Umefanya nifanye ufukunyuzi kidogo kwa jambo uliloandika!
Mpnz wangu(tunaishi pamoja japo hatujafunga ndoa, ila tuna mtoto) ni mwalimu, (shahada), ana miaka 9 kazini, basic salary yake ni 1,235,000/=
Alikopa ili kujenga kwao, aliponiambia habari za kukopa afanye maboresho ya nyumbani kwao nilimuunga mkono, akafanya hivyo....
Nanunua mahitaji yote ya nyumbani, lakini mara nyingi tu hutumia pesa yake kununulia mahitaji ya hapa na pale, sasa haya maisha ya sijui kukopa kila kitu yanahusu walimu wa jnamna gani?
Maana pamoja na kukopa anabaki na ka sh.570k kwa matumizi yake madogo madogo, na kama usingekuwa mkopo angekuwa anakunja zaidi ya 900k kila mwezi, japo si nyingi lakini sio ya kumfanya mtu akope dagaa na mafuta ya kula kwa mangi...
Mimi mshahara wangu hauna tofauti kubwa na wa mpnz wangu, lakini kwetu semina, safari posho na turushwa tunatunisha mifuko na kufanya tuheshimike kidogo kitaa!
Lakini tofauti na rushwa, na hizi seminar + safari hakika nakwambia hali ingekuwa mbaya mnooo, wote tungekuwa tunaugulia ukata!
Kizuri ni kwamba watanzania wanatupa heshima kutokana na rushwa wanazotupa wao wenyewe...
View attachment 2272097