Ni kweli kwamba watumishi wasiopitishia mishahara yao benki ya CRDB hawana nafasi ya mikopo katika benki hiyo?

Lengo ni zuri kwao na la kibiashara la kupunguza default rate kwenye mikopo

Mabenki karibia yote hufanya hivyo ili ku control marejesho, pale ambapo makato yatachelewa au yatakuja tofauti basi wanatumia kama mfumo wa standing order, fedha ya mshahara inapoingia kwenye akaunti yako wanakata sawa sawa na marejesho yako na kupeleka kwenye skaunti ya mafejesho ya mkopo
 
Hapana CRDB mbona hawana sharti hilo... Sio lazima mshahara upitie kwao ndio ukope
Wameweka utaratibu wa mshahara kupitia kwanza kwenye akaunti yao ya CRDB ndipo mteja apate Loan. Ni fedheha na udikteta huo
 
Huo ni udikteta uchwara, sasa kila benk ikifanya hivyo hali itakuwaje? Bure kabisa
Mabenki yanakopesha, mdhamana wako ni nani au dhamana ni mali gani.
Hebu tupeni uzoefu kwenye banki zingine zinafanyaje kwa mtumishi ambae mshahara aupitii kwao.
 
Mabenki yanakopesha, mdhamana wako ni nani au dhamana ni mali gani.
Hebu tupeni uzoefu kwenye banki zingine zinafanyaje kwa mtumishi ambae mshahara aupitii kwao.
Kwa mabenk mengine ambayo mshahara haupitii kwao, hakuna mashart mapya bali ni utaratibu ule ule wa kudhaminiwa na mkurugenzi wako
 
Sio kweli
 
Wanalipa mkopo ni mwajiri wako kupitia mshahara wako.

Hivyo kama una deni Bank A makato /malipo yataenda Bank A.

Na mshahara wako utaenda Bank B.

Na haya yanafanyika wakati wa mata'arisho ya monthly salary
 
Nikweli kabisa ili upate mkopo ni lazima ufungue akaunt kwao...
 
Nimeenda kutaka kuchukua mkopo Wa milioni 10 kwa miaka 2 wakaniambia mkononi nitapata milioni 9 na laki 3+ nimeshangaa sana nikauliza mchanganuo ukoje jamaa akaniandikia hivi;
1. Gharama 184000
2. Insurance laki na 60+
3. CRDB 340785.077 sasa kwa ninyi wazoefu Wa huko Crdb hicho kipengele cha 3 ni nini hiyo? Mana nilinaribu kumuuliza jamaa akaniambia ndio calculation ilivyo kwa kiwango ninachotaka kuchukua. Msaada tafadhali! Mana nafanya mpango kesho niwacheki ili ni cancel huo mkopo Mana nahisi kuibiwa
 
Linawezekana mkuu watumishi wanakopa benk moja na mshahara unapitia benk nyingine. Marejesho ya mkopo yanakatwa automatically kutoka kwenye mshahara wako kwenda benk uliyokopa.
 
Hiyo kwa ujumla wanaita Processing Fee 😅 ni ujanja ujanja tu
 
Hili suala nimelisikia sehemu ndugu zangu wanajamii forum kwa mnaojua ukweli wa suala hili Basi mtujuze tusiojua vizuri.
Lakini watu wengine mna dharau sana! Yaani wakupe mkopo halafu uwe unawapelekea mrejesho kwa cash baada ya kutoa benki B? Wacha dharau bro! Sasa kwa nini usichukue mkopo huko huko unakopitishia mshahara wako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…