Ni kweli mtu akitumia dawa ya UKIMWI hawezi kumuambukiza mwenzake hata bila kutumia kinga?

Ni kweli mtu akitumia dawa ya UKIMWI hawezi kumuambukiza mwenzake hata bila kutumia kinga?

Hii ni comment #123 sijaona aliyesema anao

watu wanazungusha tu maneno eti ooh huo ni kama malaria sijui kifua

Weeh[emoji117]weeh[emoji117]weeh[emoji117] (kwa sauti ya embarambamba)

Hiyo kitu ni deadly!

Tuache kuremba maneno hapa
 
Kuna level ya viral load (idadi ya virusi vya HIV kwenye damu) ikifikia kuwa undetected (kutoonekana kwenye damu) inakuwa huwezi kumuambukiza mwenza wako hata mkijamiiana bila ya kinga.

Ila inataka ujasiri wa hali ya juu. Yani nikijua una ngoma sidhani hata kama mnara utasoma achilia mbali kupiga kavu.

Kama ni kweli jamaa anakula mzigo kavu basi mwamba jasiri hasa.
Na yeye anatumia dawa ya kumlinda asiambukizwe
 
100% Ni kweli..
Na watu wengi sana wanaishi ni Serodiscordant..
Sisemi Kwa ushabiki bali nimeshuhudia sana..
Watu wengi ambao mara Nyingi tunaruhusu mahusiano hayo ni wale waliopima HVL na mara nyingi Huwa Zinasoma TND..("Target Not Detected")

Huyu ana Percent chini ya 0.01 ya kumuambika mwingine na hata wakinamama wakifika Hapa huwa wanaruhusiwa kuwa na watoto yaani kuchukua mimba na kuzaa..
Watu hawajiulizi kwanini Serostatus (Maambukizi) ya Watu hayaongezeki na yanazidi kupungua?

Kwanini siku hizi Idadi ya watoto Wadogo wenye maambukizi imepungua Sana tofauti na Zamani..

Jibu Ni moja Tu kuwa inawezekana na mifano ninayo na nimeiona si chini ya couple 100 zikiishi hivyo na kwa furaha

Kama kuna mtu mwenye swali namkaribisha maana hii ni moja ya Sehemu zangu za kujidai
Hii elimu inahitajika sana vinginevyo maambukizi hayatakwisha
 
Me ningeshauri watu waogope zaidi mtu yule ambaye Kipimo kinasoma Negative..

kwanini?
Mtu anapokuwa kwenye Window Period Virusi huzaliana sana na ndo kipindi ambacho Muathirika anakuwa na Peak kubwa ya Virusi kuliko wakati wowote ule maana kipindi hicho bado antibodies hazijaanza kufanya kazi ya kupambana na Virus...
Hakuna kipind Muathirika huwa Contagious Wa HIV kama kipindi cha window Period..
Kwa ile kupima mara 3 kila baada ya mwezi mmoja inaweza kuwa siyo indicator ya mtu kuwa salama?
 
So still jamii haiko salama,
USalama upo Ila hautakiwi kujiona salama kuliko mwingine ikiwa bado unaishi..

Kwa mfano kwenye IPC (Infection Prevention and Control) sasa kwenye rule za Standard precaution Huwa tunajielimisha kila siku Kuwa..
Rule number one ni Consider everyone susceptible to infection and Contagious...
hiyo haijalishi hata mke wako unatakiwa utake precaution...Na ndo maana ukija Hospitali hata kama nakujua Nitavaa Gloves..


Ukiishi kwa kufuata Roles na Miiko nakuhakikishia magonjwa utakuwa unayasikia tu..
 
HIi sijaelewa Kila baada ya mwezi mmoja unapimaje mara Tatu?

Yaani kila wiki Unapima?
Kupima sio suluhisho..
Suluhisho ni kujikinga..
Wataalamu wa afya huko mahospitalini wanasema ili kujiridhisha uko salama ni sharti upime mara 3 ikimaanisha unapima tarehe 1 January 2024, utarudia tena kupima 1 February 2024, utamalizia kupima mara ya tatu 1 March 2024, majibu yakifanana basi hapo upo salama

Ila utashangaa hivi sasa Yohana na Mwajuma wamekutana kwenye Kilimanjaro Express, wameshuka Shekilango wanapitia pharmacy wananunua kipimo wanapima wanasoma -ve wanaelekea Sinza kutest mitambo
 
Back
Top Bottom