DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Hapana U=UKwa maana hiyo U=U
Vipimo vinasoma hajaathirika au
ni kiasi cha Virusi kuwa chini sana kwenye Damu tunaita TND..
Hiyo Haifanyi Virusi visionekane kwenye Antibodies Test au Visiwepo mwilini..
Bado ataendelea Kuwa na HIV ila uwezo wa kusambaza Virusi huwa ni mdogo sana..
Kwanini mnaogopa watu ambao tayari wapo kwenye dawa?
Me ningeshauri watu waogope zaidi mtu yule ambaye Kipimo kinasoma Negative..
kwanini?
Mtu anapokuwa kwenye Window Period Virusi huzaliana sana na ndo kipindi ambacho Muathirika anakuwa na Peak kubwa ya Virusi kuliko wakati wowote ule maana kipindi hicho bado antibodies hazijaanza kufanya kazi ya kupambana na Virus...
Hakuna kipind Muathirika huwa Contagious Wa HIV kama kipindi cha window Period..