Ni kwanini serikali imeshindwa kuwaajiri wahitimu wa fani za mafuta na gesi pamoja na uchache wao?

Kipindi kile watu walilishwa upepo wakijua wataenda kwenye rig na Mandatory Course za STCW 95. Kozi za awali za kufanya kazi kwenye rig zinatolewa na South Africa sisi tulikimbilia kuanzisha kozi kubwa za kiutawala na kusahau watendaji wa chini.

Kweli mkuu, saizi pale DMI wameanzisha degree ya Offshore na masuala ya gesi. Wanafunzi watamaliza bila kwenda kwenye Rig.

Kwenye Rig kuna kazi kibao za chini ambazo tungepata wajuzi zaidi. Kuna Banksman,Rigger,Jack up, Sweepers,watu wa rescue, Helicopter operation za under water na uokozi juu ya meli
Zile STWCs za DMI zinatambulika kweli Kimataifa naziogopa
 
Ahsante kwa ushauri mzuri. Sasa wewe mfano ukipewa uongozi kwenye hiyo sekta maana yake hutoweza kufanya mabadiliko yeyote kwasababu wengine wameshindwa?
Ccm sio kwamba wameshindwa,hawataki,Kuna ufisadi mkubwa kwenye hiyo miradi,tujiulize kitu kidogo tu,kwanini mpaka leo Bado tunaagiza mafuta ya kula,sukari,ngano kutoka nje?
Jibu,Kuna watu wakubwa tu wanafanya biashara za kuagiza sukari na mafuta kutoka nje,sasa kama hizo bidhaa zitapatikana hapa,wao watafanya biashara gani?lazima watazuia sekta ya sukari isikue.
Sie tuna gesi kutoka mtwara,kwanini mtungi wa gesi usiwe shilingi 5000!,
Umeishawahi kujiuliza kwanini TTCL upo hoi inazidiwa na makampuni yote hata yalitokuja jana,kama halotel?
Nikudokezee kidogo,TTCL inauza internet,link,ISPkwa makampuni kama raha.com,nk,sasa ukipewa link ya ttcl inakuwa inasumbua,lakini ukichukua link kutoka Raha .com,inakuwa poa!
Wakurugenzi wa ttcl ndio wanaomiriki raha.com,sasa wanaona bora waihujumu ttcl,Ili kampuni zao binafsi zipate kazi.
 
Kuna kozi bongo sio za kusoma.

Unasoma kozi za mafuta kwani Tanzania ina mafuta ama inachimba mafuta? Hizo fani ni dili sana huko uarabuni ila bongo ni kupoteza muda wako.

Unasoma unakuja kusubiri uajiriwe na serikali.

Ilikua kidogo niuvae ama niingie cha kike kusoma kozi za kisiasa.

Shemeji yangu aliuvaa mkenge wa kisiasa akasoma kozi inaitwa law enforcement pale UD, hadi sasa anauza juice ya miwa mtaani maana sio mwanasheria sio nani.

Kozi kama hizo za kisiasa na procurement sio za kusoma tena sasa ulimwengu huu.

Tuhamie kwenye IT, Finance(sio accounting) Investment, Projects, Electronics, Electrical, Civil engineering, Architect, Law, Computer nk.

Mimi kwa sasa simshauri mtu kusoma kozi nje ya hizo.
Economics /agro economics/Marketing mkuu
 
Zile STWCs za DMI zinatambulika kweli Kimataifa naziogopa
Ipo kwenye white list za IMO ila kwenye nchi za Dunia ya kwanza hutoweza kupanda meli zilizosajiliwa kwenye mataifa makubwa.

Tanzania pia hatuna Memorandum of Understanding (MoU) na mataifa mengi makubwa. Hivyo wanapelekea kugomea vyeti vyetu maana kwenye Mou mnashare mpaka mitaala na mifumo mingi. Sisi tuna MoU na South Africa, ingawa wao wame fanya mabadiliko tena ya mtaala.

Mfano mzuri Ghana mwaka jana wameingia MoU na Uingereza. Hivyo ukisoma chuo cha Ghana Maritime cheti kinatambulika UK, na mitihani wanashare na mtaala.
 
Acheni kusomesha watoto ngazi ya degree. Watoto waishie f4 kisha wapelekeni veta. Mkifuata ushauri huu mtanishukuru.
Unataka watu wote wawe fundi cheleani, mapambo, umeme nk bado watakwama huko mbele, angalia walimu ni mwaka wa 4 wakomtaani
 
Mkuu wa makampuni ukiingia Mjengoni kawaambie wenzio haya.

