Kwa hiyo unataka kuniambia mwizi akiiba huwa anajichoma moto mwenyewe? ni wazi kabisa kuwa bado tunaishi kwenye hasira ya Mungu na ametuahidi kwamba atatusamehe ila bado hajatenda hivyo, hapa tulipo tuna imani kuwa kuna siku Mungu, ataitupilia mbali adhabu aliyotupatia, Mungu hafananiki kwa uweza na nguvu, hivyo unapaswa kujua siku yoyote saa yoyote mungu akiamua tu kusema badi inatosha, kila kitu kitakaa sawa na hatutaona shida tena, Mungu alikuwa na uwezo hata wa kuwasamehe kina adam tangu siku ile ile waliyofanya kosa, ila sababu alipata hasira kali ndo maana mpaka sisi vizazi wa vizazi tunaendelea kuteseka kwenye ile hasira ya Mungu, ila Sio kwamba Mungu akiamua kutumalizia hizi taabu hawezi!, La hasha anaweza sana, ila bado ana hasira na ndo maana anatuahidi kuwa atakuja, tena atakuja mwanae sio yeye kuwahukumu wazima na wafu, maana inaonekana Mungu ana hasira kali mno kwetu