'Rhetorical question' ulilouliza ndilo sahihi kuanzia wakati wa kujadili Muungano wetu. Serikali ya Tanganyika ilikufa. Vipi serikali ya Zanzibar isife tukawa na serikali moja tu? Hatusemi Zanzibar imezwe na Bara (kwa kuwa hakuna Tanganyika); au Bara imezwe na Zanzibar. Hoja ni kuwe na nchi moja inayoendeshwa na serikali moja. La sivyo, tuwe na serikali tatu: ya Visiwani, ya Bara, na ya Muungano. Hivi sasa Rais na mawaziri wa Muungano wanaweza kutoka Zanzibar, kwa kuwa nchi ni moja. Lakini hakuna mtu wa Bara anayeweza kuwa Rais, au waziri au hata Mbunge tu wa Zanzibar!
Hivi karibuni Zanzibar ilitangaza masharti ya kununua ardhi nchini Zanzibar kwa wageni; ikafafanua kwamba masharti hayo yanawahusu Raia wa Bara pia. Pamoja na yote hayo, bado kuna Wazanzibari wanaolalamika kwamba Bara inainyonya Zanzibar! Jee, kuna ukweli hapo?