The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,282
- 117,244
- Thread starter
- #21
Uanzishwaji wa TRA mchakato ulianza kipindi cha Raisi Mwinyi kama moja ya masharti ya Structural Adjustment Policy ambayo serikali ya Tanzania ilishauriwa na The Breton Woods Institutions (IMF & WB) kwamba kuwe na chombo kimoja kilichoanzishwa kisheria, na huru (Autonomous) ambacho kitakuwa na jukumu la kusimamia ukusanywaji wa mapata yote nchini.
Mambo mengi ya kuzifanya taasisi zilikuwepo kipindi cha Raisi Mwinyi kuwa ni za kisasa ili kuendana na mabadiliko ya soko huria yalifanywa chini ya Mzee Mkapa: Vyombo vingi vilikuwepo japo aidha vilikuwa chini ya Wizara fulani na siyo huru kama ilivyo leo. Japo lazima tukubali kwamba Mzee Mkapa ana sehemu yake kusukuma hili kufanyika ili aweze kuendana na mahitaji ya Uchumi wa soko huria ambao yeye aliauamini sana.
Ukiangalia vizuri kipindi hiki ndiyo yalifanyika mabadiliko makubwa sana kwenye sheria za nchi ambayo yalibadilisha muundo wa taasisi mbalimbali za kitaifa na kuzipanga upya. Sheria nyingi sana zilikuwa Revised na taasisi nyingi zikawekwa kisheria.
Role ya Kikwete ilikuwaje kama waziri wa Fedha chini ya Mwinyi?
Manake amewahi kunukuliwa pia kuhusika na uundwaji wa TRA