Ni kweli Cleopatra, mwanamke mrembo kuliko wote duniani alikuwa wa Misri?

Ni kweli Cleopatra, mwanamke mrembo kuliko wote duniani alikuwa wa Misri?

Huyo ndo cleopatra, alikuwa ni farao wa Vll wa misri, hakuwa mwanamke mzuri kuliko wote duniani, wanawake hupenda kusifiwa kwa uzuri na yy kipindi hicho alikuwa ni mtawala hivo alitaka kila mtu amwone yy ndio mzuri kuliko mwanamke yeyote, alikufa kwa kuumwa na nyoka cobra aliokuwa anawafuga"
Mkuu....
Hakuna ushahidi ulio wahi kueleza kinaga ubaga kuhusu kilicho pelekea kifo cha huyu mwana mama Cleopatra.
Pia kuna habari zinasemekana inasadikiwa alikufa kwa kuwekewa sumu
 
hata mim nliwah sikia kitu kama hicho, tupeni details bs
Warumi walitia chumvi historia ya Kleopatra wa Saba

Kleopatra lakini wako wengine hawalifahamu jina hili. Kleopatra ni mmojawapo wa watawala wa Misri wa kale, akifahamika kuwa ni mwanamke aliyeweza kuzikamata nyoyo za wanaume waliokuwa na mamlaka makubwa wakati ule wa utawala wa Rumi uliokuwa ukiitawala dunia, wakati huo, kama taifa kubwa la Marekani leo hii.

Mwanamke kutoka Misri, aliyeweza kuutumia vizuri uwanamke wake kukamilisha kile alichokuwa anakiamini kuwa sahihi na kuweza kumteka kimawazo na kimapenzi Julius Kaisari, Mark Antony na wanaume wengine ambao walikuwa watawala wa dola kubwa ulimwenguni. “Maisha ya Kleopatra yalikuwa ya kushangaza mno, alikuwa ni malkia wa ajabu, mrembo aliyeweza kukamata mioyo ya watu wengi maarufu ulimwenguni.” Haya yanasemwa na Daktari wa Falsafa, Zahir Hawass, mtaalamu wa masuala ya kale kutoka Baraza la Mambo ya Kale nchini Misri. Unapotaka kuutambua ukweli juu ya jambo lolote ni vizuri kupata ushahidi wa watu zaidi ya wawili, kama wasemavyo wayahudi kuwa ushahidi wa watu wawili ni wa kweli lakini kumbuka unaweza ata kudanganywa na watu hao wawili wakati mwingine.

Unapotaka kutambua maisha ya Kleopatra wa saba ni vizuri kusikiliza kutoka upanda wa Misri na pia kusikiliza upande wa iliyokuwa dola ya Rumi ambapo kwa hakika mwanamke huyu imara aliwahi kuishi na watawala wa Rumi na kuzaa nao watoto; Julius Kaisari na Mark Antony.

Cleopatra wa Saba alizaliwa mwaka 69 kabla ya Yesu na alifariki Agosti 12 mwaka 30 kabla ya Yesu, alikuwa ni Farao wa Misri ambaye alifariki akiwa na umri mdogo mno. Huku jina Kleopatra likitokana na neno la kigiriki Kleopatra likimanisha mtu kutoka familia bora likisimama upande wa majina ya kike na kinyume ni Kleopatrols likimaanisha mwanaume.

Doktari Robert Steven Bianchi kutoka makumbusho ya Sanaa za Misri huko Tokyo Japan anatambua kuwa Warumi kwa sehemu kubwa walimtazama Kleopatra kwa jicho baya na jicho lisilo jema, jicho la kihasidi, tangu wakati ule, ata maandishi yao yanaonesha mtazamo huo lakini Kleopatra kwa sehemu kubwa amechangia mengi katika ustaarabu wa Misri na dola nzima ya Rumi.

