DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Kwa Muongozo upi?Wataalamu wa afya huko mahospitalini wanasema ili kujiridhisha uko salama ni sharti upime mara 3 ikimaanisha unapima tarehe 1 January 2024, utarudia tena kupima 1 February 2024, utamalizia kupima mara ya tatu 1 March 2024, majibu yakifanana basi hapo upo salama
Ila utashangaa hivi sasa Yohana na Mwajuma wamekutana kwenye Kilimanjaro Express, wameshuka Shekilango wanapitia pharmacy wananunua kipimo wanapima wanasoma -ve wanaelekea Sinza kutest mitambo
Muongozo halali wa Upimaji Ni kweli utapima at Start then baada ya mwezi mmoja then baada ya miezi mitatu au Mwaka inategemea kama hauko kwenye Hali hatarishi ya kuweza ku be exposed kwenye Maambukizi..
Upimaji wa aina yoyote Unategemea na hali ya client anayeenda kupima na hali ya Kuwa exposed na Maambukizi..
Kwa mfano Unaweza ukaja wewe mama wa nyumbani ukapima kulingana na Miongozo nikakuambia rudi baada ya mwezi kupima na baada ya mwezi nikakumbia utarudi baada ya miezi mitatu..
Hali itakuwa tofauti na yule sex Workers (Anayejiuza) au Anayeishi na Mtu mwenye maambulizi ambaye yeye nitamwambia Arudie kupima kila mwezi kutokana na exposed Status yake..
Hapo sijui umenielewa..
Upimaji wa HIV una algorism yake na mipaka yake sidhani kama kupima kila Mwezi kwa mtu ambaye hayuko Exposed inaruhisiwa..