American nigga
JF-Expert Member
- Aug 8, 2014
- 673
- 974
Matatizo tuliyonayo tumejitakia.wenyewe na.wala hatujalaaniwa na yoyoteLaana walizopewa Adam na Hawa za kulaaniwa kwa kizazi na kizazi zilitoka kwa nani? Unapaswa kujiuliza sisi vizazi wa Adam ambao leo tunateseka namna hii Tulilaaniwa na nani? Shetani au Mungu,Tafsiri kubwa ya Mungu ni UTAWALA na si UPENDO kama tunavyoambiwa katika imani zetu, ingawa upendo ni tawi lililochanua kutoka kwenye Shina la Utawala wa Mungu....
Matatizo tuliyonayo tumejitakia.wenyewe na.wala hatujalaaniwa na yoyote
Mungu hajatulaani wala Shetani ila.tumejilaani wenyewe!
Unakiangalia jambo la adhabu kimakosa sana na hili limesababisha watu washindwe kuelewa mambo mengiEiyer nani alikwambia mtoto akifanya kosa nyumbani huwa anajipa adhabu mwenyewe? lazima huwa ni Baba au mama., kama Mungu Avyomuapia mwanamke na Mwanaume kupata shida katika maisha yao yote na Kifo juu?!! Suala la Upendo wa mungu kwa Wanadamu sikatai kama haupo ila unapaswa kujua kuwa hakuna aliye na Hasira kama Mungu sababu hasira yake kwa Adam na hawa kukosea mara moja tu ndiyo inayotupatia shida na taabu mpaka leo, tena ukumbuke kuwa makosa hatukukosa sisi ni mababu wa mababu wa mababu, kuhusu upendo wa Mungu tunaamini kama upo kiimani ila haujaonekana dhahiri, ila Hasira yake tunaiona wazi kwa kushudia kwa macho shida, mateso, vifo na Dhiki Duniani.
mleta mada. Mungu aliruhusu taifa lake teule la israel ambalo analipenda, kuangamiza mataifa mengine na Mungu kuwapa israel ardhi zao wamiliki. israel hadi leo hawamjui Mungu. kisa cha mataifa ya kando ya israel kuangamizwa ni kutomjua Mungu wa kweli na wakaabudu masanamu kwa kuwa hawakuwa na mwongozo kama waisrael ambao pamoja na kuwa na miongozo bado waliabudu masanamu ilhali kiongozi wao musa alikuwa akiwaeleza kuhusu. Mungu wa kweli. tuchambulie upendo katika muktadha huu
Sasa wewe unawezaje kumzungumzia Mungu bila kuijua biblia? Kiukweli sikwambii imetoka wapi maana nilijua unajuaHili umelitoa wapi?
Inaonekana hujaelewa swali langu lengo lake..Sasa wewe unawezaje kumzungumzia Mungu bila kuijua biblia? Kiukweli sikwambii imetoka wapi maana nilijua unajua
Mkuu nilifanya makusudi. Kwa namna ulivyoandika mwanzo sikutaka kujipa shida kuweka vifungu kwani nilijua yote haya unayo akilini na moyoni. Kwa wepesi ni kuwa ukisoma Agano la Kale tangu Kutoka hadi Waamuzi ndio utajua mapanzi ya Mungu juu ya Waisraeli na namna alivyowachukia mataifa ya kando kwa kuwa hawakuwa wakimwabudu yeye Mungu wa kweli. Sasa hofu yangu ni kuwa sitapata majibu niliyokuwa natarajia, ila nitakuwekea kifungu specific cha biblia na kwa upeo wako juu ya upendo ujaribu kunijibu swali langu la awali kabisa.Inaonekana hujaelewa swali langu lengo lake..
