Ni kwanini ukikutana na Wanaotoka Tamasha la Mwakasege na Mwamposa Kawe unaiona tofauti hii Kubwa?

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mwakasege hakukosea kujiita mwalimu, ni mtu anaweza sikilizwa na dini/dhehebu lolote na ukatoka na kitu kikubwa.
Ana semina ya siku tano inaendelea Kawe na anamaliza kesho. Nimehudhuria siku zote tangu ianze.

Itoshe tu kusema kwamba Mwakasege kweli ni Mwalimu na Neno la Mungu Analijua. Na napenda alivyo simple. Ni neno tu basi hakuna makorokocho mengine wala maigizo.

Somo analofundisha katika semina hii (Maombi ya Kimkakati) ni gumu kidogo lakini anakwenda polepole na anahakikisha kuwa kila mtu anaelewa kwa kadri ya uwezo wake. Ni Neno kwa Neno, Mifano kwa Mifano...

Mungu Azidi kumtunza mtumishi huyu.

Na katika miaka hii minne inayokuja anasisitiza sana tuiombee Tanzania maana itapita katika misukosuko mingi. Ndiyo lengo hasa la semina hii. Kupata makuhani watakaosimama katika zamu zao ili kuiombea nchi yetu kwa maombi ya kimkakati hasa katika miaka hii minne inayokuja...
 
Huyu ndio mlokole pekee huwa nafuatilia mafundisho yake.
 
Bulldozer kamatia hapo hapo... wanaokuponda wataendelea kuweweseka tu.
 
Hao Wana huduma mbili tofauti watafananaje SAsa.
1.Mmoja ni Mwalimu
2.Mwingine ni mtume na Nabii.
So hata wafuasi wao upata huduma tofauti.
 
Jambo hili MINOCYCLINE well informed person alikuwa anasema wata wakamuona ana chuki sasa hivi na wewe umeliona sijui watasemaje ...
 

Na wote wakiwa na maarifa hakutakuwa na haja ya uwepo wa walimu,wachungaji ,wainjilisti,mitume na manabii
 
Ukiona GENTAMYCINE namkubali Mtu ( kama Mwakasege ) jua amebarikiwa na ana Akili na siyo kama Wapuuzi Wengine.
 
Halafu huwa wanakwepa kulipa nauli kwa konda kwenye daladala wakiwa wanaenda kufuata miujiza, halafu wakifika wanashuhudia WIZI wao 😂😂😂 eti Mungu kawafanyia muujiza wa konda kuwasahau kuwalipisha nauli il hali kulipa nauli ni WAJIBU na siyo lazima mpaka konda aombe..
 
Barikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…