Ni kwanini walimu wanadharaulika sana mitaani?

Hawaelewi kuwa mwalimu akistaafu kila mwezi analipwa
Vijana wengi humu ni majobless. Hivyo wapo kimihemko zaidi, na wanafikiri watu wote humu jukwaani ni watoto kama wao.

Wanasema eti walimu wengi wastaafu wanahangaika mtaani mpaka wanatia huruma!! Sasa wanataka hao walimu wakistaafu, wasifanye shughuli nyingine za kujiingizia kipato! Mfano kilimo, ufugaji, biashara, nk?

Na ikatokea mwalimu mstaafu akafariki, shida iko wapi? Kwani sababu za kifo zinasababishwa na kustaafu tu!! Haika kuna mambo yanastaajabisha sana kutokana na uwezo wa kufikiri wa hiki kizazi cha sasa.
 
safari ya kwenda mashuleni kufundisha na kurudi nyumbani ni mazoezi yanayowasaidi sana kuwapa afya watu wengi.

Ni sehemu ya mazoezi yao japo wanaweza wasibaini kama zile movement zinaimarisha afya zao...

sasa gafla wanapo staafu ana kubadili mtindo wa maisha, huibuka mamabo mengi nyemelezi yaliyokua yakizuiwa au kudhubitiwa na zile movement za kila siku za kutoka nyumbani hadi kazini na kurudi...

hata hivyo, kifo kaumbiwa mwanadamu,
na tupo hivi tulivyo kwa neema na baraka za Mungu tyuu....
 
Wewe ni mwanamke au!! Mbona unajichekesha hovyo kama mchumba wangu wa zamani cocastic!!
 
Utafiti wako hauna uhalisia, ni maoni tu.
 
kimsingi sio waalimu tu wastaafu wengi wanakosa namna ya kuendelea kuishi vyema baada ya ajira ndiomaana wanapotea haraka sana, kumekosekana elimu mahsusi ya kuwaandaa ili waishi vyema baada ya utumishi, pili kuiga iga na kutumia hela hovyo hasa kwenye ulevi na umalaya, na kingine hakuna utaratibu maalum wa kuangalia afya zao mara wamalizapo utumishi , na kikubwa zaidi ni kukosekana kwa hela ya kueleweka baada ya utumishi, ukiskia mtu kapata kiinua mgongo utadhani ni hela ya maana kumbe yooote imeishia kwenye mamiradi ya serikali huku waliochangia wakiambulia kiduchu, wanaachaje kufa haraka?
 
Kwa kuwa thread ni ya ,PWAYUNGU basi no comment
 
Usingefundishwa na hao vilaza usingejua kuandika hivyo kaa chini tulia kama ww sio mwl pita juuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…