Ni kweli hili shirika wanatoa pesa za bure?

Ni kweli hili shirika wanatoa pesa za bure?

Nimekutana na hii post kwa mtu wa karibu tunayefahamiana kupewa million Tano kwa kujisajiri kwenye hilo shirika
Post hii

"wengi walighairi ila ni ukweli nilipokea hizi hela kutoka USAID promotion ni halali wala sio mkopo.Unalipa ada kulingana na mchango utakaochagua iwapo uko na hela zinazolingana kuwezesha, nilipokea zangu pia tsh 5,464,000 baada ya kuchagua na kulipa ada tsh 98,999.Jiunge nao kupitia huu mchongo kisha tuma n
Ndio ni kweli, wacheki upate pesa ya christmas
 
Hili swali lilipaswa kuulizwa na mtoto wa drs la 7 aliyejiunga Facebook juzi.
Hivi duniani kuna shirika linalogawa pesa ?
Yaani watu wakae waandae shirika la kugawa pesa 😭😭😭😭
 
Nimepata hilo tangazo kwa mtu tunayefahamiana kabisa yeye ana sema amepata pesa ndio mana nimekuja kuuliza
Sasa huyo mtu mnayefahamiana aliingia kwenye mtego. Kuna links wanakutumia ukijiroga basi wanakuwa na uwezo wa kuendesha social medias zako zote mpaka whatasap zako.
Kwahiyo huyo aliyekutumia sio mtu unayemfahamu bali ni tapeli aliyefanikiwa kucontrol mawasiliano ya huyo mtu. Hakuna pesa za bure. Hata haya mashirika yanayotoa misaada kwa vijana huwa wanataka uandae proposal inayoeleweka kitu ambacho lazima utumie akili na muda.
 
Back
Top Bottom