Ni kweli kuna wakati kulikuwa na wachuna ngozi za binadamu nchi hii?

Ni kweli kuna wakati kulikuwa na wachuna ngozi za binadamu nchi hii?

Ilikua miaka gani ITV walikua wanafanya live coverage?
No sio live.yaani taarifa ya habari ilikuwa Haina kificho.
Leo hauwezi Kuna mtu akiwa kafa au kajinyonga,au kavunjika kiuno n.k
Lakini za zamani nilikuwa za kibabe sana.unaons live.siku hizi Kuna faragha za marehemu.
 
Miaka ya tisini nilikuwa nasikia sana stori za uchunaji ngozi maeneo mbalimbali ya nchi, stori zenyewe zilikuwa za kutisha sana kwamba watu wanamkamata mtu hasa watoto wadogo wanawachoma sindano fulani ngozi yote inaumuka kisha wanaichana na kuivua tu.

Hizi story za uvunaji ngozi ya binadamu zilikuwa ni matukio halisi ya ukweli au ni story za uzushi tu uliokuwa unavuma kutoka pande moja ya nchi kwenda nyingine(urban myth) ?
duh, kupitia stori humu unajua umri wa watu. ulikua bado unanyonya..
bwana mdogo those era were horrific. ustaarabu unakua kidogokidogo.
waswafa wakali wa hizo kazi.
uchawi janga Tanzania..
 
Hata kuandika jina la nabii wako mbora bila kumswalia ukaliandika kana kwamba ni Mohamad muuza mitumba pia umedhihirisha jina lako. Allah mtukufu akuongoze kwalo.
Iko hivi....
Hayo madhehebu aliyataja Mtume Muhammad Sala na salaam ziwe juu yake na ni kitu ambacho hakiepukiki ktk umma na kilichokuwa bora kwako ni kuitafuta haki na uifate..
Huo Sasa ndo USHIRIKINA WENYEWE unaleta.ni sharia ipi inayosema uhakika jina la Muhammad umtakie na rehma!?
 
Tena hayo matukio yalikuwa yanatokea sana mkoani Mbeya.
USHIRIKINA wako vizuri,wenye mabucha na watu wa madini walikuwa na Imani kuwa ukipata kipara au kiganja Cha mkono biashara zako zitaenda.
NGOZI walikuwa wanafanya biashara
 
Nadhani zilikuwa story tu, kuna kipindi tukiwa watoto tukaskia kuna watu wanateka wanaume na kukata Maumbile yao eti wanaenda kutegea samaki flqni hivi walikuwa na autajiri ukiwapata😂
Ilikuwa kweli
Kama hadi leo kuna watoto wanatekwa na kuuawa na kunyofolewa viungo kwa nini isiwezekane miaka ya tisini
 
  • Thanks
Reactions: I M
Ni kweli hii..

Miaka ile tukiwa wadogo tuliona video jamaa wamenaswa wamemchuna ngozi shangazi yao, na ngozi wameijaza kwenye ndoo. Aise ilitisha sana.

Miaka ya mbele kidogo, kukawa na wapiga nondo, hao ndo walikua balaa na nusu. Wakikukuta wanakuchapa nondo ya kisogoni, wanapiga kwa nguvu mpaka damu itoke haijalishi utasurvive au lah kikubwa damu itoke, ila sio rahisi kupona baada ya hapo.

Kuna bro alipigwa nondo, alikua hawezi kugeuka. Aliwekwa hogo shingoni.
 
Kuna Ile ya kupigwa nondo kichwani,
Wenye vipara ,na viganja vya mikono.
Haya mambo yalikuwwpo kweli.
Duh! Umenikumbusha mbali aisee.
Upigaji nondo kichwani ni UKWELI kabisa kwani jamaa yetu mmoja SUA alipigwa nondo. Ile mitaa ya kutoka Msamvu hadi mjini Masika ilikuwa mwisho kupita ni saa 12 jioni(1986 - 87). Ukijichanganya huvuki reli unalambwa nondo na kila ulichonacho hadi nguo na viatu vinaenda.
 
Back
Top Bottom