Ni kweli Papa Wemba kauawa na sumu iliyowekwa kwenye Mic?

 
Jamaa hakujishughulisha na Papa Wemba kwa sababu si daktari na aliiondoa hiyo mic kwa sababu aidha ingendondoshwa na kumuangukia mgojwa ama wanaotoa huduma. Labda ni hivi kuna jamaa mmoja aliiba hapo mgodini Bulyanhulu ndani na akaanza kukimbia na kuruka uzio,walioko nje (watu wamekuja kuomba kazi) mmoja wao akamkimbiza na kumkamata hadi walinzi wakafika kumkamata mwizi wao,kilichofuata hata aliyemkamata alikamatwa kwa vile sheria za mgodi haziruhusu mtu ambaye hana mafunzo ya uasikari kukamata mtuhumiwa. Kule kwenda ananyata kubadiri hiyo mic alifanya vile ili asiharubu pozi la Papa Wemba wakati anaimba ni sawa na kukatiza mbele ya raisi akiwa anahutubia ndiyo sababu hata wapiga picha huonekana wakitembea kwa kuinama na taratibu pasipo kutoa kelele. Hata mimi au wewe siku tukifa, huku ndugu watabaki na maneno kibao mara umelogwa hata kama tutachomoka kwa ajali ama ngoma.
 
Uko sawa PW alienda kupeform akitokea Congo,hali yake haikuwa nzuri kabisa na wataalam wasingemruhusu km ingakua ni France ama ughaibuni.
ubishi wetu waswaz na kujali sana mitishamba unatuponza sometime,kiukweli kabisa hakutakiwa hata awepo maeneo hayo,ukiskiliza akiimba pia utaona sauti inavyotetemeka na haiko sawa,kuna mahali imebidi akatishe verse ili sebene lipigwe.na sebene linaanza ndipo akaanguka.huyo mbadilisha mike ye anahangaika kurekebisha mike amuokoe bosi wake kuficha soo.PW hakutakiwa kuimba pale siku hiyo,alikua mgonjwa hoi kalazimisha tu.
 
Ila kuhusu huyo mtuhumiwa mimi sijaona kama alikuwa anakwenda kwa kunyata. Nilivyoona ni kwamba mara ya kwanza alipokwenda kubadili mic wakati Papa anaongea alikwenda mbio mbio na kuondoka na mic. Pia baada ya Papa kuanguka jamaa alirudi tena stejini kwa kukimbia na kuondoa mic na ndipo aligeuka kidogo kuangalia alikoangukia Papa na kisha kuondoka taratibu na mic yake kuelekea alikoitoa mwanzo.

Pengine moja ya maswali ni kama mmoja wa watu wa karibu na Papa walio kwenye timu yake iweje baada ya Papa kuanguka huyu jamaa mbio zake zote zile ziishie tu kwenye kuondoa mic na kisha aondoke taratibu bila hata kusogea karibu kabisa kuona hali ya bosi wake? The guy just shied away as if he was expecting something terrible to have happened. Well, fans have blames on this guy and possibly will not back down until necropsy results have been released by the responsible doctor and made public.

Tunachokifanya kwa sasa ni speculations tu na pengine tunajichumia bure dhambi kwa kumhisi mtu wa watu kwamba kamwuua Papa kumbe pengine mwenzetu hana hatia na alikuwa akitekeleza tu majukumu yake ya kazi kwa uaminifu.

Mara nyingi kwenye vifo vya watu maarufu kama Papa Wemba kunakuwa na speculations au conspiracy theories nyingi tu. Wengi wetu mtakumbuka kuhusu conspiracy theories nyingi tena zenye hoja za nguvu zilizojitokeza baada ya kifo cha mwanamuziki Tupac hadi zingine kudai kwamba jamaa hajafa. Lakini hadi hii leo ni miaka 20 tangu kifo chake na Tupac hajawahi kuonekana akiwa hai hadi mama yake nae kaja kafariki siku mbili zilizopita bila kumwona mwanae.

Hata hivyo katika dunia ya leo yenye umimi (wivu), visasi, mapinduzi makubwa ya sayansi na pia tamaa ya pesa chochote kisemwacho juu ya kifo cha Papa kinawezekana. Muhimu tusubiri majibu ya necropsy.
 
Hivi wasaidizi hawatumiki kuwahujumu mabosi zao?

Hii kitu si kawaida,kuna kitu nyuma
 
Mbona video ainyeshi vizuri.wewe umeipata wapi
 
Wasanii wawe makini sana na siasa kwani vifo vyao vingi huletwa baada ya msanii fulani ambae ni public figure kupromote chama fulani.
 

Unajua kila jambo lina tafsiri yake, inategemea unaliangalia kwa jicho gani.
Kwa jicho la kitabibu/kiafya huenda ukawa upo sawia, lakini kuna mitazamo mingine pia.
Utakiwacho ni kupokea mitazamo mingine pia, kisha ufanye comparative analysis, na kuona mtazamo upi uko na mashiko zaidi.
 
Tukiweka pembeni nayo ya Papa Wemba, huu sasa ndio mjadala wa nguvu. Kuhusu Komba nakiona kabisa kitu kimefichika hapo, ni wajibu kichimbuliwe
Yaliyosemwa mtaani juu ya kepiteni yanatisha
 
Keshamaliza safar yake ametangulia. Kinachotakiwa wewe nikutafuta hela na kutandaza miti tuu hicho ndio kilichotuleta dunian. Ikifika sik yako hamna jins utaungana naye tu PW. Kwasasa zingatia hayo mawili hela na miti.

Life too short. R. I. P PW
 
sumu kupita kwenye liver ina depend na njia ilio tumika kuingilia mwilini...kama alikula sumu kwenye chakula basi itapita kwenye ini lakini kama aliivuta kwenye hewa basi itapita kwenye lungs then kwenye pulnamory circulation systeam hadi kwenye moyo
 
Keshamaliza safar yake ametangulia. Kinachotakiwa wewe nikutafuta hela na kutandaza miti tuu hicho ndio kilichotuleta dunian. Ikifika sik yako hamna jins utaungana naye tu PW. Kwasasa zingatia hayo mawili hela na miti.

Life too short. R. I. P PW
CC D.Trump
 
KAUAWA KIJASUSI??

KUUWAWA KIJASUSI NDIO VIPI??
 
Tukiweka pembeni nayo ya Papa Wemba, huu sasa ndio mjadala wa nguvu. Kuhusu Komba nakiona kabisa kitu kimefichika hapo, ni wajibu kichimbuliw
Keshamaliza safar yake ametangulia. Kinachotakiwa wewe nikutafuta hela na kutandaza miti tuu hicho ndio kilichotuleta dunian. Ikifika sik yako hamna jins utaungana naye tu PW. Kwasasa zingatia hayo mawili hela na miti.

Life too short. R. I. P PW
Hela na miti sio pekee vilivyotuleta duniani. Haina maana kama kutafuta hela huku tukiacha wanadamu wengine wakiwala wenzao kama simba alavyo swala porini apendavyo na kusema ni nature. Kuua binadamu mwingine ni nature? Hapana, kuishi ndio haki ya msingi
 
Keshamaliza safar yake ametangulia. Kinachotakiwa wewe nikutafuta hela na kutandaza miti tuu hicho ndio kilichotuleta dunian. Ikifika sik yako hamna jins utaungana naye tu PW. Kwasasa zingatia hayo mawili hela na miti.

Life too short. R. I. P PW
Mkuu kutandaza miti ndiyo nini? Maana kiswahili nacho kina misemo mingi. Mara kupiga miti, mara kutandaza miti mara sijui nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…