BUSH BIN LADEN
JF-Expert Member
- Mar 16, 2019
- 9,121
- 20,814
Hapa G sam umewaza kama mrembo anaekunwa G-Spot.
Hata sifahamu, maana sina kabila wenye makabila wataeleza vizuri.Kumbe chato ni kwa wahaya sio wasukuma ....
Si ajabu huo ndio mwisho wako wa kufikiri.Naona akili yako iko na tope kidogo.
Yatakapofanyika Chato uje uulizwe hili swali tena mkuu. Natamani JK angehamishia shughuli kama hii Chalinze ili nipate maoni yako.Kwani Mwanza Ni sehemu ya Ujerumani?
Hivi huwa kuna ushahidi wowowte kuonyesha Nyerere aliwahi kuayasema makabila hayo au Uvumi tu nishatafuta andiko sauti video sijawahi ila alionya kuhusu ukabila lakini sikuwahi ona akiyatamka bayana na kama angaliesema basi angeliwataja wasukuma kwa sababu walitaka sukumaland federation iendelee na pengine leo tungekuwa na nchi kama Lesotho na yeye akaona mbali ndiyo chanzo cha uchifu kufutwa au kutokuwa sehemu ya serikaliSina shida na watu wa kabila lile mkuu. Mbona hata wapinzani wakienda kule wanapokewa vizuri tu? Nina shida na huyo aliyepeleka sherehe huko! In fact anafanya wasukuma wenzake waanze kufikiriwa tofauti ingawa najua wapo wasiopendezwa na haya. Nakupa mfano wachaga, wahaya, wanyakyusa na wasukuma Nyerere aliwahi kutuonya kuwa wametawaliwa na ubinafsi. Sasa hatukuwahi kumpata Rais kwenye makabila hayo hapo kabla ila sasa tumempata Magufuli na ameenda mulemule alikoonya Nyerere. Hii inajenga taswira kwamba tumeshakanyaga nyoka sasa siku tukiona jani tushtuke! Kusema kweli hapo kabla sikutegemea kuona haya ninayoyaona. Mpaka huwa najiuliza hivi kuna watu huwa hawaoni aibu?
Tofauti ni kubwa. Mleta mada hajaelewa kwamba maandishi ni sawa na maneno yatokayo mdomoni, siku zote huumba.Akheri ungesema "mleta mada kakariri kwamba 'Mwanza ni kanda'", ambayo sio kweli. Mimi naona yeye na wewe hamtofautiani sana kwa mitazamo yenu.
Ww Ni mpuuzi, trust meHamuwezi kuelewa ila mwenyekiti wenu ni mtu anayetukuza ukanda kwenye mambo ya kitaifa.
Sio wote mkuuMara nyingine Magufuli mnamuonea bure. Mnafahamu fika Chato ilikuwa Kagera, Kagera wana jadi yao na Mwanza jadi yao iweje leo eti Magufuli anatoka kabila la Mwanza? Hata kama bado hajavuka mipaka ya nchi.
Halafu watu wa Dar es Salaam na Arusha nimegundua hampendi maendeleo yapelekwe sehemu nyingine za nchi. Ningelikuwa Magufuli kwanza Dar es Salaam ningeifuta kwenye ramani ya taifa hili maana ndio chanzo cha umaskini sehemu nyingine za taifa hili.
Kama mnaona ukanda basi peleka mswada bungeni tuwe na states ambazo zitasimama Kama Kanda uione mtavyoburuzwa.
Watu wa ajabu sana nyie.
Mtu wa ajabu sana ni wewe. Eti ningekuwa Rais Dar es Salaam naifuta, unaifutaje kwa mfano?Mara nyingine Magufuli mnamuonea bure. Mnafahamu fika Chato ilikuwa Kagera, Kagera wana jadi yao na Mwanza jadi yao iweje leo eti Magufuli anatoka kabila la Mwanza? Hata kama bado hajavuka mipaka ya nchi.
Halafu watu wa Dar es Salaam na Arusha nimegundua hampendi maendeleo yapelekwe sehemu nyingine za nchi. Ningelikuwa Magufuli kwanza Dar es Salaam ningeifuta kwenye ramani ya taifa hili maana ndio chanzo cha umaskini sehemu nyingine za taifa hili.
Kama mnaona ukanda basi peleka mswada bungeni tuwe na states ambazo zitasimama Kama Kanda uione mtavyoburuzwa.
Watu wa ajabu sana nyie.
