Kwahiyo mct ndio kipimo cha ubingwa? Wewe unajua nini kuhusu elimu? Ili ufanye undergraduate pale MUHAS si kwa vigezo vyenu mliweka uwe umamaliza kidato cha Sita katika tahasusi ya PCB, je kila nchi wanasoma mpaka form 6? Na wanasoma PCB? Sasa unakataa vip kuwa ubingwa wa mtu sio lazima upimwe na MCT kama interest ya mtu sio kutambuliwa?
Halafu kwanza tukusaidie kitu, kuna holders wengi wa taaluma ambao taaluma zao hawakuwa na shida ya kutambuliwa na mamlaka za sehemu husika walipo.
Mimi naweza kuwa Professor nchi husika nikija UDSM wakaishia kuniona mzalimili fulani tu, watanitaka nikawasilishe kazi zangu mbele ya jopo la wataalamu wao na mimi huo muda wa kwenda kuongea na kina Ruge sina na sihitaji kutambuliwa kama Professor na kina Anangisiye ambao hata lugha yenyewe wanaweza wasisikie ninachoongea.
Halafu umejihakikishia umeelewa maana ya Fellowship? Na nani anakupa sifa linganishi za utaalamu fulani? Hebu wasaidie wenzako hapo kwenye fellowship Janabi alitoka na kitu gani?