Ni kwanini wanyama walao nyama (carnivorous) hawatumiki kama chakula cha mwanadamu?

Ni kwanini wanyama walao nyama (carnivorous) hawatumiki kama chakula cha mwanadamu?

Wanyama walao nyama, yaani Carnivorous hawatumiki kama sehemu ya chakula cha mwanadamu karibu sehemu nyingi duniani.

Herbivorous, yaani wanyama walao majani, ndiyo hutumika kama sehemu ya chakula katika jamii nyingi.

Hii ni kutokana na mafundisho ya dini, mila au kuna madhara ya kisayansi?

Mbona nguruwe anakula nyama na anatumika [emoji23]

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hakuna mnyama asiyeliwa na ukiona haliwi jua ni eneo fulani tu kumbukumbu zao zinawazuaia kula lakini siyo kila mahali.
Mwili wa binadamu unatumia kumbukumbu nyingi mno kuanzia ndani ya seli mpaka kwenye viungo vya mwili kama macho ulimi,vionja ladha vingine (other taste buds).Kumbukumbu hizi zilizopo ndani ya miili yetu zinatufanya tupende kufanya mambo yaleyale zilizoyatunza hata vyakula tunaona ni vitamu kwa sababu ya kumbukumbu zilizopo kwenye ndimu zetu.
Unaweza ukawa wewe hukumbuki wahenga wako walikuwa wanakula nini nna wanachukia nini ila elewa kuwa kumbukumbu zao zimehifadhiwa ndani ya mwili wako na utajikuta unafanya kwa kujua au kutojua kuendana na kumbukumbu zilizopo ndani yako.
Wachina leo wanakula karibu kila mdudu na kila kiumbe kwa sababu kumbukumbu zao haziwazuii na hapa kwetu wapo wanaokula mbwa kwa sababu ladha ya nyama ya mbwa ilishakuwa stored kwenye miili yao.
"Ndiyo maana ya ule msemo hakuna jipya chini ya jua"....we are determined by memories and actions stored in our body "karma".
Hatuwezi tukasema wanyama fulani hawaliwi kabisa katika Dunia hii yenye jamii nyingi zenye kumbumbukumbu tofautitofauti katika maisha yao angalau tukisema katika eneo fulani la kijiografia kumbukumbu zao zinawazuia tutakuwa sahihi zaidi kuliko kusema "Hawaliwi"
Kwenye misitu ya Papua Guinea kuna "Cannibals" yaani binadamu wanaokula miili ya binadamu wenzao na ni kawaida tu kwao kwa sababu ndimu zao zina kumbukumbu kuwa ladha hiyo ni tamu na ni chakula kwao jambo ambalo leo ukiambiwa ufanye unaweza ukaona majibu kama hujatunza kumbukumbu hizo.
Kumbukumbu zetu ni gereza letu na ndizo zinazotawala na kutuongoza kwenye machaguo yeti mengi katika uso wa Dunia "we are full of memories".Unaweza kwa kujua au kutojua kujikuta unafanya mambo waliyokuwa wanafanya au wanapenda kufanya vizazi vingi vilivyopita kutokana na kumbukumbu zilizohifandhiwa ndani ya mwili wako.
 
Ukiondoa fisi anayekula kila kitu, wanyama wengine wawindaji huwa hawali wawindaji wenzao, mfano. utagundua simba hana kawaida ya kuwinda na kumla fisi au chui. Lakini utashangaa kuna binadamu hasa wachina wanakula chochote kinachosogea, unategemea wasipate magonjwa yasiyoeleweka chanzo kama corona.......akikatiza bundi, kobe sijui popo ni kula kwa kwenda mbele...dah!
 
Siyo

Kweli unachosema..hao viumbe hawajaweza kuliwa leo na kama ni magonjwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja namna hiyo angalau ukiniambia juu ya Genetically modified organism "GMO" naweza kupata mkuno akilini.
 
Nadhani carnivorous animals shughuli pevu na hatari kuwawinda na pili taabu kuwafuga(itabidi kuwalisha nyama) ndio maana hawatumiki kama chakula. Dhana ya mbichi hizo hazifai creeps in.
 
Hujui kuna wanyama ambao wanabeba vimelea hatari vya magonjwa....unaelewa kitu kinachoitwa carrier status au pathogen load au na wewe ndo wale wanaokula chochote kinachokatiza mbele..
 
Kuna sababu kadhaa Mkuu. Kama ifuatavyo;

1. Sababu za kidini.
Dini nyingi hasa zenye asili ya Mzee Abrahamu zinakataza jambo hilo. Dini hizo ni pamoja na Dini ya kiyahudi, Uislam na Ukristo.
Sababu kuu kwa hawa ni imani kuwa Mungu kakataza.

