Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?


Kwanza inabidi utoe hiyo definition yako ya mjini ni wapi ambako utapata kiwanja kwa milioni tano na saizi yake ni nini? Halafu ndio urudi hapa.
 
Mi mwenyewe nataka ghorofa na lazima nijenge ni kupenda tuuuu
 
Hawawezi kuamini binafsi nilikuwa naandaa estimate ya mteja wangu, Msingi upo kwenye 42m, hata tukianza project tukajibana vipi hatuwezi kutumia chini ya 35m
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji1787][emoji1787] jamani
 
Hawawezi kuamini binafsi nilikuwa naandaa estimate ya mteja wangu, Msingi upo kwenye 42m, hata tukianza project tukajibana vipi hatuwezi kutumia chini ya 35m
Asante Mkuu. Wengi wanadhani ni kujikweza. Hakika nilidhani ni rahisi. Kwa sasa naelewa kwanini si wengi wanamiliki ghorofa
 
hivi kulala juu ghorofa ya nne! ni zindiko tosha hata ndege za kichawi hazifiki hukoo, wazungu walilenga hapo!wakipanda sana ni usawa wa ghorofa ya tatu! lkn pia kuna mawimbi mengi yanawarudishaga chini! angalia hii video kwa mfano
 
mkuu
Hawawezi kuamini binafsi nilikuwa naandaa estimate ya mteja wangu, Msingi upo kwenye 42m, hata tukianza project tukajibana vipi hatuwezi kutumia chini ya 35m
uko sahihi. kuna jamaa yangu alijenga..msingi uligonga mpaka 100M. Unajua wengi wetu mawazo yetu yanaendana na vipato vyetu. kwa mwenye nazo..hiyo ni hela ya kawaida..asiye nazo..ndo hivo atakuja hapa atakwambia hiyo ni hela nyingi haiwezekani. Kikubwa kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake….

Kama una uwezo...ishi na kufurahia matunda ya jasho lako.
 
Dada cha kushangaza hapa Arusha hakuna kiwanja cha milion 5,labda huko ndani kijijini kabisa.
Kuna jirani yangu hapa anauza miguu kumi kwa kumi na tatu kwa milion kumi na nne. Yan ni balaa
Alipomaanisha mjini alimaanisha sehem zenye huduma muhimu sio lazima pawe mjini au manispaa.
 
Sahihi kabisa
 
Kijijini kwetu kuna hizo huduma zote za muhimu
Ni kijiji kwenu kwenye mabenki angalau matatu mannee au ikishindikana basi mawili..sio wakala wa benki.
Ni kijijini kwenu ambapo kuna maafisa mipango miji nk.
Kwa hilo hongera..ila sehemu kubwa ya nchi haina huduma zote muhimu.
 
Atleast wako ambao wana exposure zaidi. Maana kuna wengine wanaclaim ni show off. Binafsi maybe ningeambiwa bila kuona isingekua rahisi kuamini. Kila siku mpya tunajifunza jambo jipya
 
Fashion tu, kama una hela fetua usingizi wa kutosha
 
Badala ya kujenga nyumba kubwa kutapakaa eneo kubwa , ukijenga ghorofa inasaidia nafasi kubaki kwa matumizi mengine,

Pia eneo likibaki nafasi kubwa inapendeza zaidi kwa muonekano hata wakati wa kufanya shughuli za kifamilia unaweza kufanyia nyumbani kwako badala ya kwenda kukodi ukumbi kwa gharama kubwa.
 
bila kujenga gorofa roho yangu haitaridhika kabisa. kupenda privacy nayo ni motive nyingine. nimetenga 20m kila mwaka kwa miaka mitano,nikipata master bed room na longie kule juu inatosha. Nitatoboa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…