Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Nimeuliza hapo juu kumbe ushajibu. Kwa hiyo nihamie korogwe ili nikapate kiwanja cheap!
Mikoani kiwanja unapata cha kawaida unapata kwa 1.5M mpaka 2M

Yaani kiwanja japo sio kikuuubwa lakini cha wastani kujenga na kulima bustani
 
Hawawezi kuamini binafsi nilikuwa naandaa estimate ya mteja wangu, Msingi upo kwenye 42m, hata tukianza project tukajibana vipi hatuwezi kutumia chini ya 35m
Mna umri gani nyie?
Hamna msingi wa ghorofa la makazi wa zaidi ya 20m, avarage ni 15m tena umetumia mkandarasi kabisa. Kama mmeibiwa kwa ujinga uzembe wenu msijaribu kuhalalisha uzembe wenu hapa.
 
Mna umri gani nyie?
Hamna msingi wa ghorofa la makazi wa zaidi ya 20m, avarage ni 15m tena umetumia mkandarasi kabisa. Kama mmeibiwa kwa ujinga uzembe wenu msijaribu kuhalalisha uzembe wenu hapa.
upo sawa kwa mtazamo wako, Ujenzi mbona watu wengine wanajenga hata nyumba ya vyumba 5 kwa milion 10 tu, 😂😂😂
 
upo sawa kwa mtazamo wako, Ujenzi mbona watu wengine wanajenga hata nyumba ya vyumba 5 kwa milion 10 tu, 😂😂😂
Acha kudanganya watu na blah blah za mtaani, msingi wa hizi ghorofa zetu za mtaani ni 15-20m, hizo za 40m mnajengea Almasi? Nyie ndio mnaodanganyaga watu ghorofa moja za mtaani 300-500m wakati kwa 100m -150m unamaliza na finishing kabisa nzuri.
 
kwani ugomvi hata Milioni 5 ghorofa unajenga Mzee 😂😂😂
 
Hawawezi kuamini binafsi nilikuwa naandaa estimate ya mteja wangu, Msingi upo kwenye 42m, hata tukianza project tukajibana vipi hatuwezi kutumia chini ya 35m
Naomba tufanye jambo flani kwa pamoja. Yaani tuangalie major items za msingi. Ili nami nijifunze kitu. Professionally mimi ni QS mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 10
1. Zege la strip foundation ni CM ngapi?
2. Ukuta wa strip foundation ni SM ngapi?
3. Nondo za pad +starter columns + Plinth beams ni Tonne ngapi?
4. Zege la pad+starter Columns+Plinth beams +conc. Bed ni CM ngapi?
5. Floor area ya jengo ni SM ngapi?
 
Kwa msingi wa ghorofa unaweza kununua viwanja viwili.
Yeah.. Kuna nguzo nazijenga, kitako chake ni 3mX3m na kitanyonya zege lenye urefu wa nusu mita.. Material yatakayoingia kwenye kitako pekee ni karibu tani 15 ili kuweza kubeba floor tatu.. Concrete grade inatumika m20, na nondo tisa zinatumika kwa nguzo moja.. Kitako hiki kitakuwa na jumla ya nguzo nne.. So unaweza ukapiga hesabu hapo.
So far viko vitako viwili vya aina hii na jumla vitakula karibu tani 25 za materials.
 
Nadhani Hilo jengo sio residential.
 
Aisee [emoji119]
 
Kiwanja cba milioni tano mjini ni wapi huko mkuu nije fasta kununua ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…