Ni kwanini Viongozi Serikalini wakilazwa Mzena Hospital huwa tunafichwa, ila wakifa tu tunaambiwa Walilazwa hapo Mzena Hospital?

Ni kwanini Viongozi Serikalini wakilazwa Mzena Hospital huwa tunafichwa, ila wakifa tu tunaambiwa Walilazwa hapo Mzena Hospital?

Sasa kwanini tu kwakuwa mmeamua Kutuficha Watanzania kuhusu Kulazwa Kwao hapo Mzena Hospital basi hata Wakifa ( Wakifariki ) msiendelee pia Kutuficha kwa Kutotujajia hiyo Hospitali na badala yake muendelee tu na Ratiba zenu za Maziko nyie nyie kama nyie pamoja na Wauguzi wa Mzena Hospital na wale Walinzi Wanoko wenye Maswali ya Kukomoa pale Getini Makumbusho? Tumeivumilia hii tabia tumechoka na badilikeni!
Hivi wewe unaumwa? Na kama unaumwa, umekwenda Mzena wakakataa kukutibia? Tatizo ni nini? Kwani wakubwa wote wanaumwa? Je! Hospitali hiyo imeanzishwa kuwatibu wakubwa tu? Maswali ni mengi, tupe majibu.
 
Karibu mtataka Viongozi wote wapande daladala kwenda kazini Akili za hovyo kabisa. Wewe unatambua heshima kubwa na hadhi za Viongozi pamoja na heshima hizo na wenyewe ni binadamu wanamadhaifu yao inamaana wanahitajika Watu wenye taaluma ya Siri nje ya taaluma ya Udaktari .Hivyo basi tegemea siku zote Viongozi kutibiwa mahali pa Hivyo .Kumbuka kuwa hapo Muhimbili au. Mwananyamala akija kiongozi akifika mpaka baadhi ya huduma huwa zinasimama kwa muda kwa sababu za kiusalama Sasa Leo unataka tulazwe naye Mwananyamala huo ni upeo finyu wa kufikiri.Yaani hata kiongozi akijisikia mafua akaenda zahanati nchi nzima itajua kuwa kiongozi anayo mafua.Hivyo taarifa za matibabu kwa Viongozi kuwa siri kwa Viongozi ni muhimu Sana kuondoa taharuki na hofu kwa wafuasi wao itatolewa tu pale itakapokuwa lazima. Pia nakukumbusha kuwa siyo kila sehemu za Siri ni bora Sana bali Kinachofuatwa ni Usiri tu.
Duh mzee umekosea mimi nimesema raia hawezi kuwa sawa na kiongozi
Hiyo hospitali ni special kwa ajili yao watu fulani tu lbda na familia zao

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Ukipanda pale juu kabisa ghorofani Kairuki Hospital, unaona mle ndani na hiyo hospital ipo huku karibu na Kairuki,kuna rafiki yangu dada yake ni mfanyakazi wa hiyo idara tulienda msalimia siku moja,mle ndani,maswali mengi utadhani sijui unaomba visa ya kwenda marekani
Ni kweli yapo maswali yasiyo na tija kwa mtu ambaye anakwenda kumuona mgonjwa , vikwazo vingine ndivyo huzaa story kama hizi ni bora wapunguze maswali ili ndugu wenye huzuni wapite kwenda kuwaona ndugu zao pasipo usumbufu wowote ule
 
Sasa kwanini tu kwakuwa mmeamua Kutuficha Watanzania kuhusu Kulazwa Kwao hapo Mzena Hospital basi hata Wakifa ( Wakifariki ) msiendelee pia Kutuficha kwa Kutotujajia hiyo Hospitali na badala yake muendelee tu na Ratiba zenu za Maziko nyie nyie kama nyie pamoja na Wauguzi wa Mzena Hospital na wale Walinzi Wanoko wenye Maswali ya Kukomoa pale Getini Makumbusho? Tumeivumilia hii tabia tumechoka na badilikeni!
Naona umekuja na id nyingine.
 
Ina maana hata yule mzee wetu wa kutuita marofa alikuwa anatibiwa pale?
Ndiyo na ni hapo hapo pia hata Israeli nae alimfuata na Kuvunja Mkataba wake rasmi wa Uhai Usiku ambapo nae alikubali Mutually na Kuondoka.
 
Kwani mkuu unaumia na nini juu ya Mzena? Wakilazwa hapo wagonjwa unatesekea nini? Ulisikia pale ni ya kila mtu ndo uende ende?
Ila unashangaza sana mtanzania mwenzangu. Ulienda kwa kufata protocol inavyopaswa ama ukienda na mziki wako mkubwa masifa sifa etc?
Na aliyekuambia ninkila kiongozi anatibiwa hapo ni nani? Na mbona ni hispital ya siku nyingi sana hiyo ndo mnaijua leo ama?
Dhumuni lako la Kujifanya kuandika kwa Uchungu hivi na Kiufafanuzi ili tukujue kuwa nawe ni mwana TISS limetimia Ndugu je, kuna ulilolisahau?
 
Back
Top Bottom