Huwa nalisikia tu hilo la Mwalimu "Nyerere kuonya" juu ya makabila fulani...lakini sijawahi kuona ushahidi wa maandishi au hotuba juu ya hilo.
Sikatai, inawezekana alifanya hivyo kwa sababu alizoziona yeye kwa wakati huo.
Lakini sikubaliani na dhana ya kulishikia hilo onyo, liwe kama ni jadi isiyoweza kubadilika. Tulipokuwa tumekwishafikia kama taifa wakati Mwalimu Nyerere anatuaga, ni dhahiri tulikuwa tumepiga hatua kubwa ya kutosha ya kuendelea kukumbatia dhana ya ukabila kuturudisha nyuma, na hivyo itulazimu kuendelea kushikilia 'onyo' alilotoa Mwalimu wakati ule.
Kazi pekee tuliyokuwa tumebakiwa nayo kuifanya ni kuchambua kwa makini mTanzania yeyote anayejitokeza kuwa kiongozi wetu bila ya kujali kabila analotoka.
Sisi kazi hiyo imetushinda, na matokeo yake ndio haya tunayoyaona sasa.