Mkuu hongera kwa swali zuri na fikirishi.
Ingawa sielewi chochote kuhusu chanzo halisi cha ubaguzi huu wa chakula.
Zamani niliwahi kuuliza swali lenye kufanana na swali lako, lakini majibu yake sikuyafanyia utafiti wa kufanya kukidhi kiu yangu.
Tangia utotoni, nimekua huku nikiaminishwa baadhi ya vyakula flani flani, si kwa mpangilio huo wa walao nyama ama majani, kuwa ni 'mwiko' kuvitumia katika ukoo wetu na ndicho nilichotaka nikifahamu, kwa nini ni mwiko!
Nikaambiwa kuwa 'mwiko' huo ulianzia pale 'wahenga' wetu walipotumia baadhi ya vyakula na kisha kuwaletea mzio (allergy diet).
Ndiyo ikatokea kwamba watu fulani hawali hiki na wengine hawali kile.
Kwa hiyo, chochote alacho mtu na kisimletee madhara, kinafaa kuliwa, nikasema 'fine'.
Nikaja kuuliza tena kuhusu 'mwiko' wa mahusiano, wa mtu na ndugu yake kufanya mapenzi ama kuoana, mzee yule akawa mkali kwa maswali yangu, nilielewa ukali wake ulimaanisha nini, hadi pale mengine nilipokuja kupata majibu yake shuleni.
Sent using
Jamii Forums mobile app