EllySkyWilly
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 2,204
- 2,086
Habari za Leo wakuu,
Mimi kama mtanzania naumia sana juu ya taifa letu kuto kuwa na mafuta wakati jirani zetu wa Uganda wamevumbua.
Nilimsikiliza kwa umakini sana mzee Mseveni siku ile anahutubia kwenye uwanja mpya wa ndege chato. Na nilimwelewa sana yule mzee kuhusu historia ya kutafuta mafuta Uganda. Historia inavutia sana.
Shirika letu la TPDC tangu mwaka 1973 mpaka leo hii 2020 ni miaka 47 halijavumbua mafuta.
Wanafanya kazi gani hapo shirikani. Au wataalam wao hawana uwezo wa kuvumbua?
Tatizo ni nini?
Hata kama wakileta sababu za kwamba kufanya utafiti ni gharama, kwanini Waganda ambao ni binadamu wenye akili kama za kwetu wao wavumbue? Kwani wao waganda hizo gharama za kuvumbua walikuwa wanazipata wapi?
Lazima kuna shida mahali, kichwani, kichwani. Mafuta yanapatikana kwenye akili. "The oil is within your mind. If you don't get the oil it means your knowledge is not enough"
Mafuta yanapatikana ndani ya akili yako ukiona hujayavumbua maana yake ni kwamba akili yako haitoshi kuyavumbua. Umekosa maarifa ya kuyavumbua. Inabidi uyatafute maarifa ya kuyavumbua. Inabidi uongeze maarifa ya kuyavumbua.
Tunapata ukakasi hata kutaja jina la Shirika. Tanzania Petroleum Development Corporation. Mtu anakuuliza mna mafuta? unajibu kwa unyonge tuna gesi. Kama hawawezi kugundua mafuta wabadirishe jina liwe "Tanzania Natural Gas Development Corporation"
Mchoro huu unaofuata unaonyesha ramani ya maeneo mbalimbali ambayo tunaweza kupata mafuta tukiwa siliasi kwenye kuyatafuta. Nimeweka vidoti vya rangi. Kwa chini yake kuna ufunguo wa ramani.