Ni kwanini wanyama walao nyama (carnivorous) hawatumiki kama chakula cha mwanadamu?

Wanyama walao nyama, yaani carnivorous hawatumiki kama sehemu ya chakula cha mwanadamu karibu sehemu nyingi duniani.

Herbivorous, yaani wanyama walao majani, ndiyo hutumika kama sehemu ya chakula katika jamii nyingi.

Hii ni kutokana na mafundisho ya dini, mila au kuna madhara ya kisayansi?
Pia hapo ungeongezea Wanyama walao nyama hawalani wenyewe kwa wenyewe except mamba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sababu za kiimani ,malezi na utamaduni tu
Mbona wachina wanakula kila kitu na wanaishi miaka mingi tu
 
jibu lako mkuu nadhani lipo katika nature!.

tukiweza kuwala hao wanyama, tutaweza kula binadamu wenzetu.
 
Wanyama walao nyama, yaani carnivorous hawatumiki kama sehemu ya chakula cha mwanadamu karibu sehemu nyingi duniani.

Herbivorous, yaani wanyama walao majani, ndiyo hutumika kama sehemu ya chakula katika jamii nyingi.

Hii ni kutokana na mafundisho ya dini, mila au kuna madhara ya kisayansi?
Samaki sangara ni carnivorous tunamla[emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukila nyama ya fisi hutoboi hata wiki lazima parapanda italia
Wiki kadha Shinyanga waligawana nyama ya fisi kama kitoweo,hii inathibitisha hata carnivorous wanalika jamii ikihitaji.

Nilimsikia mkuu mmoja akiagiza kuwepo na bucha ya nyama pori,nafikiri huko tutakuta nyama za aina zote ikiwemo simba, chui, mamba, swala nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi pia hapa hua nashindwa kuelewa. Ila pia hua najiuliza mimi hua niko allergic kwa red meat, maziwa fresh na prawns(sina uhakika na spelling) je kuna cases ziko proved kuwa wanyama wala nyama nao hua wanakuwa na tatizo la allergy?
 
Wiki kadha Shinyanga waligawana nyama ya fisi kama kitoweo,hii inathibitisha hata carnivorous wanalika jamii ikihitaji.

Nilimsikia mkuu mmoja akiagiza kuwepo na bucha ya nyama pori,nafikiri huko tutakuta nyama za aina zote ikiwemo simba, chui, mamba, swala nk
Fisi yule walimgawana siyo kwa ajili ya kitoweo, hapana. Bali kila aliyechukua sehemu ya mzoga wa fisi yule, alichukua kwa ajili ya matumizi ya kuchanganya na dawa za uganga au uchawi; kwa kisukuma inajulikana kama "Jingila" au "Shingila".
Fisi ni mnyama anayehusishwa na mambo ya kichawi, kwa sababu huwa anafugwa na kutumiwa na wachawi kwenye shughuli zao za kichawi kama usafiri, pia fisi hutumwa na " boss" wake kutekeleza majukumu mbalimbali kama kukamata mifugo kwa watu wengine kwa ajili ya kitoweo kwa "boss". Fisi hutumwa pia kwenda ku-harrass kwa hasimu wa " boss" wake kama ishara ya kuonya.
Jingila (Shinyanga na Simiyu) au Shingila (Mwanza na Geita) ni vitu MAALUM vinavyotumika kuchanganya (reagents) kwenye dawa za kutibu au kuroga. Vitu hivi ni maalum kama viungo vya binaadamu, viungo vya baadhi ya wanyama, maji yaliyooshewa maiti, kamba aliyojinyongea mtu, kipande cha sanda, kipande cha ubao wa mlango wa jela au gereza, n.k.
 
Kwasasa tumezungukwa na vyakula vingi sana kuliko idadi ya watu, so kuchagua ni ruksa. Ila as time goes, idadi ya watu itakuwa kubwa sana kuliko vyakula vilivyopo, hapo ndio utajua kuwa almost everything kinaliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fisi yule walimgawana siyo kwa ajili ya kitoweo, hapana. Bali kila aliyechukua sehemu ya mzoga wa fisi yule, alichukua kwa ajili ya matumizi ya kuchanganya na dawa za uganga au uchawi; kwa kisukuma inajulikana kama "Jingila" au "Shingila".
Fisi ni mnyama anayehusishwa na mambo ya kichawi, kwa sababu huwa anafugwa na kutumiwa na wachawi kwenye shughuli zao za kichawi kama usafiri, pia fisi hutumwa na " boss" wake kutekeleza majukumu mbalimbali kama kukamata mifugo kwa watu wengine kwa ajili ya kitoweo kwa "boss". Fisi hutumwa pia kwenda ku-harrass kwa hasimu wa " boss" wake kama ishara ya kuonya.
Jingila (Shinyanga na Simiyu) au Shingila (Mwanza na Geita) ni vitu MAALUM vinavyotumika kuchanganya (reagents) kwenye dawa za kutibu au kuroga. Vitu hivi ni maalum ni kama viungo vya binaadamu, viungo vya baadhi ya wanyama, maji yaliyooshewa maiti, kamba aliyojinyongea mtu, kipande cha sands, kipande cha ubao wa mlango wa jela au gereza, n.k.
Duh hadi nimehisi kuwaogopa majirani zangu wasukuma
 
Wanyama walao nyama, yaani Carnivorous hawatumiki kama sehemu ya chakula cha mwanadamu karibu sehemu nyingi duniani.

Herbivorous, yaani wanyama walao majani, ndiyo hutumika kama sehemu ya chakula katika jamii nyingi.

Hii ni kutokana na mafundisho ya dini, mila au kuna madhara ya kisayansi?
Umeuliza swali zuri, ila binafsi sina jibu.
 
Kuna watu wanakula mpaka Omnivorous,sasa sijui huu ni ulafi!!😅
 
Wanyama walao nyama, yaani Carnivorous hawatumiki kama sehemu ya chakula cha mwanadamu karibu sehemu nyingi duniani.

Herbivorous, yaani wanyama walao majani, ndiyo hutumika kama sehemu ya chakula katika jamii nyingi.

Hii ni kutokana na mafundisho ya dini, mila au kuna madhara ya kisayansi?
Sababu hata hao wanyama wenyewe walao nyama hawalani wenyewe kwa wenyewe, (kwa maana hawawindani wenyewe kwa wenyewe wakalana)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwalimu wangu wa biology alitufunddisha kuwa sababu ni flow of energy. Kwenye majani kuna viinilishe vingi. Hivyo mnyama anayekula majani anakuwa na viinilishe vingi. Hivyo wanyama wanaokula nyama hula zaidi wanyama walao nyasi kwa sababu huwa wanapata viinilishe vingi kuliko wakila wanyama wengine walao nyama. Kwa hiyo mnyama alaye nyama kiasili havutiki kula myama mwenzake alaye nyama.
 
Back
Top Bottom