Nimekuuliza hayo uliyoandoka ulipoyatolea,kama ji kwenye Biblia ulipaswa kunijibu na kuniwekea na ushahidi halafu tungeanzai hapo,sijui ni kwanini huwa hamtaki kujibu maswali ....!!
mleta mada. Mungu aliruhusu taifa lake teule la israel ambalo analipenda, kuangamiza mataifa mengine na Mungu kuwapa israel ardhi zao wamiliki. israel hadi leo hawamjui Mungu. kisa cha mataifa ya kando ya israel kuangamizwa ni kutomjua Mungu wa kweli na wakaabudu masanamu kwa kuwa hawakuwa na mwongozo kama waisrael ambao pamoja na kuwa na miongozo bado waliabudu masanamu ilhali kiongozi wao musa alikuwa akiwaeleza kuhusu. Mungu wa kweli. tuchambulie upendo katika muktadha huu
Mkuu nilifanya makusudi. Kwa namna ulivyoandika mwanzo sikutaka kujipa shida kuweka vifungu kwani nilijua yote haya unayo akilini na moyoni. Kwa wepesi ni kuwa ukisoma Agano la Kale tangu Kutoka hadi Waamuzi ndio utajua mapanzi ya Mungu juu ya Waisraeli na namna alivyowachukia mataifa ya kando kwa kuwa hawakuwa wakimwabudu yeye Mungu wa kweli. Sasa hofu yangu ni kuwa sitapata majibu niliyokuwa natarajia, ila nitakuwekea kifungu specific cha biblia na kwa upeo wako juu ya upendo ujaribu kunijibu swali langu la awali kabisa.
1. Kumb 7: 6-9
2. Kumb 7: 1-4
Soma vyema.
Sawa nimekuelewa ....
Kwanza Mungu hakuyaangamiza hayo mataifa bali Waisraeli ndio waliofanya hivyo
Pili,sababu ya Waisraeli kupigana vita na hayo mataifa saba sio kwasababu ya hayo mataifa kutomjua Mungu bali ni kwasababu Waisraeli walikuwa wamepewa ardhi ile na Mungu
Sasa kwa mkabala huu swali lako limekosa maana labda ulijenge upya!
Unakiangalia jambo la adhabu kimakosa sana na hili limesababisha watu washindwe kuelewa mambo mengi
Ninapokosea na kuadhibiwa kimsingi adhabu ile ninakuwa nimeileta mimi yule anaetamka anakuwa anaiwakilisha tu
Unapokwenda kuiba na unajua kabisa kuiba ni kosa halafu ukapelekwa mahalamani hakimu anakueleza adhabu ya kosa lako kwa mujibu wa sheria na sio yeye anaekuhukumu
Sheria imetamka adhabu la kosa lako na unajua,unapoamua kutenda kosa unajiadhibu mwenyewe kwasababu ulitenda bila shuruti
Kwa hiyo unataka kuniambia mwizi akiiba huwa anajichoma moto mwenyewe? ni wazi kabisa kuwa bado tunaishi kwenye hasira ya Mungu na ametuahidi kwamba atatusamehe ila bado hajatenda hivyo, hapa tulipo tuna imani kuwa kuna siku Mungu, ataitupilia mbali adhabu aliyotupatia, Mungu hafananiki kwa uweza na nguvu, hivyo unapaswa kujua siku yoyote saa yoyote mungu akiamua tu kusema badi inatosha, kila kitu kitakaa sawa na hatutaona shida tena, Mungu alikuwa na uwezo hata wa kuwasamehe kina adam tangu siku ile ile waliyofanya kosa, ila sababu alipata hasira kali ndo maana mpaka sisi vizazi wa vizazi tunaendelea kuteseka kwenye ile hasira ya Mungu, ila Sio kwamba Mungu akiamua kutumalizia hizi taabu hawezi!, La hasha anaweza sana, ila bado ana hasira na ndo maana anatuahidi kuwa atakuja, tena atakuja mwanae sio yeye kuwahukumu wazima na wafu, maana inaonekana Mungu ana hasira kali mno kwetu