2. Sababu za Kisayansi.
Kwenye Food web au Food Chain. Au kwenye Nitrogen Cycle of Life.
Kuna mambo yafuatayo.

Kuna Producer ambao ni uoto wa asili au wakutengeneza. hapa kuna mimea na miti kwa jamii zake. Hawa ndio hutegemewa na viumbe wote. Mimea huchukua madini na virutubisho vyote kutoka kwenye udongo na kuuhifadhi kwenye Mizizi, shina na majani ya mimea.

Ardhi inavirutubisho 100%. Virutubisho hivyo ni madini kama vile calcium, iron, nitrate, carbonhydrate n.k. kwa asilimi zote.

kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine katika food web au chain 10% zinapungua.

Mmea hupata virutubisho kutoka ardhini kwa 90%. Mmea hauwezi kula asilimia zote kutoka kwenye ardhi, hivyo kwenye ardhi itanyonya madini kaa asilimi 90.

Sasa Wanyama wala majani Ambao huitwa Herbivoras, wao nao katika hatua yao inapungua asilimia 10 kutoka kwenye 90, Hivyo huwa 80% Hivyo wanyama wala majani wana 80% ya virutubisho kama ukiwala.

Unaweza kuona tofauti ya mtu anayekula mboga za majani, nafaka na matunda na wale wanaokula nyama za kuku, mbuzi n.k.

Wale wanaokula kutoka kwa Producer ambao ni mimea huwa na virutubisho vingi mwilini tofauti na wale wala nyama.

Tukija kwenye Wanyama wala nyama ambao ni Carnivoras. Hawa nao hupungua 10% za virutubisho kutoka kwa Herbivorus ambao walikuwa na 80. Hivyo wao wanavitubisho kwa 70%.

Wanyama hao ni kama vile Mbwa, Simba, chui, n.k.

Wanyama hawa ukiwala unapata virutubisho vichache ambavyo seli za mwili wako zitakosa baadhi ya madini na nutrient hali inayoweza sababisha maradhi yasiyoambukiza na yasiyo na dawa kama vile Kansa.

Mlolongo upo hivi.

Ardhi 100%
^
Mimea 90
^
Wanyama wala mimea 80
^
Wanyama wala nyama 70
^
Viumbe wala vyote 60.

Kisayansi mtu hushauriwa zaidi kula nafaka, matunda na mboga mboga. Na mtu wa hivi anauhakika wa kuishi maisha marefu pasipo kuumwa.

Lakini watu wanaokula nyama au wanyama wala nyama hukumbwa mara kwa mara na magonjwa yasiyoeleweka.

Nadhani nimejibu swali lako kwa sehemu kubwa
 
Nadhani carnivorous animals shughuli pevu na hatari kuwawinda na pili taabu kuwafuga(itabidi kuwalisha nyama) ndio maana hawatumiki kama chakula. Dhana ya mbichi hizo hazifai creeps in.
Mmmh..hawatumiki kama chakula wapi Mkuu?
Naunga mkono hoja yako kwenye shughuli pevu ya kuwawinda ila kwenye kuliwa wanaliwa tu.
Ngiri ni mnyama hatari sana pamoja maneno yake kuwa nje kama visu anawindwa na wanaliwa tu.
 
Wanyama walao nyama, yaani Carnivorous hawatumiki kama sehemu ya chakula cha mwanadamu karibu sehemu nyingi duniani.

Herbivorous, yaani wanyama walao majani, ndiyo hutumika kama sehemu ya chakula katika jamii nyingi.

Hii ni kutokana na mafundisho ya dini, mila au kuna madhara ya kisayansi?
kuku anakula mende, minyoo hata nyoka akikaa vibayaanaliwa na bado mbona tunamla..
 
Sababu ni hii hapa:
Chakula halisi na bora anachotakiwa kula binadamu ni majani, matunda na mizizi. Sasa unapokula nyama ya mnyama anaekula majani maana yake unafanikiwa kula mabaki kidogo ya majani, unapoenda kula nyama ya mnyama anaekula nyama maana yake hakuna unachopata pale, yaani virutubisho hupungua kwa kasi kadri unavyosogea kutoka majani, mnyama anaekula majani kuelekea mnyama anaekula nyama. Mtiririko uko hivi:

Majani—mnyama anaekula majani—Mnyama anaekula wanyama

Yaani kadri unavyosogea mbele ndivyo virutubisho hupungua!
 
Mkuu hongera kwa swali zuri na fikirishi.
Ingawa sielewi chochote kuhusu chanzo halisi cha ubaguzi huu wa chakula.
Zamani niliwahi kuuliza swali lenye kufanana na swali lako, lakini majibu yake sikuyafanyia utafiti wa kufanya kukidhi kiu yangu.

