Ni kwanini walimu wanadharaulika sana mitaani?

Sio walimu tu, kwa yeyote pesa ndo kigezo cha heshima miongoni mwa binadamu.
 
Walimu naomba mpuuzeni huyu Mpwayungu kwani tokea alete mada ya dada yake kushikwa matiti na kuchezewa sehemu za siri na wahindi niliona kabisa hayupo sawa kichwani.

Binafsi nawapenda na kuwaheshimu walimu wangu kwani wamefanya kazi kubwa mpk mimi kuwa hapa muda mwingine wangekuwa kama wazazi kwangu..
 
Wakifanya hivyo, wajinga wanaowaponda walimu leo ndio hao hao watakua mstari wa mbele kulalamika sababu watagundua watoto wao ni mapopoma kupitiliza.
 
Hapo asilimia mia wataheshimika, shida yao wamejigeuza watumwa sijui wamefungwa na nguvu za giza, yani unakuta mwisho wa vipindi ni saa nane mchana yeye anaforce mje jioni hata saa kumi ili awafundishe zaidi ya hapo anafanya tofauti na maagizo ya wizara, ndio maana ndalichako alikemeaga hili alisema walim likizo acheni wanafunzi waende nyumbani maana mnafundisha non stop shida nini?, bado ummy mwalimu alikemea hili ila wao kila siku na chaki mkononi. Nadhani hawana kazi za ziada ndio maana wanaona bora wafundishe hata Bure tu kwasababu hawana overtime hawa watu.
 
[emoji848][emoji848] au sio
waalimu mmesikia[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hicho ni kiherehere chenu [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Inategemea na mazingira uliyopo. Na aina ya walimu unaowafahamu.
Kama uko kijijini sana usitegemee kumuona mwalimu akiwa tofauti.
Hata watu wa kada nyingine wako hivyohivyo. Inategemea na mazingira.

Darasa limejaa vumbi, barabara hakuna full kukanyaga umande, salon hakuna, usafiri shida, unategemea huyo mtu ataonekana smart kweli?

Serikali iboreshe mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji, itoe transport allowances, utaona tu mabadiliko. Hata walioko Dar, anaefanya kazi mjini -posta hawezi kuwa sawa na wa mbagala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…