Ni kwanini walimu wanadharaulika sana mitaani?

Tate umechachamaa balaa.

Ulikuwa Mwalimu wa shule ya msingi?
 
Umeandika vema,lakini kuna kitu/vitu hujavifanyia utafiti haswa.
Kwa andiko lako inaonekana mwalimu ndiye daraja la chini kabisa kiuchumi,kiheshima na hata kimwonekano.
Hii siyo kweli,kwa mfano:
1.Walimu ndiyo waumini wazuri katika sehemu za ibada.
2.Walimu kwa kiasi kikubwa ndiyo hutumika pale jamii inayomzunguka ikiwa na shughuli/tukio(MC,wenyeviti wa vikao,waandaa ratiba n.k)
3.Walimu kuna wakati huwasaidia msaada wa hali na mali watoto/wanafunzi bila hata wazazi kujua.Pia hutoa zawadi kwa watoto kuliko hata wazazi wao(baadhi ya wazazi)
4.Walimu wengi hujitahidi kusomesha watoto wao na kusimamia elimu zao vizuri zaidi.Mara nyingi wao hujinyima kumiliki vitu vya gharama kubwa ili wasomeshe watoto wao.
5.Wakulima asilimia kubwa,Wachuuzi,machinga,mgambo na hata wafugaji mara nyingi hutamani kuwa na maisha kama ya walimu wanao wazunguka.(Japo ni kweli walimu hukopa kopa lakini siyo kusema wanakokopa wote wamewazidi vipato.

Kwa ujumla ni kweli walimu ukiwalinganisha na wafanyakazi wengine wao wanaonekana wapo chini.Ila kumbuka nao kuna makundi mengine wameyazidi ktk jamii.
 
Walimu wengi hawajitambui over
 
Walimu mnawaonea ila mishahara ya watumishi serikalini ni midogo sana sema kinachowafanya hao wengine wa survive ni per diem tu kitu ambacho walimu wana kosa wao wanasubiria mwisho wa mwezi tu wakati kada nyingine huko posho na madokezo ndo yanawaweka mjini ila mishahara inafanana tu.
 
Katika mada za kijinga, hii namba moja.
Huwezi kuwadharau watu muhimu kwa maneno ya kejeli kiasi hiki. Bila walimu ungeweza kuandika uharo ulioandika hapa. Hata kama una uwezo kiasi gani huwezi kudharau wenzako kiasi hiki. Wamekuwezesha kuandika unaleta dharau.

Halafu watu kama nyie utakuta mnaishi kwa shemeji zenu. Kuwa na adabu.
 
Wewe si ulienda fundisha lindi ikataka kula ka under age?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…