JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 8,556
- 18,428
Hii serikali inachojua ni uteuzi na kuunda taasisi za kiutawala tu,Habari za Leo wakuu,
Mimi kama mtanzania naumia sana juu ya taifa letu kuto kuwa na mafuta wakati jirani zetu wa Uganda wamevumbua.
Nilimsikiliza kwa umakini sana mzee Mseveni siku ile anahutubia kwenye uwanja mpya wa ndege chato. Na nilimwelewa sana yule mzee kuhusu historia ya kutafuta mafuta Uganda. Historia inavutia sana.
Shirika letu la TPDC tangu mwaka 1973 mpaka leo hii 2020 ni miaka 47 halijavumbua mafuta.
Wanafanya kazi gani hapo shirikani. Au wataalam wao hawana uwezo wa kuvumbua?
Tatizo ni nini?
Hata kama wakileta sababu za kwamba kufanya utafiti ni gharama, kwanini Waganda ambao ni binadamu wenye akili kama za kwetu wao wavumbue? Kwani wao waganda hizo gharama za kuvumbua walikuwa wanazipata wapi?
Lazima kuna shida mahali, kichwani, kichwani. Mafuta yanapatikana kwenye akili. "The oil is within your mind. If you don't get the oil it means your knowledge is not enough"
Mafuta yanapatikana ndani ya akili yako ukiona hujayavumbua maana yake ni kwamba akili yako haitoshi kuyavumbua. Umekosa maarifa ya kuyavumbua. Inabidi uyatafute maarifa ya kuyavumbua. Inabidi uongeze maarifa ya kuyavumbua.
Tunapata ukakasi hata kutaja jina la Shirika. Tanzania Petroleum Development Corporation. Mtu anakuuliza mna mafuta? unajibu kwa unyonge tuna gesi. Kama hawawezi kugundua mafuta wabadirishe jina liwe "Tanzania Natural Gas Development Corporation"
Kuna sumatra,Kuna LATRA,Kuna Tarura&Sumatra,Kuna TBS,Kuna DFD,Kuna TARIRI(watafiti wa mifugo)harafu Kuna wakala wa mbegu,TARI,)Kuna NHC,harafu Kuna TBA,wote wanajenga nyumba.
Kuna TPDC harafu Kuna state oil,maataasisi Mengi yanayofsnya kazi moja,hapa ni kuongeza ukiritimba tu,serikali haitakiwi kujenga nyumba,iwezeshe sekta binafsi ifanye,
Kuna haja gani ya kuwa na wizara nyingi,26,maji,kilimo,mifugo,ilibidi iwe wizara moja.