“Warumi waliongeza chumvi katika simulizi ya maisha ya Kleopatra, walimsimulia kama mwanamke aliyejitongozesha kwa wanaume na kahaba mkubwa, aliyeweza kufanya mapenzi na mwanume yoyote wa Roma.” Kleopatra alikuwa na asili ya Ugiriki ya zamani baada ya utawala wa Axelander Mkuu kufariki wakati wa utawala wa Hellenistic ambapo katika uhai wake alikuwa akizungumza Kigiriki na alikataa katakata kuzungumza lugha ya Kimisri na wakati wa utawala wake Kigiriki na Kimisri zilitumika kwa pamoja kama lugha rasmi za mahakama.

Katika kuitawala Misri Kleopatra alitawala sambamba na baba yake na baadaye sambamba na kaka yake akishirikiana kwa karibu mno na Julius Kaisari ambaye alimjenga mno kuwa mtawala wa Misri na baadae kuzaa naye mtoto. Daktari Christina Riggs kutoka chuo Kikuu cha Mashariki mwa Anglia bado anamtazamo wa Warumi kuichezea historia ya Klepatra wa Saba.

“Ata umaarufu wa Kleopatra, yale tunayotambua ni simulizi tu, la muhimu kujua kuwa alikuwa mtawala wa Misri, ukipata ushahidi wa wamisri tutapata mtazamo wa utawala wa Kleopatra ulivyokuwa na si Warumi.” Waandishi na vyombo vya habari vinaweza kuliona tukio moja likasimuliwa kwa namna tafauti, kila mmoja akiwa na malengo yake kulieleza tukio hilo namna alivyopenda liwe, ndivyo ilivyokuwa kwa Warumi wa kale. Ikumbukwe kuwa Julius Kaisari aliuwawa mwaka 44 kabla ya Yesu huku Kleopatra akiungana na Mark Antony aliyejulikana kama Augustus walizaa nae watoto mapacha wawili Klepatra Selene II na Alexander Helios na baadaye wakazaa mtoto wa kiume mmoja. Baada ya kushindwa vita na Ocktavian, Mark Antony alijiua. Baada ya kifo hicho Caesarion mtoto wa Kleopatra na Julius Kaisari alijitangaza mtawala lakini punde tu aliuwawa kwa amri ya Octaviana na hapo hapo Misri ikawa sehemu ya Roma. Mama wa Kleopatra inaaminika kutofahamika lakini inahisiwa kuwa ni Cleopatra wa tano Kutokana na hali ya ufisadi na kutoa uhuru wa madaraka katika dola yake kulisababisha mapinduzi na kutolewa madarakani. Klepatra wa sita VI alifariki katika mazingira yasiyofahamika ambapo iliaminika kuwa alipewa sumu katokana na ushindani wa madaraka.

Mwaka 55 kabla ya Yesu Ptolemy Baba wa Kleopatra wa Saba alirejea akiwa na uungwaji mkono mkubwa wa Warumi na yule aliyesababisha kifo cha mama wa Klepatra alifungwa baadaye kunyongwa. Haya yote yakitokea Kleopatra wa Saba , tunayemzungumzia leo hii alikuwa na umri wa miaka 14 yaani mwali kabisa, akiwa msaidizi wa karibu wa baba yake, huku majukumu yake yakiwa madogo. Miaka minne baadaye Baba wa Kleopatra wa Saba alifariki dunia huku akiaacha wosia kuwa bintiye ambaye sasa alikuwa na miaka 18 tu na kijana wake wa kiume yaani kaka wa Kleopatra wapewe madaraka kwa pamoja. Miaka mitatu ya utawala wao ilikuwa migumu mno. Kwani nyota mbaya iliwaandama wakikumbwa na mafuriko kutoka mto nile, njaa kubwa na uchumi kwenda kombo.

Baadaye Kleopatra alikaa na kaka yake na kuwa mke na mume lakini alimzidi kete kaka yake na kutochangia mamlaka huku Kleopatra akiwa kinara wa madaraka.

Hakika hata mm nina hamu sana
 
Umeelezea vizuri sio ki_dot com,maana kuna watu wametulisha tango poli hapa...ni vizuri umefafanua historia yake..
 
Acheni nyinyi, siku hizi kuna makeup, digital cameras na vinginevyo hata mwanamke awe mmbaya kama Remmy atatengenezwa awe mzuri. Cleopatra hakuwahi kupigwa picha, alichorwa. Kilikua kifaa si cha kawaida.
mimi napenda kuona picha ya Maria Antoneta nasikia naya alikua mzuri sana
 
Habari wanajamii forum
Katika historia ya ulimwengu huu nasikia kulitokea mwanamke mmoja mzuri sana aliyeitwa CLEOPATRA ambaye alikuwa mtawala wa misri,na inasemekana hatakuja kutokea mwanamke mzuri tena kama CLEOPATRA,sasa nilikuwa naomba kwa wanaofahamu historia yake vixuri sana watuelezee ili tupate cha kujifunza kuhusu huyu CLEOPATRA
Now kuna wanawake ni wazuri kama hawajazaliwa ndugu,ni kama wa viwandani,hvyo siamini kua huyo CLEOPATRA ndo mzuri kuliko wote toka enzi hzo mpaka leo siyo kweli
 
Habari wanajamii forum
Katika historia ya ulimwengu huu nasikia kulitokea mwanamke mmoja mzuri sana aliyeitwa CLEOPATRA ambaye alikuwa mtawala wa misri,na inasemekana hatakuja kutokea mwanamke mzuri tena kama CLEOPATRA,sasa nilikuwa naomba kwa wanaofahamu historia yake vixuri sana watuelezee ili tupate cha kujifunza kuhusu huyu CLEOPATRA
Mafarao walikuwa watu weusi,,hivyo Cleopatra alikuwa ni mwanamke mweusi ti,,,wazungu waongo wamebadilisha historia
 
Huo uzuri wake kipimo chake ni nini? Alikuwa na kipi cha ziada kwenye mwonekano wa wanawake wengne? Binadamu wote ni sawa
 
Julius Cesar aliyekua mtawala wa Roman Empire alikwisha kabisa kwa Cleopatra ukumbuke Roman Empire ilitawala dunia kabla ya Uingereza. Cleopatra alikua na asili ya Afrika.
umenikumbusha seriez moja kari sana inaitwa Rome
ukitaka kujua kuhusu huyu mwanadada na habari za julius na mark antony pamoja na ukahaba wa huyu binti tafuta seriez inaitwa ROME
 
Mafarao walikuwa watu weusi,,hivyo Cleopatra alikuwa ni mwanamke mweusi ti,,,wazungu waongo wamebadilisha historia
Kwaivyo hapo ndio umetupa historia jinsi wazungu walivyo badilisha hizi aneno[emoji15]
 
Habari wanajamii forum
Katika historia ya ulimwengu huu nasikia kulitokea mwanamke mmoja mzuri sana aliyeitwa CLEOPATRA ambaye alikuwa mtawala wa misri,na inasemekana hatakuja kutokea mwanamke mzuri tena kama CLEOPATRA,sasa nilikuwa naomba kwa wanaofahamu historia yake vixuri sana watuelezee ili tupate cha kujifunza kuhusu huyu CLEOPATRA

Uzuri uko kwenye macho ya yule anaeangalia kile kitu.

Hata Elizabeth Taylor walimsema hivyo hivyo. Lakini ukitaka kujua historia ya Cleopatra, google utapata taarifa au nenda youtube utakuta filamu zake.
 
Mkuu....
Hakuna ushahidi ulio wahi kueleza kinaga ubaga kuhusu kilicho pelekea kifo cha huyu mwana mama Cleopatra.
Pia kuna habari zinasemekana inasadikiwa alikufa kwa kuwekewa sumu

Historia inasema alikufa kwa kuumwa na nyoka cobra (alimuweka nyoka kwa makusudi siyo bahati mbaya)
 
Acha mbwembwe ulimuona au muhemko umekusukuma kusema,umemuona kwenye picha za kuchora hahaha we kiboko,historia inamuelezea alikuwa ni mzuri............Ninakushanga kidogo alikuwa mzuri enzi zile na usijidanganye walikuwa wanatumia make up sana, dunia ya kileo kuna warembo acha kabisa bila hata make up.....
Maneno huumba watu. Ndio maaana tunasoma story mbalimbali, binti anasifiwa kwa uzuri mpaka unamkubali. Yote hiyo ni kazi ya sanaa. Zamani mtu unamweleza wasifu wa mtu anamchora mpaka unakubali kuwa ndiye.
Mchoraji wa kifaransa Leonardo da Pinci alichora watu mbalimbali ama kwa kusoma maandiko mbalimbali au kwa kupewa maelezo namna wanavyofanana. Ndio maana picha za Yesu, na zingine zilichorwa na tukakubali kuwa alikuwa anafanana nazo.
Tukubali Cleopatra alikuwa mzuri!
 
huyo cleopatra hamzidi mke wangu, my wife is such a beautiful and innocent woman, she always smiles sweeter than my money.
 
@bintimkongwe,
Ebu jaribu kupitia hapo chini pengine tunaweza tukaenda sawa ili kwa pamoja tukaelimika
Historia inasema alikufa kwa kuumwa na nyoka cobra (alimuweka nyoka kwa makusudi siyo bahati mbaya)
Cleopatra alizaliwa Alexandria mwaka wa 69 K.K (kabla ya kristo),Wakati wa utawala wa familia ya Ptolemy kwenda kwa Ptolemy XII. Cleopatra lilitokea kuwa jina maarufu ndani ya familia, kwani mama yake alilipenda kiasi cha kuchukiza kwa wengine lakini pia ndiye alikua binti mkubwa . Cleopatra hakua Mmisri, ispokuwa mMacedonia familia yake ikitoka katika kipindi cha utawala wa Alexander the Great.

Cleopatra alikuwa mtawala wa kwanza katika familia yake ambaye aliongea lugha halisi ya Misri.

[http://1]URITHI WA UTAWALA WA PTOLEMY

Mfalme wa Misri ,Ptolemy wa XII ,anakufa mnamo mwaka wa 51 K.K. anaacha utawala kwa kijana wake mdogo mwenye miaka 12 Ptolemy XIII. Lakini anaagiza kwamba, kijana huyu atawale pamoja na dada yake mkubwa, Cleopatra. Pia ni lazima amuoe, kama desturi ya utawala wa ukoo wa Ptolemy, ingawa ndoa hiyo ilikua ni kama kuigiza.

ukizingatia umri wa mumewe huyo, Cleopatra alitawala yeye binafsi kama atakavyo.

Cleopatra mwenye miaka 18 mapema anathibitisha umahiri na uwezo mkuu wa kutawala, hususani katika historia ya kipindi hicho cha Medditerania. Lakini ukaribu wake na utawala wa Roma, baadae unakuja kupoteza uhuru wa Misri.

Caesar na Cleopatra: 48-44 K.K

Kuwasili kwa Julius Caesar Alexandria, kunampa fursa Cleopatra kuonekana Ulimwenguni ,kwa wakati huo. Anaachia Misri, mikononi mwa Julius Caesar ambaye baada ya kushinda vita Pompey anakua mtawala mwenye nguvu katika dola ya Roma.

Julius Caesar anaamua kupumzika kati ya 47 – 7 K.K huko Misri, akimsaidia Malkia huyu hata kuangamiza majeshi ya kaka yake (ambaye hakuweza kufua dafu).

Mara baada ya Caesar kuondoka Alexandria , Cleopatra anajifungua katika majira ya Kiangazi mnamo mwaka wa 47 K.K, anadai kuwa mtoto ni wa Caesar, na pia anamfanana sana .

Katika mwaka wa 46 K.K Caesar anamualika Cleopatra Roma pamoja na mwanae (ambae mara baada ya kuzaliwa alipachikwa jina Caesarion, “Caesar mdogo) ambao walikaribishwa katika jumba la kifahari likiwa na kila aina ya anasa. baadae caesar anauwawa.

Baada ya Caesar kuuwawa mwaka wa 44, Cleopatra aliamua kurudi Misri na mwanae.

ANTONIUS NA CLEOPATRA, 41- 31 K.K

Misri ya Cleopatra bado ni utawala ambao ni huru. Lakini karibu kila sehemu ya ukanda wa Mediterrania unajihusisha na siasa za Roma na kuna uvumi umeenea Roma kwamba Cleopatra amemsaidia “Cassius, mmoja kati ya waliomuua Caesar.

Katika majira ya kipupwe mnamo mwaka wa 41, Marcus Antonius anaamuru majeshi ya Roma kwenda upande wa Mashariki, na anaamuru Cleopatra aje aeleze juu ya tuhuma dhidi yake katika makao makuu yake huko Anatolia.

Cleopatra anavuka medditerania kwenda kumuona Marcus Antonius, lakini akiwa katika hali ya ujeuri, tena akiwa hana simanzi.

Kambi ya Antonius iko Tarsus, maili kadhaa kwenda mto Cydnus. Malkia anawasili akiwa katika Boti ya kifahari , akiwa amevaa mavazi yakuvutia ya mahaba , yenye asili ya Kigiriki. Hazuiliki kutamanika, na mapenzi yake mara yanaangukia ndani ya nyumba ya jenerali Marcus Antonius.

Cleopatra anamualika Antonius amtembelee Alexandria.

Anakubali mwaliko wake kwenda Misri kumtembelea, na anawasili Alexandria wakati muafaka kwa ajili ya kupumzika wakati wa majira ya Baridi.

Baada ya Antonius kuondoka kurudi Roma, Cleopatra patra anajifungua mapacha, mvulana na msichana. Wanakaa muda mrefu, hadi mwaka wa 37 K.K ndipo Cleopatra na wanawe wanaungana tena na Antonius.

Antonius Anamuagiza kuja Antioch, Syria ambako huko anamuoa.

Sasa wanajionesha waziwazi pamoja. na wanaungana kumpinga Octavian, mpinzani mkubwa wa Antonius katika Roma.

Jenerali Antonius akiwa na jeshi lenye nguvu eneo la Mashariki , anakua na uwezo wa kumpa mkewe huyo mapokezi makubwa ya ndoa zaidi ya yale yaliokuwa mashariki ya kati (Syria).

Katika desturi ya tawala nyingi za Mashariki, Cleopatra na Antonius sasa wanakua na uwezo wa kuabudu katika miungu mmoja. Katika Ugiriki wanakua “Dionysus (Antonius) na Aphrodite (Cleopatra), katika desturi za wamisri wanakua Osiris na Isis, hali kadhalika.

Makutano katika Alexandria 44 K.K

Makutano wengi wanakusanyika katika Alexandria, macho yao yakiangalia yanayojili toka kwa utawala huu, Katika jukwaa kuu ameketi Antonius na Mkewe Cleopatra akiwa amevaa mavazi ya sherehe maalum mithili ya miungu wa kike wa Misri.

Na katika viti vingine vinne vya kifalme wameketi watoto wao wote watatu, pamoja na “Caesar –mdogo”, mtoto mkubwa wa Cleopatra, kwa Julius Caesar.

Mnamo majira ya jioni katika tafrija hii, ambayo baadae ilijulikana kama “harambee katika Alexandria”, Antonius anaugawa utawala wa Medditerania Mashariki kwa familia yake hiyo mpya.

