Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Kujenga gorofa labda apartment upangishe vinginevyo ni kusababisha ugomvi wakati ukifa na kila mmoja atataka gorofa lako.
Pili unapozeeka una sukari, pressure, moyo,mguu kwishney yaani utatesa tu watu kukubeba.
Jenga nyumba ya chini tu bana.
Hizi ni akili za umasikini wa kutupwa
 
Wenye ndoto za kujenga ghorofa msitishwe. Tafuteni watu sahihi ili wawaongoze vyema kuanzia hatua ya uandaaji wa michoro mpaka gharama zote za ujenzi kabla hamjaanza ujenzi.

Binafsi mimi nimesomea ujenzi na ndio shughuli ninazofanya kila siku. Nimejenga ghorofa yenye eneo la mraba 204 (chini 102 , juu102), Toangoma-Dar es salaam. Mpaka sasa nimetumia around 75m, na tayari ninaishi humo humo sehemu ya chini. Maana juu ndio naezeka ndani ya siku 7.

Kiufupi Sijakamirisha mambo yafuatayo
1. Plaster sehemu ya juu na nje
2. Tiles Chini na juu
3. Ceiling juu
4. Wiring sehemu ya juu
5. Aluminium windows chini na juu
6. Grills juu pekee
7. Plumbing juu pekee
8. Milango ya chini na juu
9. Rangi juu na nje

Ifahamike kwamba, kwa sababu tayari naishi kwenye jengo hilohilo, kuna baadhi ya vitu nimeviweka temporarily kwa ajili ya kuwezesha maisha kwa sasa. Ila baadae nitavitoa.

Vitu vilivyosalia navitafutia 30m, ili nivikamirishe. Picha nitawatumia wiki ijayo pindi wakimaliza kuezeka.

Lakini pia karibuni kwa huduma ya ujenzi , kutengenezewa Ramani na BOQ. Kwa sasa namalizia kazi flani Zanzibar, ila pia kwa sasa nina kazi ya ujenzi wa ghorofa Dodoma. Kwa walio Dodoma wanaweza nitembelea. Namba yangu 0755678173
 
Mkuu mwaka huu najenga kaghorofa changu ,nitakutafuta unisaidie vitu
 
[emoji28][emoji28][emoji28] jamani nyie Kuna watu wanafurahisha sana, Hichi kipande looks so funny


Kwa ujumla, kuna watu wana mentality za ajabu. Kwa sababu ana hela, hata akiwa na eneo la ukubwa wa ekari nzima, ataamua atumie hata 10% ya eneo lakini ajenge nyumba ya ghorofa.

Ghorofa inatakiwa lijengwe kwa sababu ya shida ya ardhi, na siyo ufahari.

Watu wengi hawajui kuwa jengo la ghorofa lina risks nyingi: kukitokea hitilafu za kiufundi na kihandisi katika ujenzi, na hasa kwa nchi kama yetu ambayo nondo na vyuma vinavyopatikana madukani ni hafifu sana katika ubora, hujui hilo jengo litaanguka lini.

Jambo la pili, ni endapo kutatokea majanga ya kiasili kama tetemeko la ardhi, ambaye upo kwenye jengo la ghorofa, upo kwenye hatari kubwa zaidi. Huwa kuna maafa madogo sana kukiwa na tetemeko la ardhi kwa watu waliopo kwenye nyumba za kawaida.

Jengo la ghorofa, kama kukiwa na ajali ya moto, upo kwenye hatari kubwa zaidi, na hasa kama moto huo utaanzia chini.

Zamani, nilipokuwa bado sijayajua masuala haya ya usalama, kila nikisafiri, nilikuwa najisikia ufahari kulala kwenye mahoteli yale ya majengo marefu sana. Lakini siku hizi, kwa kuzingatia sababu mbalimbali za kiusalama, na kwa sababu hoteli nyingi ni za ghorofa, basi napendelea niwe kwenye chumba angalao isizidi floor ya pili tokea chini, labda iwe imeshindikana kabisa.

Nchi kama Australia, nilishangaa kuona kuna hoteli aghali sana na zina huduma za viwango vya juu sana, lakini siyo za ghorofa.

Kwa ujumla, kama una uwezo wa kupata eneo kubwa, jenga nyumba yako nzuri ya kawaida, achana na mambo ya ghorofa. Kwetu hapa, nondo na vyuma vina viwango vya chini sana katika ubora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…