Hamtaki kumuelewa tuu mleta mada. Imekuwa ni kawaida sherehe hizi kufanyika makao makuu ya nchi, hivyo ingekuwa sio ajabu ingefanyikia Dodoma.
Lakini hata hivyo yanaweza kufanyika nje ya makao makuu ya nchi, lakini lazima yakafanyike mahali ambapo pana historia ya jambo lenyewe, yaani UHURU. Mfano Tabora, sababu zingekuwepo zinazohusiana na harakati za Uhuru.
Sasa Mwanza kuna lolote limesha tajwa kuifunganisha na Uhuru?
Hapo ujue Magufuli kaamka asubuhi moja na kusema Mwanza! Na hakuna wa kuhoji, kushauri au kupinga. Full serikali ni makondoo tuu, kila utakaye mhoji atakuambia rais kasema.
Taifa gani linalokwenda kama kundi la kondoo hili?