Ni kweli Mkapa alianzisha TRA?

Ni kweli Mkapa alianzisha TRA?

Uanzishwaji wa TRA mchakato ulianza kipindi cha Raisi Mwinyi kama moja ya masharti ya Structural Adjustment Policy ambayo serikali ya Tanzania ilishauriwa na The Breton Woods Institutions (IMF & WB) kwamba kuwe na chombo kimoja kilichoanzishwa kisheria, na huru (Autonomous) ambacho kitakuwa na jukumu la kusimamia ukusanywaji wa mapata yote nchini.

Mambo mengi ya kuzifanya taasisi zilikuwepo kipindi cha Raisi Mwinyi kuwa ni za kisasa ili kuendana na mabadiliko ya soko huria yalifanywa chini ya Mzee Mkapa: Vyombo vingi vilikuwepo japo aidha vilikuwa chini ya Wizara fulani na siyo huru kama ilivyo leo. Japo lazima tukubali kwamba Mzee Mkapa ana sehemu yake kusukuma hili kufanyika ili aweze kuendana na mahitaji ya Uchumi wa soko huria ambao yeye aliauamini sana.

Ukiangalia vizuri kipindi hiki ndiyo yalifanyika mabadiliko makubwa sana kwenye sheria za nchi ambayo yalibadilisha muundo wa taasisi mbalimbali za kitaifa na kuzipanga upya. Sheria nyingi sana zilikuwa Revised na taasisi nyingi zikawekwa kisheria.

Role ya Kikwete ilikuwaje kama waziri wa Fedha chini ya Mwinyi?
Manake amewahi kunukuliwa pia kuhusika na uundwaji wa TRA
 
Since Mtei aliwahi kuwa waziri wa fedha
Possibility ni kuwa wazo lake kama kweli lake
Lilikuwepo Tu hapo wizarani likifanyiwa kazi na
Review miaka kibao..na ndo maana naona sio Sahihi kusema Mkapa alianzisha TRA

Kulingana na Kitabu chake alivyojiuzulu Ugavana akaenda WB/IMF mojawapo kati ya hizo mbili na huko ndipo alipokuwa mshauri wa Serikali yetu kwenye reforms na TRA ikiwa ni mojawapo, nilikisoma muda mrefu hivyo sikumbuki vizuri kila kitu lkn alielezea kwenye hicho kitabu uuwandwaji wa TRA, ...
 
Role ya Kikwete ilikuwaje kama waziri wa Fedha chini ya Mwinyi?
Manake amewahi kunukuliwa pia kuhusika na uundwaji wa TRA
Sheria hii ilipitishwa mwaka 1995 kipindi cha utawala wa Mzee Mwinyi. Sheria zote kabla ya kupelekwa bungeni huanzia Wizara husika ambao wao hufanya jitihada za kuwatafuta wadau mbalimbali wa ndani au nje ya nchi ili waweze kutengeneza rasimu ya muswada ambao utaenda kusomwa mara ya kwanza kabisa bungeni. Katika hili watu wa Wizara hupewa hata ruhusa ya kwenda kufanya Benchmark kutoka nchi jirani ambayo imefanikiwa kwenye hili.

Jakaya kama Waziri ndiye aliyesaidia kufanya haya hadi tukapata sheria mwaka 1995, lakini Mzee Mkapa alihakikisha taasisi inaanza kufanya kazi mwaka 1996 kwa kuifanya taasisi isiwepo tu kwenye makaratasi kama mashirika mengi ya serikali yalivyo. Hivyo nadhani kusema Mzee Mkapa ndiyo anatakiwa kupewa pongezi peke yake nakataa kabisa maana hili jambo lilikuwepo serikalini muda sana likishughulikiwa.
 
Shukran sana..
 
Website ya TRA
20200726_211409.jpg

Sheria ilitungwa enzi za mwinyi
Operation ilianza enzi za Mkapa
 
Since Mtei aliwahi kuwa waziri wa fedha
Possibility ni kuwa wazo lake kama kweli lake
Lilikuwepo Tu hapo wizarani likifanyiwa kazi na
Review miaka kibao..na ndo maana naona sio Sahihi kusema Mkapa alianzisha TRA
Hivi kwa mfano hii Stiglers gorge ikikamilika credits zinaenda kwa nani? Mwalimu, Ruksa, BWM, JK ama JPM? Mimi kwa mawazo yangu ni JPM....hata kuhamia Dodoma, clearly credits zaidi zinaenda kwa JPM, sivyo?
 
The Tanzania Revenue Authority (TRA) was established by Act of Parliament No. 11 of 1995, and started its operations on 1st July 1996. In carrying out its statutory functions, TRA is regulated by law, and is responsible for administering impartially various taxes of the Central Government.
 
TRA ilianzishwa na Mzee Mwinyi mwezi August mwaka 1995 kabla Mkapa hajawa rais.

