Generali aliyewahi kupigana vita akiwa Private,Na Generali ambaye toka akiwa Private hajawahi kushiriki vita yoyote hadi anakuwa Generali.Huwezi niambia hawa watu watakuwa sawa katika majukumu yao ya kivita....
Mbona mmekaririshwa vita,vita,vita kama ndiyo majukumu pekee ya kijeshi!
Jeshi ni 'mult purpose activities job' na kazi ama majukumu ya jeshi zimeainishwa wazi katika vitabu vya sheria za kijeshi (National defence act) zilizotungwa na bunge.
Majukumu ya mwanajeshi pa1 na vita ni kuzuia majanga, uokoaji, kujilinda, ulinzi wa mipaka, kutoa elimu ya ulinzi wa jamii, ujenzi, uhandisi nk nk, pia kufanya kazi yoyote ile itakayoamriwa na amiri jeshi mkuu.
Kazi zote hizo hutakiwa kufanywa na mwanajeshi kwa weledi na nidhamu isiyohojika.
Kazi yoyote inayofanywa na jeshi kwa weledi, iwe vita ama kazi yoyote iliyoamriwa na mkuu wa majeshi huchukuliwa kama ni ushindi.
Na uzembe wowote unaobainika katika utekelezaji wa majukumu hayo, uzito wa mashitaka na adhabu yake hufanana.
Kuhusu vyeo na maslahi ya jeshi havitolewi kama njugu. Magroup ya vyeo yapo kimpangilio wa kimuundo na kimataifa.
Corporal rank ya Marekani hauwezi kulinganisha na Liutenant rank ya Tz kwa kuwa kila cheo kinapata mafunzo ya kada ya uongozi wa cheo chake.
Ndiyo kusema, ukisema 'Corporal' inamaana ileile katika jeshi lolote kwamba cheo hicho kina hadhi ya balozi wa nyumba kumi na ukisema 'General' utakuwa unazungumzia ngazi ya waziri kwa muktadha wa vyeo vya kiraia.
Watu wasichanganye vyeo na maslahi kwa kuwa kila nchi hulipa askari wake kutokana na uchumi wake, lakini vyeo na madaraka ya kijeshi vinafanana kimataifa.