Ni kweli makampuni ya Australia yametuingiza chaka kuvuna Graphite na Niobium mikoa ya Lindi na Mbeya

Hivi unafahamu maana ya mkataba? Sijawahi ona nchi yeyote ambayo mkataba wa uwekezaji uko wazi kwa wananchi.

Tuna watu tumewapa kazi hizo na ni wataalamuu, tuwaamini kwa kazi hii
 
Hivi unafahamu maana ya mkataba? Sijawahi ona nchi yeyote ambayo mkataba wa uwekezaji uko wazi kwa wananchi.

Tuna watu tumewapa kazi hizo na ni wataalamuu, tuwaamini kwa kazi hii

HUo uliondika ni upuuzi unaotumiwa na wajanja kuhujumu nchi; kwanza sio sahihi kusema duniani kote mikataba ya uwekezaji haiwekwi wazi na hata kama hiyo ni Kweli hatuna ulazima wa kufuata mkumbo wa nchi nyingine!! Nilitegemea nchi kama yetu ambayo haina watendaji waaminifu [ angalia historia ya mikataba yaa Barrick Gold/ Acacia] ndio ingekuwa mbele katika kuweka mikataba yake wazi!!!

Kama wananchi [ SOVEREIGN ] ndio wanaotwishwa mzigo wa kulipa pale serikali inapotakiwa kuwalipa hao wawekezaji kutokana na kusaini mikataba mibovu , kwanini wasijue kile kilichomo kwenye hiyo mikataba kabla haijasainiwa? Usiri huo una justification gani and for whose interest?
 
Technology inabadilika kwa kasi sana hizo rare minerals zinaweza kuwa outdated very soon.
Hatuna pesa na technology hatuna options zetu ni very limited
 
Niwekee hapa mkataba wowote duniani kati ya mwekezaji na nchi husika ambao uko wazi kwa wananchi wote ndipo niamini kuwa mimi ni mpuuzi. Hivi unajuwa kwa nini parties wana saini NON DISCLOSURE AGREEMENTS (NDAs).

Kuna general terms wananchi wanaweza wakajua lakini unapokwenda kwenye specifics kama trade secrets, loyalties and patents lazimanutazuiwa na NDAs.
 
Technology inabadilika kwa kasi sana hizo rare minerals zinaweza kuwa outdated very soon.
Hatuna pesa na technology hatuna options zetu ni very limited
Duuh! Hii kali ya karne!
 
Kuna sababu gani za msingi apart from being standard practice ya kudaini NDAs?
 
Niobium imetoka wapi hapo mlima panda, historia inasema wazungu waliokuwa wanachimba dhahabu hapo, Kawawa akawafukuza wakiwa na tani kadhaa za dhahabu, wakazizamisha ardhini tukose wote, serikali ikajua kuna siku watarudi kuyabeba, wakaweka kambi ya magereza hapo. Leo dhahabu imegeuka niobium?
 
Hatuna utamaduni wa kuwekeza Tu waoga Sana itachukua miaka mingi kupata wawekezaji
Tunapenda kuwekeza miradi ya uwoga kuporomosha majumba.
Bora yachimbwe Tu Kwanza tunalilia ajira tunasomesha Kwa ajili ya ajira.
Suala la watanzania kuwekeza bado sana
 
Naamini nitapata mawili matatu kwenye hili. Hivi hiyo 16% base ni nini?
 
Naamini nitapata mawili matatu kwenye hili. Hivi hiyo 16% base ni nini?
Base kwakeli sijui ni kitu gani, ila kwa mikataba tunayoongelea Tanzania ina 16% non diluted shares. Maana yake ni kwamba thamani zake aiwezi shuka iwapo huko mbele, new shares are issued in the capital market in future, which might dilutes the values of existing shares.
 
Huu ujinga ulisomea wapi au nani alikusimulia?

Dhahabu kuzamishwa chini!

Kwa nini usiulize kwa wajuzi badala ya kujitangazia ujinga!
 
Naamini nitapata mawili matatu kwenye hili. Hivi hiyo 16% base ni nini?
Ni hisa za uwekezaji mtaji. Hisa hizi hazitapanda wala kushuka kwa mwenendo wa soko la mitaji.
 
Madini ya kutengenezea Penseli hayana ughali wowote.
 
Hii hapa nilienda hombolo na wachina

Kwenye lithium .....

Wabongo sahv wanachotakiwa kufanya wayakamate maeneo yenye
Madini mfano graphite, nickel, lithium nk....wawe na makaratasi yote
Sasa wao wakae mkao wa kula tu kutoka kwa hao wageni
Ila tukikaa kulialia tu bila kuchukua hatua kila siku tutakuwa watu wa kulalamika

Ova
 
Madini ya kutengenezea Penseli hayana ughali wowote.
Watu wakishasikia madini tu basi ni mabilionsss [emoji1]
Hii imenikumbusha kisa kimoja kilitutokea morogoro,dc --- alikuja na team +wazee walikamata ruby corrhndumn,ilikuwa tanis 1 na nusu
Basi dc,na watu wake wakajuwa ule mzigo ulikuwa mabilion ,oh sijui tunawaibia+serikali
Tukawambia soko la ndani tunauza haya madini kg 1 ni 3000/
India huko bei ni $4
Tulivutana sana,mpk RMO moro alingilia kati wanasasiasa wakaambuka

Hata leo hii ukiambiwa bei ya gypsum
Utashanga....sema ili uione faida yake
Unatakiwa uchimba tons na tons

Na hapo mtaji+uwekezaji wake lZima uwe mkubwa

Ova
 
Roho zilitaka kuwatoka😂😂
 
Madini ya kutengenezea Penseli hayana ughali wowote.
Graphite is used in pencils, lubricants, crucibles, foundry facings, polishes, arc lamps, batteries, brushes for electric motors, and cores of nuclear reactors.
 
Graphite is used in pencils, lubricants, crucibles, foundry facings, polishes, arc lamps, batteries, brushes for electric motors, and cores of nuclear reactors.
Ni madini yaliyojaa bwelele kila Nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…