Ni kwanini kila migogoro ikitokea Dangote Cement lazima Obasanjo atue nchini?

Ni kwanini kila migogoro ikitokea Dangote Cement lazima Obasanjo atue nchini?

Kama ni mfatiliaji mzuri wa Matajiri wa Nigeria akina Mike Adenuga hutasitajabishwa na Obasanjo kuja Ku solve mgogoro wa hicho kiwanda.

Matajiri wa Nigeria wanasema utajiri wa Dangote umejaa hadaa,na tenda nyingi alikuwa anapata kwa njia ya rushwa na upendeleo kutoka Serikalini hasa kipindi cha Obasanjo na Jonathan.

Kwa hiyo connect dot.
 
Vijana wa JF bwana mnapigana jeki naona

Sasa unadhani huyo mama hakusema kuwa ni mke wa Olisegun au??

Au mlikua hamfwatilii bado maswala ya nchi ndo mmeanza juzi???

Halafu mnajua umri wa Sky Eclat ???

Wengine humu wanamtania Obasanjo ndo rika lao......kaeni kwa kutulia

NB: Hata mimi nilimshuhudia huyo maza akilalamika. Na anakaa mbezi beach mpaka leo hii yupo Tanzania hii
Hata kama...haikupi guarantee ya kumtania mzee na aliyewahi kuwa kiongozi wa kitaifa. Mambo ya wanawake yapo kila mahali duniani refer Monica Lewinsky wa USA.
Nikukumbushe tu utani wa idris sultan ulipomfikisha.
Tujifunze kuwa na kiasi kwa kila jambo.
 
Hakuna sehemu alipotaniwa. Kasema kuna mama alisema ni mkewake ila kwenye listi ya wake wa Babu hayupo

Ila huyo mama yupo na ni kweli alisema

Idris Sultan unaongelea mambo Yale Yale ya kupigana biti enzi zile zilizoishia Mwezi March??

Kama mambo ya wanawake yapo unatolea na mfano wa Bill na Monica yalikyowisha kuongelewa kwenye vyombo vya habari huoni unajipinga mkuu?
 
Wasalaam Wakuu,

Hivi ni kwanini kila kunapotokea changamoto/mgogoro kwenye kiwanda cha Dangote Cement Mtwara basi ndani ya siku chache tu lazima Rais Mstaafu wa Nigeria Obasanjo atue nchini na kuzungumza na Mkuu wa Nchi?

Ilitokea hili mara mbili wakati wa Rais Hayati Magufuli, na hivi majuzi badala ya mgogoro wa kiwanda na madereva nasikia leo hii Obasanjo ameonana na kufanya mazungumzo na Rais Mama Samia.

Kuna nini nyuma ya pazia Kati ya Dangote Group na Obasanjo?
Obasanjo ni broker wa siasa na uchumi kwa nchi ya nigeria
 
Wasalaam Wakuu,

Hivi ni kwanini kila kunapotokea changamoto/mgogoro kwenye kiwanda cha Dangote Cement Mtwara basi ndani ya siku chache tu lazima Rais Mstaafu wa Nigeria Obasanjo atue nchini na kuzungumza na Mkuu wa Nchi?

Ilitokea hili mara mbili wakati wa Rais Hayati Magufuli, na hivi majuzi badala ya mgogoro wa kiwanda na madereva nasikia leo hii Obasanjo ameonana na kufanya mazungumzo na Rais Mama Samia.

Kuna nini nyuma ya pazia Kati ya Dangote Group na Obasanjo?
Niliwahi kusoma somewhere makala inayomhusu Mzee Olusegun na maisha yake baada ya kustaafu kwamba he's ready to go anywhere, to meet anyone, to talk anything provided that you've met his fee!
 
Ninakumbuka awamu ya nne kuna mama Mtanzania alisema yeye ni mke wa Mzee Obasanjo na alitapeliwa kiwanja wakati anataka kuwekeza Tanzania.

Lakini katika profile ya Obasanjo hakuna maelezo ya kuwa na mke Mtanzania. Inawezekana mama ni mpango wa kando.

Huyu mzee ni shemeji yetu.
Obasanjo alishapata kesi ya kutafuna mke wa mwanawe wa kumzaa
 
Ni kawaida sana kuweka mwenyekiti board au hata shares fulani kumilikiwa na rais au wanasiasa wenye nguvu .....naamini wame solve issueiliyopo mbele yao hasa mgomo huko kiwandani
 
Amevaa sandals mkuu hahitaji soksi
Ukishakuwa mtu mzima hivyo viatu binasumbua miguu...inavimba shida nini ? Unataka avae buti kabisa na kamba zake ? Hao wazee wanakuwa washauri tu sasa wanakula maisha...
 
Matajiri wengi huwa wanawapa hisa au vyeo Marais wastaafu au mawaziri wakuu kwa mambo kama haya na pia kampuni kuaminika zaidi.

Jambo la kawaida sana wakubwa kuwa Directors.
Hapo ndiyo ujuwe ufisadi Africa hautakwisha kwa mtindo huo!!
 
Nishakutana na wa naijeria Kam wa 3 hiv seem tofaut tofaut unapofany nao mazungumzo ukawaambia dangote ndo tajir mkubwa naijeria wanakataa wanasema Hana hela yule no ujanja ujana tu
 
Hata kama...haikupi guarantee ya kumtania mzee na aliyewahi kuwa kiongozi wa kitaifa. Mambo ya wanawake yapo kila mahali duniani refer Monica Lewinsky wa USA.
Nikukumbushe tu utani wa idris sultan ulipomfikisha.
Tujifunze kuwa na kiasi kwa kila jambo.
Acha kumtisha mwenzako afterall mtu anatumia fake ID bado unamuandama kwa vitisho, au wewe ni mama yake na huyo mama mchepuko wa obasanjo?
 
Ninakumbuka awamu ya nne kuna mama Mtanzania alisema yeye ni mke wa Mzee Obasanjo na alitapeliwa kiwanja wakati anataka kuwekeza Tanzania.

Lakini katika profile ya Obasanjo hakuna maelezo ya kuwa na mke Mtanzania. Inawezekana mama ni mpango wa kando.

Huyu mzee ni shemeji yetu.

Hata wewe unataka kumchafua Bi mkubwa??!!
 
Hapo unatakiwa kuelewa wenzetu ni majasusi wa kiuchumi!

Unaweza dhani Dangote ndo mwenye kiwanda kumbe serikali ya Nigeria ndo inamiliki hivyo viwanda,

Unaweza kuta Dangote ni share holder tu!
Sisi tumeshindwa kukuza vyaketu hata ndani,wenzetu wanavuka mipaka kwa usaidizi wa serikali zao,siku tukiamka usingizini wenzetu wanakula cha mchana kama sii cha jioni.
 
Back
Top Bottom