Ni kwanini wamiliki wa lodge na hotels ni wagumu sana kufanya marekebisho ya biashara zao?

Ni kwanini wamiliki wa lodge na hotels ni wagumu sana kufanya marekebisho ya biashara zao?

Poker

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
7,349
Reaction score
21,802
Unakuta mtu kajenga lodge au hotel yake nzuri kabisa, ila sasa kufanya marekebisho au renovation inakuwa mtihani sana.

Kuna mkoa nilienda mwaka 2022, nikafikia lodge X, ilikuwa nzuri kabisa ila vitanda na shower zake zilikuwa zishachoka. Nilirudi tena mwaka 2025 na nikakuta shower na vitanda vile vile 😳.

Wengi wanapenda kuifanya hii biashara ila hawajui kuifanya hii biashara, wanataka kuona hela zinaingia tu na sio kutoka.

Ukarabati pekee wengi wanaofanya ni kubadili wafanyakazi na kupaka rangi tu, ila vitanda, magodoro, shower za kuogea, kuboresha floor kwao ni kosa la jinai.

Wamiliki wa lodge na hotels mjitathmini sana juu ya hizo biashara zenu, msipende hela tu bali huduma ziendane na pesa mteja anayolipa.
 
Hotel za Tz ambazo bei ni kati ya 30,000 mpaka 60,000 huwa ni 'nzuri'miezi sita ya kwanza. Yaani kama bajeti yako ni chini ya 60,000 hakikisha unalala hotel mpya.
Hizi nyingi wanatumia vifaa vya finishing vya kichina havidumu na kufanya marekebisho ni kama unajenga tena.
 
Unakuta mtu kajenga lodge au hotel yake nzuri kabisa, ila sasa kufanya marekebisho au renovation inakuwa mtihani sana.

Kuna mkoa nilienda mwaka 2022, nikafikia lodge X, ilikuwa nzuri kabisa ila vitanda na shower zake zilikuwa zishachoka. Nilirudi tena mwaka 2025 na nikakuta shower na vitanda vile vile 😳.

Wengi wanapenda kuifanya hii biashara ila hawajui kuifanya hii biashara, wanataka kuona hela zinaingia tu na sio kutoka.

Ukarabati pekee wengi wanaofanya ni kubadili wafanyakazi na kupaka rangi tu, ila vitanda, magodoro, shower za kuogea, kuboresha floor kwao ni kosa la jinai.

Wamiliki wa lodge na hotels mjitathmini sana juu ya hizo biashara zenu, msipende hela tu bali huduma ziendane na pesa mteja anayolipa.
MNAWAKOPA WATAFQNYIQ MAREKEBISHO

NA

TORCH
 
Kama basi linatembea, linaingiza faida vizuri, abiria wanaligombania na dereva hatoi malalamiko yoyote.. Kwanini uhangaike kubadilisha rangi mkuy? Kama hutaki lodge kalale nae kwako au vichakani huko.. Other wise TULIAAAAA... Kula nyama nyamaza.

Lalamika kama walikunyima sabuni ya kuogea tu.
 
Sio kweli ndani ya miaka 5 hela inarudi na faida juu yake, nazungumza kwa uzoefu, vitanda na magodoro unaeza viuza kwa mnada ukaongezea hela ukanunua vipya.
Low budget hotels hazina proper management. Mtu anaendesha kwa utashi wake. Ukikuta mmiliki anajqli na kupenda vitu vizuri hotel itakuwa nzuri ukikuta kinyume chake ndio hizo unazoziongelea.
Mmiliki anapata pesa hajali ubora tena.
 
As long as you make money na kurekebisha hapaongezi value ya wateja, Kwa Nini?
 
Maintenance is key--kwenye biashara hii,ndoo za rangi,vifaa vya bomba viwe standby kila wakati.
Kila mwezi(au miwili) unaweza ukafanya full renovation ya chumba kimoja tu...kwa mzunguko lets say una vyumba 10 kila kimoja kinakuwa kwenye hali nzuri--wateja hawatakauka.
Kwenye swala la management---vijana wako wengi tu wanaoweza kusimamia lodge--tafuta mama mmoja wa hapo mtaani ambae analipwa commision ya usafi na mtu mmoja wa reception--kama biashara ni kubwa,sogea juu kidogo tafuta mtu aliesomea hotelia akusaidie ku-manage(commision based)...the older the person the better.
Kila la heri.
 
Gharama ya ujenzi na faida haviendani,ni ngumu kufanya marekebisho Huku hujapata faida
 
Back
Top Bottom