Joni, kwa taratibu za kiutumishi na nidhamu, huyo dereva kama kweli kafanya hivyo, kakosea sana kumuacha Nape, hilo ni kosa na dereva anaweza poteza kazi yake. Dereva hata kama boss wake katumbuliwa, inafaa amchukue na kumrudisha hadi nyumbani au ofisini kwake, kumbuka Nape bado hajakabidhi ofisi yake kwa Waziri mpya wakati tu ametumbuliwa, pia katika gari unaweza kuta kuna vitu vidogo vidogo vya Nape, mfano laptop au simu au nyaraka zake au nguo au hata kibegi chake, hivyo dereva kama kamuacha ni kosa.