Mkapa alichaguliwa mwezi November mwaka huo kuwa rais wa awamu ya tatu.

TRA ilianzishwa kisheria na Mzee Mwinyi, Mkapa hakuunda TRA, ila ndiye wa kwanza kutumia chombo hicho kilichoundwa na mwenzie kukusanya mapato.

Mkapa kafanya mengi sana mazuri kwa nchi hii lakini hakuunda TRA

Hapa Chini ni muhtasari wa lini TRA iliundwa (Angalia tarehe kwenye rangi nyekundu)
IMG_20200726_0001.jpeg
 
Hivi kwa mfano hii Stiglers gorge ikikamilika credits zinaenda kwa nani? Mwalimu, Ruksa, BWM, JK ama JPM? Mimi kwa mawazo yangu ni JPM....hata kuhamia Dodoma, clearly credits zaidi zinaenda kwa JPM, sivyo?

Shida sio credits
Ni namna ya kuandika ukweli.
Tutasema JPM alianzisha stiglers gorge?
Au alikamilisha?..

Sidhani sahihi kusema Mkapa alianzisha TRA
Labda tuseme Mkapa alikamilisha uanzishwaji wa TRA..
 
Mkapa kajenga uwanja wa Taifa,kaanzisha TRA,bima ya Afya kwa watumishi NHIF,watumishi kulipwa salary kupitia Benki,Tasaf,mpango wa elimu uitwao MMEM shule zilijengwa vizuri na vitabu.
 
Shida sio credits
Ni namna ya kuandika ukweli.
Tutasema JPM alianzisha stiglers gorge?
Au alikamilisha?..

Sidhani sahihi kusema Mkapa alianzisha TRA
Labda tuseme Mkapa alikamilisha uanzishwaji wa TRA..
Factually tuseme hivi:
1. Wazo na sheria ya kuunda TRA lilipitishwa chini ya Rais Mwinyi (kutunga sheria)
2. Kuunda TRA na kuanza kufanya kazi kulifanywa chini ya Rais Mkapa (kutekeleza sheria)

Tukiazima mfano wa fani ya ujenzi, tunaweza kusema Mwinyi alichora ramani ya jengo, lakini jengo lenyewe aliyelijenga ni Mkapa. Unaweza kuchora ramani nzuri, lakini itabakia kwenye karatasi mpaka atokee mtu wa kuweka pamoja matofali na mortar.

Btw, pengine shida pia ipo kwenye lugha tu...."kuunda" maana yake nini? Kwa mfano wangu huo wa ujenzi, kuweka pamoja matofali, mchanga, cement, mbao, si ndio kuunda?

Fair?
 
Ni vizuri kukawepo na ukweli zinapoandikwa historia za Viongozi wetu na historia ya nchi yetu Kwa ujumla..

Nimesikia mara kadhaa watu wakisema Rais Magufuli kajenga daraja la Kigambon na nabaki na maswali mengi..

Sasa hili la Mkapa kuunda TRA pia linanitatiza sana ..kivipi?

Nimemsikia mara kadhaa Rais mstaafu Kikwete akisema aliunda TRA alipokuwa waziri wa fedha wakati Rais ni Mwinyi..
Na alisema alienda Uganda nafikiri kupata uzoefu wao WA URA..na wapo waliokuwa wanamshauri vinginenevyo..

Ifahamike wakati Rais Mwinyi anamteua Kikwete kuwa waziri wa Fedha hata uchaguzi wa ndani wa CCM wa mgombea ulikuwa bado na hakuna aliekuwa anajua kama Mkapa au anyone atakuja kuwa Rais wa Tanzania miezi michache baadae...

Binafsi nafikiri kuna 'watu wanaostahili' credit za kuunda TRA lakini hawatajwi..
Hata Kikwete probably alikuta 'process' IPO tayari akafanya kuiongeza nguvu..
Na Mkapa alipokuwa Rais miezi michache later 'ikawa rasmi'...

Kusema Mkapa aliunda TRA sio sawa..
Na hata Kusema Kikwete aliunda TRA pia sio Sahihi..labda tuseme Mwinyi? Au
'wataaalam wetu wa wizara ya Fedha'
Ambao hawatajwi na kuacha wanasiasa kubeba credits ambazo sio zao?..

Ni Sawa na kusema Mkapa alianzisha DSE
Au UTT wakati nimewahi msikia Mtaalam mbobezi na first CEO wa DSE na first CEO wa UTT akisema alikuwa anaenda waeleza
Viongozi kuhusu UTT hawaelewi kitu..wanamshangaa..hata DSE walikuwa wanasema nchi bado haipo tayari...

Sijui Yuko wapi Hamis Kibola Leo hii na kama kuna mtu hata anamtaja kama
'The brain behind DSE na UTT....

