Kiongozi si mtu binafsi, ni mtu aliyejivua haki zake za mtu binafsi na kuamua kuwa "public figure".
Angetaka kuwa na faragha ya "mtu binafsi", asingegombea uongozi tungetetea haki zake za faragha.
Waingereza wanasema "You can't eat your cake and have it too".
Yani watu wana uchaguzi wa kuamua, ama wanataka maisha ya faragha, bila ya kuwa viongozi, au wanataka maisha ya uongozi, yasiyo na faragha.
Haitakiwi mtu agombee uongozi na kutoa maisha yake yawe ya huduma kwa wananchi, huduma ambayo inategemea afya yake kuwa nzuri, halafu akipata matatizo ya kiafya atake kufanya faragha afiche.
That is like eating your cake and expecting it to be there. Kama unataka maisha ya faragha, usigombee uongozi.
Ndiyo maana Rais Mstaafu Kikwete alipopata matatizo ya tezi dume aliutangazia ulimwengu. Bila aibu. Namuheshimu sana Kikwete kwa hilo, ingawa kuna matatizo yake mengine ya kuangukaanguka tangu zamani hakuyasema wazi, kwa sababu za kisiasa.
Kama kawaida, viongozi wetu wanajifunza mambo baada ya kutoka madarakani.
Sasa wewe ungependa mtu mwenye kifafa kwa mfano, anayeangukanguka kila mara, agombee urais bila ya kuwaambia watu kwamba ana kifafa na muda wowote anaweza kuanguka jukwaani? Utaona mtu ana haki ya kugombea urais bila kuwataarifu wananchi kwamba ana kifafa? Kwa sababu ni suala la binafsi?
Unapokuwa kiongozi wa nchi, suala la afya binafsi ni suala la usalama wa taifa.
Nyerere aliwahi kusema hili, rais akikohoa tu watu wanaulizana, kile kikohozi cha kawaida au ana kifua kikuu yule?