Tangia utotoni, nimekua huku nikiaminishwa baadhi ya vyakula flani flani, si kwa mpangilio huo wa walao nyama ama majani, kuwa ni 'mwiko' kuvitumia katika ukoo wetu na ndicho nilichotaka nikifahamu, kwa nini ni mwiko!

Nikaambiwa kuwa 'mwiko' huo ulianzia pale 'wahenga' wetu walipotumia baadhi ya vyakula na kisha kuwaletea mzio (allergy diet).

Ndiyo ikatokea kwamba watu fulani hawali hiki na wengine hawali kile.
Kwa hiyo, chochote alacho mtu na kisimletee madhara, kinafaa kuliwa, nikasema 'fine'.

Nikaja kuuliza tena kuhusu 'mwiko' wa mahusiano, wa mtu na ndugu yake kufanya mapenzi ama kuoana, mzee yule akawa mkali kwa maswali yangu, nilielewa ukali wake ulimaanisha nini, hadi pale mengine nilipokuja kupata majibu yake shuleni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna siku mzee aliniusia nisije kujaribu kuvuta bange maana nitakua chizi, kwenye ukoo wao ni mwiko kusmoke weed.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwasababu kwenye energy level piramid kiasi cha energy hupungua kadiri unavyoacha kutumia chakula cha mimea ndio maana mtoto wa nyumbu akizaliwa ni swala la dk anaanza kukimbia wakati wa simba inamchukua muda.
Hivyo kula nyama ya mla nyama ni kula chakula chenye less energy
Na the least energy ni decomposers kama bacteria

Sent using Jamii Forums mobile app
KWAHIYO unamaanisha Mtoto wa Rastafari akizaliwa ni dakika tu ataanza kukimbia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chunguza utagundua hili.

Wanyama wote walao nyama hawazaliani sana kama wanyama walao majani. Kiafya ukila nyama ya simba, mbwa, chui nk hupati madhala yoyote lakini kwa kuwa wanyama hao hawazaliani sana, wangekuwa wanaliwa na binafamu lazima wangeisha.

Lakini siyo tu sisi wanadamu ndiyo hatuwali lakini pia hata wao kwa wao hawalani. Fisi tu ndiyo hachagui aina ya nyama. Kwa tafsili hiyo Mungu ndiyo aliyetunyima utashi wa kula nyama ya wanyama walao nyama maksudikaly

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, utashi nini maana yake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujui kuna wanyama ambao wanabeba vimelea hatari vya magonjwa....unaelewa kitu kinachoitwa carrier status au pathogen load au na wewe ndo wale wanaokula chochote kinachokatiza mbele..
Nimekukatalia kwa sababu hao wanyama hawajaanza kuliwa mwaka jana au mwaka huu.Wanaliwa from the time immemorial na kama ni carriers wa vimelea ina maana hawajaanza leo ni jambo ambalo lipo hivyo lilivyo. Ukiangalia hoja yangu nimesema angalau tukisema kama kuna genetic modification au naweza kuongeza 'gene mutation' ndiyo tunaweza kusema tatizo hili lina mawanda mapya.
 
Binadamu hatakiwi kula hata nyama licha ya mnyama mla nyama

Kwa asili mifumo ya mimea ambayo ni producers ina software rahisi kudigest kwenye mifumo yetu sisi tutegemeayo nishati yake

Kwa asili wanyama wote ni herbivorous ila kuna baadhi ya species kupitia climatic change zilishindwa kurejelea uasili wake na kusababisha utegemezi wa kudumu ndio hao carnivores

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mafundisho ya dini,mila na ugumu wa kuwawinda na kuwaua carnivorous.
Jaribu kumchinja paka uione shughuli yake.
Wanyama walao nyama, yaani Carnivorous hawatumiki kama sehemu ya chakula cha mwanadamu karibu sehemu nyingi duniani.

Herbivorous, yaani wanyama walao majani, ndiyo hutumika kama sehemu ya chakula katika jamii nyingi.

Hii ni kutokana na mafundisho ya dini, mila au kuna madhara ya kisayansi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanyama walao nyama, yaani Carnivorous hawatumiki kama sehemu ya chakula cha mwanadamu karibu sehemu nyingi duniani.

Herbivorous, yaani wanyama walao majani, ndiyo hutumika kama sehemu ya chakula katika jamii nyingi.

Hii ni kutokana na mafundisho ya dini, mila au kuna madhara ya kisayansi?
Mbona mimi Carnivore ila nakula wewe Sky eclat?
Inategemea na aina ya mnyama mla nyama ni gender gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom