Jina la Cleopatra sio Jina geni masikioni mwa wengi, malkia aliyeitikisa misri katika Enzi zake za utawala.
Hata hivyo , inasemekana Cleopatra alikua maarufu kutokana na mvuto na uzuri aliokua nao , ukweli ni kwamba cleopatra hakuwa mzuri kama baadhi ya picha , statue na michoro mbali mbali ilivyom portray mwana mama huyo, swali je? Kwa nini alikua maarufu kuliko Ma cleopatra wote waliotangulia?, ni kwa nini viongozi wenye ushawishi mkubwa kama Julius na Marc Antony walinaswa na cleopatra ambaye tunaambiwa hakuwa mzuri wa sura na kulikua na wanawake wazuri kumzidi?
Jibu ni hili , tunaambiwa cleopatra alikua Ana akili nyingi sana na ushawishi mkubwa sana katika muda wake, alikua ni msomi na mwenye haiba ya kipekee sana na alikua ni mtu wa watu , hata Caesar na mark Antony walivutiwa na cleopatra kutokana na personality yake na akili alizokua nazo hasa kwenye mambo ya siasa, so waliona wakimtumia cleopatra itakua ni njia rahis zaidi kwa wao kufanikisha mambo Yao ya kisiasa.
Cleopatra Alipewa cheo kama malkia wa Makahaba( Queen of whores) , kutokana na tabia yake chafu ya kubadilisha wanaume kila wakati, Alizaa na Marc Antony pamoja na Caesar ambaye alikua ni mume wa mtu , pia alikua na mahusiano ya kimapenzi na kaka yake wa damu kabisa .
Huyo ndo cleopatra ninayemjua, pengine wewe ulishasikia mengi zaidi kumhusu mwana mama huyu aliyekua maarufu zaidi duniani , share chochote ulichokuwa nacho tujifunze
Warumi .