Siku zote, hata katika mataifa mengine sherehe kama hii hufanyika makao makuu ya nchi. Unatakiwa kufahamu hilo. Hii ndiyo sababu hakuna kipindi chochote cha utawala wa Marais wengine, sherehe hizi ziliwahi kupelekwa mahali pengine popote zaidi ya mahali yalipo makao makuu ya serikali. Au sasa hizi makao makuu yapo Mwanza?Hii hoja hapana, nadhani mleta mada kama kuna kitu tofauti tuambie, vinginevyo acha ifanyike popote hii ni sherehe kama zingine.
Siyo kila kitu kinaongozwa na sheria. Kuna mambo mengi tu yanafanyika hakuna sheria. Kunapokuwa hakuna sheria ya moha kwa moja kuelekeza jambo fulani, hekima, busara, utamaduni na mazoea huzingatiwa.Ni sheria ipi iliyovunjwa mkuu. Hayo ni maadhimisho tu mkuu, na sio sherehe halisi za Uhuru wa Tanganyika. Kumbuka hatupo mwaka 1961 , huu ni waka 2019. Ukitaka hata Moshi kule Marangu inaweza fanyika alimradi ni sehemu ya Jamhuri.
Unaelewa gharama zinazotumika kuhamisha sherehe kama hizo kufanyika eneo tofauti kila mwaka?mkuu sherehe za uhuru kufanyika Mwanza imekuwa nongwa? nlidhani Magu anahitaji pongezi kwa kuondoa mazoea ya sherehe hiyo kufanyika sehemu moja tu mwakani Iringa au Mbeya au Tanga au Kigoma nk
Wewe unayewaza kwa angle ya Kanda na Kabila ndo mkabila. Kwani Mwanza sio Tanzania.Huku kukiwa na lundo la tuhuma kuwa utawala wa awamu ya tano umegubikwa na ubaguzi wa kikanda hatimaye Rais John Pombe Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Sherehe hizo kwa mara ya kwanza zinafanyika nje ya makao makuu ya nchi ukiachilia mbali serikali ilipohamia Dodoma.
Swali la msingi ni kwanini sherehe hizo ziende jijini Mwaanza eneo ambalo limetawaliwa na kabila atokalo Rais Magufuli? Ni hoja gani hasa iliyotumika kuzipeleka jijini humo?
Ni jambo la ajabu kuona serikali ikikumbatia waziwazi upendeleo wa ukanda! Haya yanayofanywa yanatupa sisi ari ya kujiridhisha kuwa tumetawaliwa na upendeleo wa waziwazi wa kikabila awamu hii ya uongozi.
Kwa maana hiyo sasa jeshi, viongozi wote wa juu pamoja na wageni wanapelekwa Mwanza ili kuhudhuria sherehe za uhuru.
Siwezi kusema mengine yaliyotokea huko nyuma katika utawala huu yakionyesha mwenendo mbaya wa kikabila ila kiukweli jambo hili halileti picha nzuri hata kidogo.
Hii ni Tanzania imejengwa ila kiobomoa ni kazi rahisi sana.
Kama kilivyo chama kinatukuza Ukabila na kuuvisha joho la Ukanda ili kuvicha ukweli.Hamuwezi kuelewa ila mwenyekiti wenu ni mtu anayetukuza ukanda kwenye mambo ya kitaifa.
Ngoja tumkumbushe mleta mada.Uzi wa kijinga sana. Yaani jitu zima linalalamika kwa nini mwanza ambako hawajawahi kuwa nazo sasa wamekumbukwa..ufipa mmelaaniwa. Mwanza ni tanzania na wana haki. Msiwe wakabila kiasi hicho kwamba kanda ya ziwa wakipata kama watanzania basi wamependelewa.
Kwani Mwanza hawakupigania Uhuru kama Wachaga?Hamtaki kumuelewa tuu mleta mada. Imekuwa ni kawaida sherehe hizi kufanyika makao makuu ya nchi, hivyo ingekuwa sio ajabu ingefanyikia Dodoma.
Lakini hata hivyo yanaweza kufanyika nje ya makao makuu ya nchi, lakini lazima yakafanyike mahali ambapo pana historia ya jambo lenyewe, yaani UHURU. Mfano Tabora, sababu zingekuwepo zinazohusiana na harakati za Uhuru.
Sasa Mwanza kuna lolote limesha tajwa kuifunganisha na Uhuru?
Hapo ujue Magufuli kaamka asubuhi moja na kusema Mwanza! Na hakuna wa kuhoji, kushauri au kupinga. Full serikali ni makondoo tuu, kila utakaye mhoji atakuambia rais kasema.
Taifa gani linalokwenda kama kundi la kondoo hili?
Kwani Sheria inasemaje?Ilihamishiwa Dodoma kwakuwa yaliandaliwa kuwa makao makuu ya serikali. HUKO MWANZA KUNA MAKAO MAKUU YA SERIKALI?