Antonius anamtangaza Cleopatra kuwa “Malkia wa Wafalme, na “Caesar-mdogo kuwa Mfalme wa Wafalme, kwa pamoja wakitawala Misri na Cyprus. na tawala zingine kwa watoto wao. Kwa Alexander, kijana wake mkubwa (umri miaka 6), anampa sehemu ya mashariki mwa Euphratia; kwa Mapacha, dada zake Alexander, Cleopatra, anawapa Libya na Tunisia, na kwa kijana wake mdogo, Ptolemy Philadelphus (miaka 2) ambaye amevaa mavazi ya kihistoria ya Macedonia, anamgawia Syria na sehemu kubwa ya Anatolia.

Inakua sherehe inayovutia, lakini ambayo baadae italeta uhasama na vita.

Actium na baadaye: 31-30 K.K

Mapigano kati ya majeshi ya Octavianus na yale ya Antonius na Cleopatra yanafanyika Actium, Ugiriki katika mwezi September. Pande zote mbili, wana majeshi makubwa ya miguu na yale ya farasi, lakini pia swala jingine ni meli za kivita za Roma, waliokuwa nazo pia.

Antonius na Cleopatra wanafaida ya kuwa na meli 500, 100 zaidi ya zile za Octavianus ambazo ni 400. Hizi ni zana za mbao ambazo ni imara sana. Zikiongozwa na na jeshi mahiri linalofikia askari hadi ya 250. Antonius anapanga jeshi lake la meli, pamoja na Cleopatra na majeshi yake nyuma, hazina kubwa ya Misri, tayari kwa mapigano.

Chanzo halisi cha mapigano haya hakijulikani. Lakini Octaviunus ameenda kinyume na matakwa ya wenza hawa wa utawala wa Mashariki.

Katika mapigano ya Actium meli za Octavianus zilishinda;

Katika hatua flani, Antonius anamjulisha Cleopatra juu ya meli zake , na mpango wakuvunja mapigano na kutoroka nae.

Antonius na Cleopatra wanafanikiwa kurudi, katika milki ya Cleopatra. Lakini wote wanaamua kujinyonga katika mwaka unaofuata, wakati Octavianus alipowasili Misri na jeshi lake. Marcus Antonius anaamua kujiua, malkia alijaribu kumshawishi kutofanya hivyo, lakini ilishindikana. Alielewa ya kwamba angepelekwa Roma na kuoneshwa kama mfungwa mbele ya halaiki. Hapa aliamua kufa tar. 12 Agosti 30 KK.

[http://3]

“asp” nyoka aliemuu Cleopatra 30 K.K

Cleopatra anaamua kujiua , kama ishara ya ushujaa mkubwa. Mara nyingi alichukulia “serious” uwajibikaji wake kwa Misri. Na pia ndiyo mtawala pekee wa kutoka ukoo wake aliejifunza na kujua kuongea lugha ya Misri.

Malikia anatambua kama akiwa hai tayari atakua mfungwa wa Octavianus.

Akilindwa na askari wake wachache katika sehemu ndogo ya makazi yake, anaagiza sumu ndogo ya nyoka, asp, ambayo inaingizwa kwa siri kupitia kwenye kikapu chake anachotumia kuletewa matunda.

[http://4]

Cleopatra anavaa mavazi yake mazuri ya ki-malikia, na analala katika kiti chake cha dhahabu. anamweka “asp” katika maziwa yake. Akijitoa kafara kwa “Amen-Re” mungu wa jua wa Misri.

Anakufa kwa sumu ya nyoka huyu (asp).

Muda wa mwisho wa uhai wa Malkia unakua kama “maigizo”, na unakumbukwa sana katika historia ya maisha yake. Na pia unaweka kikomo cha utawala wa Ptolemy katika Misri.

Octavianus alimtafuta pia Caesarion kwa sababu aliogopa mtoto wa Caesar angekuwa hatari kwake, akamuua. Akawachukua watoto wote watatu wa Marcus Antonius, akawaonesha mbele ya halaiki ya Roma kuonesha ushindi wake.

Pia anaichukua Misri kuwa sehemu ya utawala wa Roma, na kuchukua milki zote za ufalme wa Misri.
 
Back
Top Bottom