Ni kweli kwamba nisipoenda kuyasafisha makaburi ya wazazi na mababu nitapata laana au mikosi kwenye kazi zangu?

Restless Hustler

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2017
Posts
5,150
Reaction score
20,025
Habari za muda huu!

Kufuatia uzi wa tycoon wa fasihi ndugu ROBERT HERIEL alioeleza sababu za watu wengine kuishi umri mrefu na wengine umri mfupi, kuna nukta alieleza kwamba tunapaswa kuwaheshimu wazazi hata kama mameshakufa! Na akaeleza kwamba tutawaheshimu kwa kutembelea makazi yao( makaburini) na kusafisha kila mara.

Nimeona nichukue nukta hiyo na kuuanzishia uzi ili sote tujadili kwa upana zaidi ili kama ni kweli kuna umuhimu huo, wote tuujue.

Je, ni kweli kwamba tusipoenda kuyasafisha makaburi ya wazazi na mababu tutapata laana au mikosi kwenye kazi zetu ?!

Karibuni
 
Kama heshima ya utamaduni wenu na aliokufunza mama ni kufagia basi utafagia, Kama ni kuweka ya utaweka ya, na the like.

Ni ishu ya utamaduni.
 
Kusafisha makaburi hakuna uhusiano wowote wa kufanikiwa au kufeli katika maisha.

Na kama unaamini kuna uhusiano huku ukiwa ni mkristo,
Tayari ina maana biblia siyo kitabu cha Mungu na mafundisho yake ni batili.
 
Sawa mkuu. Naendelea kukusanya maoni
 
Tunayasafisha kama kuwaenzi wapendwa wetu, pale umelala mwili na sio nafsi au roho. Roho ipo kuzimu au paradiso kulingana na matendo ya mhusika. Ila shetani anao uwezo wa kuvaa roho ya muhusika na kuendelea kuwadanganya ndugu za marehemu ikiwemo hata kuwatokea live au kupitia ndoto. Mtoto akishakufa na kumbukumbu yake utolewa duniani. Mengine ni michezo ya shetani. Hakuna laana kutosafisha au kutambika makaburi, Ili laana, uchawi au mikosi yeyeto ikupate ni lazima wewe mwenyewe ndio uiruhusu iingie kwako.
 
Sawa mkuu. Naendelea kukusanya maoni

Mtu atakayesema kusafisha makaburi kunasaidia katika kufanikiwa maishani,
Basi inapaswa aukane ukristo wake au uislamu wake.

Kwa mujibu wa mafundisho yao, Mungu pekee ndiye msaada katika maisha.

Sasa akisema kusafisha makaburi kunasaidia maishani, tayari huyo mtu atakuwa amekubali "Mizimu" inasaidia katika maisha kama vile tu Mungu afanyavyo.

Mimi binafsi siamini katika yote hayo!
 
Kusafisha makaburi hakuna uhusiano wowote wa kufanikiwa au kufeli katika maisha.

Na kama unaamini kuna uhusiano huku ukiwa ni mkristo,
Tayari ina maana biblia siyo kitabu cha Mungu na mafundisho yake ni batili.

Mafunzo ya biblia na Quran utufundisha tuyakumbuke makaburi,kuyakumbuka ni pamoja na kuyafanyia usafi.
Kiimani inatulenga sisi tulio hai inasaidia kuondoa roho ya kiburi,majivuno,kujisahau,na kuona kwamba sisi ni wapitaji wa dunia, kwamba vyoote ni kuukimbiza tu upepo.
 
Naomba andiko moja la biblia linalosema
 
Back
Top Bottom