Ni kwanini shirika la TPDC tangu lianzishwe mwaka 1973 mpaka leo halijafanikiwa kuvumbua mafuta?

Ni kwanini shirika la TPDC tangu lianzishwe mwaka 1973 mpaka leo halijafanikiwa kuvumbua mafuta?

Jaribuni kuwatafuta Tullow Oil, hawa ndo walifanya kazi ya mafuta na Gesi kule Uganda. Hawa Tullow oil si Waganda.
Siku ya hotuba ya Mseveni, alikwambia walio gundua mafuta ni Waganda watalaam wa Ndani, naomba uelewe hoja hii. Kwani kugundua mafuta mpaka utumie mtalaam wa nje mkuu. Waganda ndio walio gundua hizo kampuni zilikuja baadaye.

Kugundua mafuta, ni kazi ndogo ukiwa na watalaam wako, kwa umri wa kampuni hiyo ilitakiwa iwe na uwezo wa kufanya uvumbuzi, kampuni imelala. Yamekuja makampuni mbalimbali yamewekeza na kuwapa pesa inamaana mpaka sasa wamekosa mtaji wa kuchukua hata data za miamba chini ya ardhi na kuanza kuzichambua. Shida iko kwenye akili mkuu sio pesa, pesa yenyewe ipo Ndani ya akili.
 
Niliwahi kufanya kazi hapo,wataalam na wasomi waliosoma Vyuo mbalimbali Ulaya wapo wa kutosha
sasa kwanini washindwe kuvumbua mafuta na huo utaalam wao. Wameanza kutafuta mafuta 1973 mpaka Leo hawaja yapata huo ndio utaalam gani
 
Badala kukaa nakupanga wafanye nini, humo itakuwa nikupigana juju na kila mmoja anataka kuwa boss badala yakutumia elimu zao mpaka wanazeeka
elimu zao hazijatumika popote wanakaa ofisini tu hamna wanalo lifanya pale. Wala hawana mikakati yoyote ya kutafuta mafuta. Wanaota tu vitambi
 
Siku ya hotuba ya Mseveni uliwekuwepo, alikwambia walio gundua mafuta ni Waganda watalaam wa Ndani, naomba uelewe hoja hii. Kwani kugundua mafuta mpaka utumie mtalaam wa nje mkuu. Waganda ndio walio gundua hizo kampuni zilikuja baadaye.

Kugundua mafuta, ni kazi ndogo ukiwa na watalaam wako, kwa umri wa kampuni hiyo ilitakiwa iwe na uwezo wa kufanya uvumbuzi, kampuni imelala. Yamekuja makampuni mbalimbali yamewekeza na kuwapa pesa inamaana mpaka sasa wamekosa mtaji wa kuchukua hata data za miamba chini ya ardhi na kuanza kuzichambua. Shida iko kwenye akili mkuu sio pesa, pesa yenyewe ipo Ndani ya a

Inawezekana ni Waganda wenyewe.
 
Aliyekwambia mafuta yapo kila nchi/sehemu ni nani?
Ni kweli kabisa mafuta hayapo kila nchi, Ila kwa geology ya Afrika Mashariki ilivyo Mafuta hayawezi kukosa hata maramoja.
 
tunazungumzia mafuta sio gesi mafuta ndio kila kitu mkuu. Swali ni kwanini Waganda ambao ni binadamu kama sisi kwanini wao wagundue mafuta alafu sisi tushindwe kugundua mafuta? Tatizo liko wapi. Tatizo lipo kwenye akili zetu tu
waliongundua mafuta uganda ni kampuni ya uingereza inaitwa tullow. hii kampuni ilitaka kutafuta nafuta ghana wakanyimwa leseni. wakasema basi ngoja tuende uganda. watu wakawacheka sana na kuwaambia wanaenda kupoteza pesa na mda. wakaenda uganda nakufocus kwenye rift system -bonde la ufa na hatimae wakapata mafuta. tullow ndio wakaja kuuza kwa Total
 
Tatizo sio pesa mkuu, kama tatizo ni pesa kwanini waganda maskini kama sisi wagundue, hata kama rigs zinakodiwa, swali ni kwanini waganda wagundue alafu sisi tushindwe?
sio uganda tu hata kenya pia. hata hapa pia tafiti zinaendelea kwenye maeneo ya bonde la ufa. maeneo kama kilosa, kilombero, lake eyasi, lake rukwa. uganda ndio walianza nasisi huku ndio tumeanza
 
Wako ofisini wanacheza candy crash

Trust wafanyakazi wa serikalini na Taasisi zake hawana kazi nyingi sana

Mfano Leo tu nimetoka ofisi moja ya serikali Ni kubwa tu nimekutwa soga zinaendelea
 
Ile kitu nakumbuka waziri nani yule aliwaambia wawekezaji wa Tanzani, kuwekeza kwenye mafuta sio kama kuuza juice.
na watu walimuona Muhongo kama vile anawabania vile kumbe ndio uhalisia wenyewe
 
Wako ofisini wanacheza candy crash

Trust wafanyakazi wa serikalini na Taasisi zake hawana kazi nyingi sana

Mfano Leo tu nimetoka ofisi moja ya serikali Ni kubwa tu nimekutwa soga zinaendelea
Wanaota vitambi tu, hawana lolote wanalofanya, wanakariri presentation hakuna chochote wanacho kielewa.
 
kwanza unaweza kutofautisha au kufananisha
petroleum na Gas?
je ni sawa au sio sawa??

Tuanzie hapo
Neno petroleum lenyewe limetokana na maneno mawili ya kilatini
petra, linalomaanisha “rock,” yaani mwamba oleum, linalomaanisha “oil” yaani mafuta.

Kwa hiyo maana ya petroleum ni kimiminika cha asili chenye mchanganyiko wa kampaundi zilizo undwa kwa kaboni na hydrojeni kinachopatikana kwenye miamba chini ya ardhi ya dunia.

Au unaweza kusema petroleum ni kimiminika kinachowaka chenye rangi ya njano au nyeusi chenye mchanganyiko wa kampaundi za gesi, vimiminika na yabisi vilivyoundwa kwa elementi ya kaboni na hydrojeni vilivyotokea kwa njia ya asili chini ya ardhi ya dunia kwenye miamba. Na mchanganyiko huo unaweza kutenganishwa nakupata gesi asilia yaani mithane, gesi ya kimiminika ya petroli yaani LPG (propane na butane), petroli, mafuta ya taa, mafuta ya ndege, dizeli, mafuta ya kulainisha sehemu za injini, inta ya kutengenezea mishumaa, mafuta mazito ya kwenye mitambo mikubwa, mali ghafi za kuzalishia kemikali mbalimbali na rami ya kutengenezea barabara.
 
Back
Top Bottom