Swali linabaki pale pale je Mkapa ndo aliunda TRA?
Sometimes history huwa hazina ukweli aslimia 100% hivyo sishangai kwa wanaosema hivyo hata sasa wapo watu wanasema Magufuli ameanzisha Mahakama ya mafisadi

Je ni sahihi kusema hivyo?
Ama mahakama ya mafisadi ni division katika mahakama kuu
 
Factually tuseme hivi:
1. Wazo na sheria ya kuunda TRA lilipitishwa chini ya Rais Mwinyi (kutunga sheria)
2. Kuunda TRA na kuanza kufanya kazi kulifanywa chini ya Rais Mkapa (kutekeleza sheria)

Fair?

TRA ilishaundwa kisheria na Mzee Mwinyi,

Mkapa alitekeleza sheria tu iliyokwishaweka mifumo yote ya TRA iweje.

Kwa kweli siyo sahihi kumpa Mkapa credit za kuunda TRA

Mkapa ana credits za Mifumo kama vile, NHIF, TACAIDS, TANROADS, TVT (Siku hizi TBC1), Uwanja wa Mpira wa Taifa, Kuvuta Maji kutoka mwanza hadi Shinyanga, TASAF, PSRP, TCU, LOANSBOARD, REPOA na mengine mengi mazuri

Hayo ndo aliyaanzisha yeye, kwa michakato aliyoifanya yeye akiwa Kiongozi, Lakini siyo TRA, TRA alikuta ishaundwa kisheria tayari na mzee Mwinyi, yeye alitekeleza tu sheria.
 
TRA, URA na KRA yote yalianzishwa pamoja 1995 kwa msaada toka Benki ya dunia, ikiwa ni fedha ya msaada toka kwa mabeberu.
Kwahio Credit should go to Mabeberu ?

Nadhani hapa cha maana ni kuona nani alikuwa mtekelezaji.., ukifuatilia hii mifumo yote ni copy and paste from somewhere, VAT, Revenue, mfumo wa serikali, governing bodies n.k. , very little is new under the Sun..., and visionaries siku hizi hawapo tena
 
Mkuu nadhani hua wanapewa credit wanasiasa kuondoa mlolongo mrefu wa walioshiriki kitu kufanyika au kutokea. We mwenyewe unaona ulivozunguka sana kumpata muanzilishi wa TRA. Ila pia kwa nchi zetu ni utashi wa kisiasa ndo hupelekea vingi kuwezekana
 
Mkuu nadhani hua wanapewa credit wanasiasa kuondoa mlolongo mrefu wa walioshiriki kitu kufanyika au kutokea. We mwenyewe unaona ulivozunguka sana kumpata muanzilishi wa TRA.
Yeah ni kwel hata neno serikali ukilichanganua ni pana lakin kunyoosha maelezo huwa wengine wanasema serikali ya Magufuli lakini japokuwa haipaswi kuwa hivyo
 
TRA ilishaundwa kisheria na Mzee Mwinyi,

Mkapa alitekeleza sheria tu iliyokwishaweka mifumo yote ya TRA iweje.

Kwa kweli siyo sahihi kumpa Mkapa credit za kuunda TRA

Mkapa ana credits za Mifumo kama vile, NHIF, TACAIDS, TANROADS, TVT (Siku hizi TBC1), Uwanja wa Mpira wa Taifa, Kuvuta Maji kutoka mwanza hadi Shinyanga, TASAF, PSRP, TCU, LOANSBOARD, REPOA na mengine mengi mazuri

Hayo ndo aliyaanzisha yeye, kwa michakato aliyoifanya yeye akiwa Kiongozi, Lakini siyo TRA, TRA alikuta ishaundwa kisheria tayari na mzee Mwinyi, yeye alitekeleza tu sheria.
Kuunda, kuanzisha, ....nafikiri tunachanganya hapo. Sheria peke yake haifanyi kitu au jambo litokee....ni mpaka mtu atende. Kuunda TRA maana yake nini? Kwangu mimi ni kule kuteua Bodi ya TRA pamoja na Commissioner General kama sheria inavyotaka. Haya mawili alifanya Mkapa, sio Mwinyi. Angeweza kuacha kufanya, kama ambavyo Mamlaka kadhaa ambazo zimetungiwa sheria lakini bado hazijaundwa mpaka leo....nimetoa mfano wa Mamlaka ya kushughulikia Madawa ya Kulevya.....again, "imeundwa" chini ya Rais Magufuli ingawa sheria yake ilipitishwa chini ya JK.

Hata kama Mkapa hakuanzisha/hakuunda TRA (kwa kuwa ni ukweli hakuwa muasisi wa wazo la TRA, tunaambiwa ni proposal ya IMF), lakini bila shaka tunaweza kukubaliana kuwa alikuwa na mchango mkubwa sana katika mafanikio ya TRA hasa kwa hatua za awali. Maana TRA ilianza operations wakati wa utawala wake.
 
Back
Top Bottom