Ni kweli makampuni ya Australia yametuingiza chaka kuvuna Graphite na Niobium mikoa ya Lindi na Mbeya

Ni kweli makampuni ya Australia yametuingiza chaka kuvuna Graphite na Niobium mikoa ya Lindi na Mbeya

Makosa yaleyale yanaendelea kufanywa na wanasiasa wetu ambayo yatalipwa na vizazi vijavyo huku wao na familia zao wakineemeka katikati ya lindi la umasikini wa walio wengi. Hatuna wataalamu wa kutosha badala tupambane kusomesha vijana waje kusaidia taifa kwenye nyanja husika tumekalia kupiga siasa na ngonjera zisizoisha
 
View attachment 2602708
Kwamba sisi tuaambulia $ 600+ milioni wakati wao watavuna mabilioni ya dollars kila mwaka.

Madini ya graphite yanapatikana kwa wingi huko Lindi wakati niobium ipo tele pale Panda Hill Mbeya. Kwa nini tusingesubiri nchi ipate uwezo tuweze kuchimba wenyewe badala ya kuwapa hawa wa Australia kwa bei ya kutupa?

Prof. Kabudi na Prof. Mruma kweli hamkuona mtego huu Wa- Australia hawa hakituingiza chaka!

Tafadhali tunaomba ufafanuzi!
Shida inaanzia kwako, huna taarifa sahihi na kamili juu ya suala la mkataba husika, si kila mkataba unakuwa fully exposed to the general public, kuna some common areas zinakuwa exposed na zinatumika kama ni "mileage aspect" kwa wanasiasa kukaliana kooni kwenye rasilimali za taifa kwa maana ya ulaji, kwa hivyo hizo some exposed areas, hutumika pia kama ni "weakness hole" by the opponent, so hapa utapokea ushauri wa kipinzani zaidi kutokana na namna nilivyoeleza.
 
Utafiti ulikwisha fanywa kabla hujazaliwa kilichokuwa kinasubiriwa ni kuanza uchimbaji tu!
Wacha kujidanganya na assumptions za uwongo. Eti kwa vile gereza la Songwe lilikuwa pale inamaanisha Nyerere alikuwa anahifadhi madini?

Kwa Songwe hapana, sema haya madini ni gemstones kama zongine tu ila matumizi yake zamani hayakuwako kama hiyo ya ku preserve joto kwenye ndege, smart phone na batteries.

Kisayansi mawe yote yana majina kama yalivyo majani au wanyama.

Kwa hiyo hata kama Nyerere angekuwa na uwezo wa kuchimba lakini asingejuwa ayatumie vipi
 
Shida inaanzia kwako, huna taarifa sahihi na kamili juu ya suala la mkataba husika, si kila mkataba unakuwa fully exposed to the general public, kuna some common areas zinakuwa exposed na zinatumika kama ni "mileage aspect" kwa wanasiasa kukaliana kooni kwenye rasilimali za taifa kwa maana ya ulaji, kwa hivyo hizo some exposed areas, hutumika pia kama ni "weakness hole" by the opponent, so hapa utapokea ushauri wa kipinzani zaidi kutokana na namna nilivyoeleza.
Sasa wewe ndiyo shida mwenyewe kwa kujifanya unafahamu siri za serikali wakati ni kapuku tu unasubiri sadaka!
 
Wacha kujidanganya na assumptions za uwongo. Eti kwa vile gereza la Songwe lilikuwa pale inamaanisha Nyerere alikuwa anahifadhi madini?

Kwa Songwe hapana, sema haya madini ni gemstones kama zongine tu ila matumizi yake zamani hayakuwako kama hiyo ya ku preserve joto kwenye ndege, smart phone na batteries.

Kisayansi mawe yote yana majina kama yalivyo majani au wanyama.

Kwa hiyo hata kama Nyerere angekuwa na uwezo wa kuchimba lakini asingejuwa ayatumie vipi
Acha kuonyesha ujinga wako hadharani! Kama wewe ulikuwa hujui jiite mjinga lakini wajuzi wanafahamu matumizi yake tangu kitambo!
 
Usokwe ni pale tunapofikiri kuwa Yepi Merkezi ni Shirika la Umma la Tanzania.

Watanzania ni Masokwe yaliyochangamka kidogo.
Mkuu GT usiangake sana na wabongo. Wee tulia kwako kwenye swimming pool yako na kisima chako kinachobubujika maji na usiache kuwasaidia wanaokuzunguka maji.
 
Kwani lazima tuchimbe sasa?

Ndiyo. Kizazi cha mbele hakina thamani zaidi yetu hata sisi tuna haki ya kula mema ya nchi. Mambo ya kusubiri sijui kina nani waje kufaidi as though sisi ndo hatupaswi kufaidi kwani tumezaliwa kuteseka. Tunakula sasa na wao watakula watachokikuta.
 
Unasikitisha

🤣 🤣

Ukweli lazima usemwe. Huwezi wekeza less afu ule sawa na mtu aliyewekeza zaidi. Haiwezekani.

