[emoji28][emoji28][emoji28] jamani nyie Kuna watu wanafurahisha sana, Hichi kipande looks so funny
Kwa ujumla, kuna watu wana mentality za ajabu. Kwa sababu ana hela, hata akiwa na eneo la ukubwa wa ekari nzima, ataamua atumie hata 10% ya eneo lakini ajenge nyumba ya ghorofa.
Ghorofa inatakiwa lijengwe kwa sababu ya shida ya ardhi, na siyo ufahari.
Watu wengi hawajui kuwa jengo la ghorofa lina risks nyingi: kukitokea hitilafu za kiufundi na kihandisi katika ujenzi, na hasa kwa nchi kama yetu ambayo nondo na vyuma vinavyopatikana madukani ni hafifu sana katika ubora, hujui hilo jengo litaanguka lini.
Jambo la pili, ni endapo kutatokea majanga ya kiasili kama tetemeko la ardhi, ambaye upo kwenye jengo la ghorofa, upo kwenye hatari kubwa zaidi. Huwa kuna maafa madogo sana kukiwa na tetemeko la ardhi kwa watu waliopo kwenye nyumba za kawaida.
Jengo la ghorofa, kama kukiwa na ajali ya moto, upo kwenye hatari kubwa zaidi, na hasa kama moto huo utaanzia chini.
Zamani, nilipokuwa bado sijayajua masuala haya ya usalama, kila nikisafiri, nilikuwa najisikia ufahari kulala kwenye mahoteli yale ya majengo marefu sana. Lakini siku hizi, kwa kuzingatia sababu mbalimbali za kiusalama, na kwa sababu hoteli nyingi ni za ghorofa, basi napendelea niwe kwenye chumba angalao isizidi floor ya pili tokea chini, labda iwe imeshindikana kabisa.
Nchi kama Australia, nilishangaa kuona kuna hoteli aghali sana na zina huduma za viwango vya juu sana, lakini siyo za ghorofa.
Kwa ujumla, kama una uwezo wa kupata eneo kubwa, jenga nyumba yako nzuri ya kawaida, achana na mambo ya ghorofa. Kwetu hapa, nondo na vyuma vina viwango vya chini sana katika ubora.