaka yote ndiye mwanzilishi wa Kanisa, na kawapa Wafuasi wake funguo za Mbinguni.
...........
Mathayo 16:18
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
..............
Hamwoni kuwa wote mnastahili kuwa wanafunzi wake kama alivyo agiza?
..........
Mathayo 28:19
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
............
 
Na Jina la Roho mtakatifu, anaitwa Roho wa Yesu.

Na Jina la mwana ndiye Yesu Kristo.

Na Jina la baba ndilo Hilo Hilo pia Yesu KRISTO.
 
Sijawahi kumuona Papa anawatoa watu mapepo namuona kiboko ya wachiwi tu akitoa watu mapepo na kupiga laki 5 Kila kichwa
Sasa papa Si mkristo, ni kiongozi wa Dini ya kipagani. Waabudu sanamu.
 
Sasa papa Si mkristo, ni kiongozi wa Dini ya kipagani. Waabudu sanamu.
Papa asingedhibitiwa nina uhakika lengo lake lilikuwa ni kuwaozesha Mashoga Kanisani Roman Katoriki.
Alikuwa anakuja mdogo mdogo hadi Maaskofu wa huku Afrika walivyo mkemea.

Sasa Kiongozi kama huyo atapata wapi nguvu za Roho Mtakatifu za Kuyafukuza Mapepo ?
Lazima uwe na Ushirika wa kweli na Yesu Kristo, ndio uwe na uwezo wa Kuyakemea Mapepo na Yakakutii.

Simuhukumu Papa ila maamuzi yake yanathibitisha kuwa Yupo mbali na Yesu Kristo na anatakiwa kutubu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…