Ni kweli Lissu kakosa pesa za kuendesha uchaguzi wa kamati kuu ya chama?

Si mlikuwa mnasema Magufuli ajenge taasisi ili akiondoka mambo yasikwame?
Siyo one man show.
Mbowe amesifiwa kujenga taasisi Sasa taasisi gani inategemea mfuko wa mtu mmoja ambaye akiondoka taasisi ina anguka?
Kadiri mnavyo ongea Sana kuendeleza vita vya wakati wa uchaguzi mnazidi kumchafua Mbowe. Muachieni heshima kidogo aliyo nayo ibaki ilivyo, heshima ya uchaguzi huru na kukubali kushindwa ni kubwa mno usimuharibie na hiyo.
Nyie wapambe katafuteni kazi nyingine za kufanya. Yapo maisha mengine mazuri nje ya uongozi wa CHADEMA.
 
Hawezi kukosa pesa, jana tu alikuwa anakula bata (happy hrs) kushangilia ushindi wake.
 
Mtu tangu azaliwe hajauza hata sindano, atapata milioni 50? Tangu apewe lengo la kukisanya milioni 30 za mkutano mkuu, hakuleta hata mia
 
Kwanini usitoe hiyo hela baada ya kuja kuandika humu? Ukishajua utatoa au ni umbea tu umekujakuutafuta?
 
Mkuu hapa nazungumzia million 50 sio mabillion ya kampeni za uchaguzi mkuu. Unaendeshaje chama kama hauna financial muscles?

Aseme tumpe mipango ya kutafuta pesa.
Ulikuwa wapi kugombea uenyekiti.
 
Lisu hauzi unga, ni mwenyekiti wa cdm. Mkutano kama hakuna pesa huo ndio uhalisia. Ni wendawazimu kukaaa vikao vya kufadhiliwa na majizi ya ccm.
 
Bora chama kife kuliko kuwa na chama ambacho kilitegemea pesa za mtu flani mmoja ili kiwepo. Ni hatari kwa chama hicho kushika dola maana atakayekuwa ameshind sio chama au sera zake basi ni huyo mwenye hizo pesa na nchi ataifanya anavyotaka kwa kisingizio cha pesa zake.

kwa hiyo uchaguzi ule ulikuwa unafaida sana kitaifa katika kufanya mayengenzeno. Ni qfadhali kisiwepo kuliko kuwepo kwa mfumo ule.
 
Nadhani lissu pia after time haya mambo atayaweka sawa. Pia mbowe hatakiwi kukaa mbali mpaka ahakikishe aliyemuachia anafata tracks zake, thereafter, amuachie aende. Bila hvo, CHADEMA msahau hata kuikuna ccm au vyama vingine.
Kwa yale matusi? Aisee Mbowe atakua mpumbavu wa kiwango cha lami kuwasaidia hao wahuni…. Ni muda wa Lissu ku apply zile nadharia zake
 
Haya mambo acha kabisa,nimekumbuka mbali,niliwah kuachiwa kiwanda kidogo cha nafaka

Wakat sijakusanya pesa vzur,mashine moja ikaharibika na ilihitaji pesa ndefu kidogo kuirekebisha,hapo ndo nilipogundua haya mambo yanahitaj wenye pesa
Watu wamevimba matumbo Yao wanamtumkana Mbowe huku wamevaa Tshirt’s zake…. Ukumbi kalipa yeye na posho juu Lkn wakashindwa hata kumrudishia fadhila kwa kumbeshimu Leo honeymoon imeisha unatakiwa ugali mezani wanahaha
 
Hizi mbegu ni heri zingemwagwa chooni nzi wapate lishe aisee….
 
Ripoti ya Ukaguzi ya mkaguzi mkuu inaonyesha hakuna hilo tatizo

Kuwa kila pesa ilitumika vizuri

Lisu atoe pesa za hivyo vikao aache uswahili
Ukaguzi unaangalia pesa za akaunti rasmi ya chama sio pesa binafsi. Sasa kama Mbowe anapewa pesa na watu/taasisi/wadau kama mwenyekiti kwa akaunti yake binafsi je CAG anaruhusiwa kukagua?
 
Uongozi mpya alishakabidhiwa Lisu na mkutano mkuu na kuanza kabisa kazi ya kuteua wajumbe wa kamati kuu nk

Unataka akabidhiwe mara ngapi?
Uliona kuna vitabu vya bank amekabidhiwa pale? Acha upuuzi dogo
 
Uliona kuna vitabu vya bank amekabidhiwa pale? Acha upuuzi dogo
Katibu mkuu bado ni Mnyika.
Yeye ndie mtendaji mkuu wa chama
Mwenye mafaili sio Mbowe

Kila kitu vikiwemo.hivyo vitabu vya benki viko ofisini kwake sio nyumbani kwa Mbowe
Lisu akitaka amuone katibu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…