Nyie mmeweka nini hadi mpate zaidi?

Mnataka shingapi ili mseme hamjaonewa? Unaweza pewa 50% na usipate hata hiyo 600M USD.

Kuleni 16% hiyo mtulie.
 
Haahah

Wakati maeneo ya graphite yapo mengi tu kama wanataka na wao waingie kuchimba

Ova

Exactly, wachimbe na wao kama wanadhani ni rahisi rahisi tu.

Ardhi yote ya bongo ina madini wachimbe wapate hiyo 100% wanayotaka wawekeze kila kitu wenyewe from exploration, running costs, equipment, workforce, etc.

Migodi ya makaa ya mawe tu imewashinda. Leganga na mchuchuma inahitaji 3B TSH tu kufanya uzalishaji wenye tija umewashinda afu leo wanajidai kutaka kurun mgodi ambao hata hawana maabara nchini ya kupima sample zake.
 
Hakuna kitu kama hicho.. 99% ya madini yote yamesha gunduliwa..
Na Mimi nakazia Hakuna kitu kama hicho !! Hata dhahabu wanaume wa shoka walikubali Serikali iwe inapata asilimia 3 na wenye mgodi wachukue 97% kama sikosei kipindi kileeee !!
 
Umeliweka vizuri. Watu wananangalia faida tu ila wanasahau gharama za utafiti na uchimbaji

Tunawauliza ni taasisi gani ya serikali inajiendesha kwa faida hawana jibu.

Leganga na Mchuchuma inayotaka 3B TSH tu kujiendesha kwa faida imewashinda, leo wanajikuta experts wa madini ambayo hawana hata maabara nchini ya kuyapima. Mtu awekeze kila kitu afu ule nae sawa utakua na wazimu kuomba huo usawa.

Unaweza pewa hisa 50% na usipate hata hiyo 600M USD kama your input doesn't match the input ya mwenzako.
 
Acha kuonyesha ujinga wako hadharani! Kama wewe ulikuwa hujui jiite mjinga lakini wajuzi wanafahamu matumizi yake tangu kitambo!
Weka ushahidi, kinyume chake utakuwa ni bingwa wa matusi. JF ni mahali ambapo kama unajuwa unaweka hoja na siyo kuweka sweeping statements za kudharau na kutukana
 
Ningemuhusisha mwamba freedom fighter Freeman Aikael Mbowe na mambo yote yangeenda sawa.
Mbowe elimu yake mwisho FVI pale Ihungo Secondary. Experience yake ni clerk BOT na owner wa Bilicanas club. Otherwise ni mtaalamu wa siasa. Atakusaidiaje huyu kwenye mikataba. Labda unimabie Tundu Lissu
 
View attachment 2602708
Kwamba sisi tuaambulia $ 600+ milioni wakati wao watavuna mabilioni ya dollars kila mwaka.

Madini ya graphite yanapatikana kwa wingi huko Lindi wakati niobium ipo tele pale Panda Hill Mbeya. Kwa nini tusingesubiri nchi ipate uwezo tuweze kuchimba wenyewe badala ya kuwapa hawa wa Australia kwa bei ya kutupa?

Prof. Kabudi na Prof. Mruma kweli hamkuona mtego huu Wa- Australia hawa hakituingiza chaka!

Tafadhali tunaomba ufafanuzi!

Unajua vitu vingine ni kumwachia Mwenye Enzi Mungu adeal navyo maana vinatia kichefuchefu
Mola smaweza yote na makosa siyo ya wazungu bali ni utawala
Eeh Mwenye Enzi Mungu
Tuhurumie sisi watanzania walahi
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Tunawauliza ni taasisi gani ya serikali inajiendesha kwa faida hawana jibu.

Leganga na Mchuchuma inayotaka 3B TSH tu kujiendesha kwa faida imewashinda, leo wanajikuta experts wa madini ambayo hawana hata maabara nchini ya kuyapima. Mtu awekeze kila kitu afu ule nae sawa utakua na wazimu kuomba huo usawa.

Unaweza pewa hisa 50% na usipate hata hiyo 600M USD kama your input doesn't match the input ya mwenzako.
Wapumbavu wanadhani uwekezaji wa madini sawa na kufungua saloon ya nywele au grocery.
 
Weka ushahidi, kinyume chake utakuwa ni bingwa wa matusi. JF ni mahali ambapo kama unajuwa unaweka hoja na siyo kuweka sweeping statements za kudharau na kutukana
Kwani kuna data au ushahidi wo wote wewe umeweka? Halafu nimeona mahali umepotosha kuwa niobium na graphite ni gemstones huo ni uongo. Fanya assignment yako vizuri hizo ni metals!
 
6A29E49F-AEEF-4E34-A892-3806DD40399D.jpeg

☝️Hizo ndio income projection za mradi mmoja tu watu wamewekeza $321m halafu unasifia shares za 16% hiyo hela yao si inarudi ndani ya miaka miwili au mitatu tu.

Huko ni kugawa mali za nchi sio uwekezaji wenye tija.
 
Back
Top Bottom