Ni kweli mwanamke hawezi kumpenda mwanaume fukara?

Ni kweli mwanamke hawezi kumpenda mwanaume fukara?

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Naombeni mnipe majibu, ni kweli mwanamke hawezi kumpenda mwanaume fukara? Lakini mbona baba yangu alipendwa na mama yangu akiwa hana kitu, mimi nimezaliwa mpaka nafikia umri wa kujitambua nimekuta baba yangu anaishi kwao, yaani kwenye nyumba ya wazazi wake nayo ilikuwa chumba kimoja na sebure.

Lakini mbona ndoa za uswahili asilimia kubwa zinadumu ukilinganisha na zile za ushuwani? yaani unakuta mtu anaishi na mke wake wamepanga chumba kimoja na wanaishi maisha ya kuungaunga Lakini wanadumu wanazaa watoto wanafanikiwa kujijenga na kuwa na makazi yao.

Lakini mbona mwanamke huyohuyo unaweza kumpa kila kitu na bado akaenda kumpa penzi fukara?
 
Naombeni mnipe majibu ...ni kweli mwanamke hawezi kumpenda mwanaume fukara? Lakini mbona baba yangu alipendwa na mama yangu akiwa hana kitu, mimi nimezaliwa Mpaka nafikia umri wa kujitambua nimekuta baba yangu anaishi kwao, yaani kwenye nyumba ya wazazi wake nayo ilikuwa chumba kimoja na sebure.... Lakini mbona ndoa za uswahili asilimia kubwa zinadumu ukilinganisha na zile za ushuwani? yaani unakuta mtu anaishi na mke wake wamepanga chumba kimoja na wanaishi maisha ya kuungaunga Lakini wanadumu wanazaa watoto wanafanikiwa kujijenga na kuwa na makazi yao... Lakini mbona mwanamke huyohuyo unaweza kumpa kila kitu na bado akaenda kumpa penzi fukara?
Wakati wanapendana ulikuwepo?
 
Lakini mbona mwanamke huyohuyo unaweza kumpa kila kitu na bado akaenda kumpa penzi fukara?
Mkuu vijana wa sasa wamekosa kitu kinaitwa MASCULINITY.

Wazee wa zamani walikuwa Masculine, ndio maana walikuwa hawana hela na bado waliweza kuwatuliza wake zao.

Mwanamke anapenda Mwanaume yeyote, uwe Fukara au Tajiri.
 
Kijana,

Kuna mabinti upendo wao haupo katika vitu, sio jambo la kustaajabisha fukara kupendwa….japo kwa miaka hii mambo n tofauti sana, tuseme ukweli bila kupepesa macho!

Ili binti avutiwe na wewe, anataka aone una nini zaidi ya hyo muonekano! Vingnevyo umekwisha
 
DDF878AA-6BDE-4AF5-9A86-025658D0C854.jpeg
 
Back
Top Bottom