01. Sera zetu haziaminiki hata kwa week moja. Huwezi jua kesho itakuwaje. Kwa hiyo uwekezaji mkubwa hautakuwepo.
02. Huko kwenye oil and gas, serikali lazima ifanye kazi ya kupeleka vijana kama cheap labour mambele huko ili kupata uzoefu na technology( iwe ni programme rasmi kama wanavyofanya kwenye kilimo). Nilishangaa siku moja nilipojua kuwa wapiga xray wako wawili tu Bongo. Sijui kama wameongezeka sasa hivi.
03. Google Bonn Island Nigeria ( pale kuna chuo cha local people), madogo wa pale ambao ni vichwa wanakulia kwenye plant kubwa na kuna VETA pale pale ya mambo ya gas na Oil tu, humo kuna kila takataka ihusiyo oil na gas. hawa madogo hawasomi habari za Kilimo cha Buni Burundi, wao ni gas oil tu. Shell ndo wanamiliki ile facility, dogo akipasua vizuri, basi anaingia Shell international. Hivyo, fundi huyo akipelekwa duniani kwenye mitambo ya Shell atachukua fundi wa kwao sbb ana uhakika kapita kwenye tanuru la ukweli. Bila taasisi ndogo za hivi ni mtihani kuingia soko la Kimataifa.
04. Tupunguze bla bla kwenye mambo ya msingi kwa Taifa letu. Aliyeua TIPER/AGIP hakuwa na uzalendo kwa nchi yetu hasa kizazi cha wapenda petrol ( tulioiona TIPER na AGIP) tunasikitika ilivyopotea na kuhamia kwa majirani hapo chini. Walikuwa jiko la taaluma ya petrol, wakimiliki refinery, lubricants processing plant, Agip Dar (ilikuwa meli), Bitumen Emulsion Plant, Natural Gas ( hata ya Songo Songo walichimba wao vile visima kwa ushirika na TPDC), Motel Agip kwa wahenga, palikuwa na disco la kufa mtu pale. Vituo vya mafuta na depot za kutosha.
 
Ahsante sana kwa andiko zuri.
 
Nadhani mleta uzi ni mhanga wa haya ma petroleum nini nini. Petroleum walianza kudahili mwaka 2010 pale Udom. Petroleum engineering. Wale vijana walikuwa 13 kama sikosei.

Shida kubwa iliyowakumba watu wa petroleum ni ile kujiona kwa uchache wao basi wao ni Ajira direct. Basi wakaanza kujiona wao ni watu flani hivi special.

Mambo yalivokuja kuwa ndivo sivyo, wakaanza kuona wao ndo wameonewa vibaya. Ndio matokeo ya nyuzi kama hizi.

Naomba nikusanue mleta uzi, wala hata usilaumu serikali wala bunge. Ajira ni ngumu, haijalishi ni ajira gani. Lakini pia nikukumbushe, kuna wana wamekula mashavu huko huko kwenye petroli wemeenda mpaka ughaibuni. Kwahyo mzani uko vilevile.
 
Noamba zungumza kama wewe ndio kiongozi boss, zungumza kisera. Kusema walikua wanajiona ni watu special hapo unazungumza kama matatizo yanayohusu sekta zetu hayakuhusu. Hivyo hata ukipewa uongozi kuna baadhi ya matatizo hutawajibika kwasababu ya sababu zako binafsi.
 
Law enforcement inatakiwa kusomwa na askari walio kazini tayari
Kuna kozi bongo sio za kusoma.

Unasoma kozi za mafuta kwani Tanzania ina mafuta ama inachimba mafuta? Hizo fani ni dili sana huko uarabuni ila bongo ni kupoteza muda wako.

Unasoma unakuja kusubiri uajiriwe na serikali.

Ilikua kidogo niuvae ama niingie cha kike kusoma kozi za kisiasa.

Shemeji yangu aliuvaa mkenge wa kisiasa akasoma kozi inaitwa law enforcement pale UD, hadi sasa anauza juice ya miwa mtaani maana sio mwanasheria sio nani.

Kozi kama hizo za kisiasa na procurement sio za kusoma tena sasa ulimwengu huu.

Tuhamie kwenye IT, Finance(sio accounting) Investment, Projects, Electronics, Electrical, Civil engineering, Architect, Law, Computer nk.

Mimi kwa sasa simshauri mtu kusoma kozi nje ya hizo.
 
Law enforcement inatakiwa kusomwa na askari walio kazini tayari
Sasa ile kozi ilianzishwa kwa ajili ya fresh students pale UD na ikapigiwa debe balaa. Ilikua initiative za Saidi Mwema yule IGP.

Kozi ilipaswa kusema toka mwanzo kwamba ni maalum kwa law enforcement officers kama polisi, magereza, uhamiaji, takukuru.

Ukitaka kuishi maisha mazuri Tanzania, soma noble courses, kozi ambazo zina uwanda mpanda na hizi emerging global courses kama IT, computer na mambo ya ma software na ma artificial intelligence nk.

Kozi za kisiasa zinazozilishwa bongo utateseka bure.
 
Excellent adviseversa!

Kahiyo mpaka wale, wanasheria watarajiwa tupeleke VETA weeee [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sasa Bro si'tutakuwa kama vile nchi ya Wagagagigikoko

Yaani hiyo mwisho wa siku nchi mzima tunakua mafundi [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ni Mara 1000 Nchi nzima iwe na mafundi kutakuwa na tija katika Taifa,ni lazima Nchi itengeneze ajira katika uzalishaji kuliko huduma.MTU akisoma VETA akiwa na ujuzi Fulani ataweka ujuzi wake katika uzalishaji wa moja kwa moja kuliko huyo wa fani ya sheria.
 
Back
Top Bottom